Viongozi CHADEMA wanasurika kutekwa Mkoani Dododoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi CHADEMA wanasurika kutekwa Mkoani Dododoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Oct 13, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamenusurika kutekwa baada ya gari lao aina ya Toyota Opa lenye namba za usajili T 850 BLK, kushambuliwa na watu wasiojulikana na kuvunjwa kioo cha nyuma na kitu kizito.


  Tukio hilo lilitokea Oktoba 9, mwaka huu majira ya saa nne usiku wakati viongozi hao wakitoka katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani katika Kata ya Mpwapwa Mjini.


  Shambulizi dhidi ya viongozi hao waliokuwa katika gari hilo mali ya Eva Mpagama ambaye ni Mratibu wa Vijana CHADEMA Mkoa wa Dodoma, lilifanyika katika eneo la Mwanakianga, nje kidogo ya mji wa Mpwapwa.


  Walioshambuliwa ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo CHADEMA Taifa, Benson Kigaila, Mratibu wa Vijana Mkoa wa Dodoma, Mpagama na Kunti Yusufu ambaye ni mratibu wa akina mama CHADEMA mkoa.


  Tukio hilo liliripotiwa Oktoba 10 katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Mpwapwa, na kufunguliwa jalada namba RB/1934/2012.

  Tanzania Daima
   
 2. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Asante kwa taarifa mkuu lakini mbona picha na habari havirandani?
   
 3. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Inawabidi viongozi wa cdm wawe makini sana.
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye REd :spy::spy:
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Pole, mambo mengingine ya taswira tunaweka ili upate nafasi ya kutafakari matukio yanayotokea, kwa vyo vyote mleta mada hawezi kuweka kitu ambacho hakina kiashiria fulani na matukio yanayojilia. Kwenye picha wapo viogozi wa Serikali ambao ni kutoka CCM na viongozi wa Chadema.

  Kwenye picha wapo Kikwete, Mbowe, Slaa, Emmanuel nchimbi, Wasira na wengine, jaribu kutafakari kidogo.
   
 6. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Modesty is not necessary where struggle for survival has become necessity. I say we start a fight!
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa mkuu. Makamanda kuweni makini wanawawinda kama swala. Tumaini Makene mbona hukutuleta habari hii mkuu? Naona ni ya muda kidogo au mimi nimepitwa na wakati sikupita hapa? Tunawaombea mkomboe hii nchi tuachane na uhasama uliopo kwa sasa!! Amani imetoweka, udini, uharibifu ambao haufuatiliwi. Jana watu wameumizwa mbagala na kuchoma makanisa na bado wanasema wanaendelea huku eti tunasema tuna inteligensia!! Wapi na wapi? Kwa CDM intelligensia ndiyo ipo lakin kwa waislam kuandamana na kuleta fujo ni ghafla inteligenzia imepotea. It does not click in my mind.
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Makamanda tafadhali muwe makini. CCM ni wauawaji, msiwape nafasi kwa hali yoyote ile
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  I wish Mkuu wa Gombe angekuwa rais. Tungepata watalii wengi sana wa kuitembelea ikulu, Tanzania ingekuwa nchi mashuhuri duniani
   
 10. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona siasa imechafuka hivi hapa nchini kwetu?
   
 11. k

  kipimo JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 830
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama tu hata udiwani, unahofiwa kupotea na watu wanajua mtaji wa chama tawala ni vijijini, kuna haja ya kujitathmini hao
   
 12. Heavy equipment

  Heavy equipment JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 930
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 80
  Poleni makamanda, tulianza na mungu tutamaliza na mungu
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Mkuu Slaa hayupo kwenye picha,halafu pia hujasema ni kivipi walitaka kutekwa zaidi ya kusema tu "kitu kizito kilivunja kioo cha nyuma",wekeni taarifa zilizokamilika,especially wewe mkuu?Hujasema how,kwa mfano kama kioo cha nyuma kilipovunjwa,je waliamriwa kutoka ndani ya gari?Walijuaje/ulijuwaje kwamba walita kutekwa?what went on other than kioo kuvunjwa?duh!
   
Loading...