Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya Umoja wa kitaifa wa Zanzibar Maalim Seif,Habib Mnyaa na Diwani wa Kibaga kwa tiketi ya CUF Bwana Juma Mkumbi wametumia muda mwingi sana kuituhumu chadema kwa ubinafsi,udini na ukanda wakati walipokuwa wanawahutubia wananchi wa Singida mjini katika eneo la stand ya zamani.
Habib Mnyaa anasema kuwa CHADEMA wameshindwa kushirikiana na vyama vingine bungeni kwa kuwa chadema ni wabinafsi na wanawaonea wivu cuf kwa kuwa wapo kwenye serikali.
Aliendelea kuituhumu chadema kwa kusema kuwa walishasema kuwa nchi haitatawalika hivyo haya matukio yanayotokea hivi sasa ni matokeo ya kauli tata za chadema.Bwana Mnyaa alihoji pia uhalali wa wabunge wa chadema kutumia quatation za biblia ndani ya bunge wakati hapo zamani biblia na msahafu zilikuwa zinaingizwa bungeni wakati wa kiapo tu!
Naye Maalim Seif pamoja na kulaani yaliyotokea jana huko Arusha na kuelezea faida zilizopatikana kutokana na serikali ya umoja wa kitaifa pia alionekana kupiga vijembe kwa chadema pale aliposema "kwa sasa imedhihiri chama cha kisiasa ni kipi na chama cha kidini ni kipi"
Kabla ya Hotuba za viongozi wakuu hao wa CUF Diwani wa Kibaga aliwaambia wananchi kuwa ichagueni CUF kwa kuwa mtapatiwa ubwabwa wa uhakika kama walivyofanyiwa watu wa Kibaga walipoichagua CUF.
Alisema kuwa watu wa Kibaga walikula ubwabwa kwa siku tatu fullizo.
Pia Diwani huyo ambaye ni mzaliwa wa Singida alisema kuwa amewachangia wazee wa Ikungi magunia kumi ya mahindi maana mbunge wao amekuwa wa miongozo na vurugu bungeni badala ya kuwasaidia watu waliompeleka bungeni.
My take: CUF haina tena mvuto huku bara na hata watu waliohudhuria mkutano huo hawakuwa wengi sana.