Viongozi kuweni waungwana kukubali kukosea.

Sungurampole

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2007
Posts
984
Reaction score
206
Kwa maelezo ya waziri Mh Lukuvi jana 'serikali haijawahi kusitisha tiba ya babu wa Loliondo' kila mtanzania anayefuatilia anajua huo ni uongo. Swali langu mbona tunakosa uungwana wa kukubali kuwa tumekosea na sasa tunarekebisha. Kwa maoni yangu hii ingewapa heshima zaidi na pia ingetujenga kuwachukulia serious mnapotamka jambo. Hii siyo mara ya kwanza kufanya hivi tunakumbuka matamko mengi ya nyuma- kulipwa kwa dowans ni moja mengi. Nilitarajia kama Lukuvi hapingani na waziri Mponda angeendeleza yale alianzisha Mponda kuhusu kutuma timu ya wataalamu na kuangalia kama taratibu zimefuatwa.. Badala yake Lukuvi kaja na mapya utafikiri katokea Kenya. Binafsi naunga mkono hii sura mpya ya serikali ya kuwa mwezeshaji lakini hoja yangu hapa ni mkanganyiko serikali inaowasababishia raia kupelekea kudharauliwa kwa matamko yao
 
Kutokubali kuwa tumefanhya makosa ndo kunalighalimu taifa mambo kibaompaka sasa! Angalia mikataba ya kijinga hadi sasa hakuna lokubali kuwa serikali ilifanya makosa!
 
Kwa kweli Mawaziri wa awamu hii ni makanjanja wanajishushia hadhi wanapopingana katika kila jambo kuna ukosefu mkubwa wa mawasiliano na uajibikaji wa pamoja aibu tupu
 
:lol:

Serikali hii naifananisha na wapiga ramli......tawire baba!!!!
 
Kwa maelezo ya waziri Mh Lukuvi jana 'serikali haijawahi kusitisha tiba ya babu wa Loliondo' kila mtanzania anayefuatilia anajua huo ni uongo. Swali langu mbona tunakosa uungwana wa kukubali kuwa tumekosea na sasa tunarekebisha. Kwa maoni yangu hii ingewapa heshima zaidi na pia ingetujenga kuwachukulia serious mnapotamka jambo. Hii siyo mara ya kwanza kufanya hivi tunakumbuka matamko mengi ya nyuma- kulipwa kwa dowans ni moja mengi. Nilitarajia kama Lukuvi hapingani na waziri Mponda angeendeleza yale alianzisha Mponda kuhusu kutuma timu ya wataalamu na kuangalia kama taratibu zimefuatwa.. Badala yake Lukuvi kaja na mapya utafikiri katokea Kenya. Binafsi naunga mkono hii sura mpya ya serikali ya kuwa mwezeshaji lakini hoja yangu hapa ni mkanganyiko serikali inaowasababishia raia kupelekea kudharauliwa kwa matamko yao

we chakuangalia ni kauli ya mwisho kutoka basii,kama ni ya lukuvi basi fuata cha lukuvi. mengine waachie wenyewe viongozi,,jaribu kuwashauri na wanachi wenzetu pia wasiumizwe na maswali kama yako
 
au zaidi, afuate analoona yeye linafaa, si lazima serikali itoe muongozo, je, kama muongozo wake ni mbaya ataufuata? from where we are, kila mtu na afuate nini anachoamini na uwkeli, serikali sio issue,
 
Back
Top Bottom