Viongozi CHADEMA, Vipi kuhusu bendera ya ADC?

Hmaster

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
346
86
Kwanza kabisa napenda kuanza kwa kuwapa pongezi kwa kazi kubwa mnayoifanya kusini mwa nchi yetu kwa sababu kwa kufanya hivyo tunaendelea kujihakikishia kushika dola hapo 2015.

Pamoja na pongezi hizo ningependa kujua msimamo wa CHADEMA kuhusu rangi za bendera ya chama kipya cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE (ADC) kufanana sana na za bendera ya CHADEMA.

Nakumbuka sana wakati chama hicho kinapata usajili wa muda hata msajili wa vyama vya siasa nchini mh. Tendwa aliliona na alilitolea ufafanuzi na kusema kwamba anasubiri kama ataletewa malalamiko na chama chochote alishughurikie kwa mujibu wa sheria.

Wakati usajili unafanyika vikao vya bunge vilikuwa vinaendelea na hivyo nilitegemea kwamba vitakapokwisha lingeshughurikiwa lakini hadi leo wahusika wakuu wakiwa ktk movement kusini sijasikia chochote kuhusu hilo.

Wasiwasi wangu ni endapo chama hicho kitapata usajili wa kudumu wakiwa na bendera hiyo kwamba inaweza katika nyakati za uchaguzi kuwachanganya wapiga kura na hasa wale ambao mara nyingi huangalia rangi za bendera tu na kufannya maamuzi.

NINGEFURAHI KAMA NINGEPATA UFAFANUZI JUU YA HILI; People's Power!
 
nape.jpg

Nasaidia tu ku-upload bendela ya CDM.. Mimi nachangia kwamba kwa hakika Sura iliyoko kwenye Avatar yako inafanana sana na ile ya Chair wa ADC brother Said.., embu cheki
chair.jpg
 
Upande mmoja wanaitangaza pipoz pawa lakn wakipata umaarufu itakuwa confusion kwa laymen
 
ADC imeundwa kuimaliza CDM. Hizo rangi hazijafanana kwa bahati tu, ni mpango mahsusi.

CDM ikae mkao wa kunyolewa na wanachama wajiandae kwa mshangao.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom