Viongozi acheni kulalamika chukueni hatua

bensonlifua92

Member
Dec 9, 2010
84
33
Nimesoma magezeti mengi tangu mafuriko ya Dar na mahali kwingineko, yanasikitisha sana. Zaidi ya yote nimefuatilia namna vile viongozi wa ngazi mbalimbali wanavyoshughurikia jambo hili na hata maoni ya watu mbalimbali juu ya jambo hili. Nimefanya uchambuzi wangu na nimegundua hili. Viongozi wanawalaumu wanao ishi mabondeni na wanawaagiza wahame, waondoke mabondeni. Na hata kiongozi mwingine amefikia hatua ya kuwa ambia "tunawambia muhame hamtaki kusikia" Zaidi pia raisi wetu naye anaishia kutoa kauri nyepesi sana mfano:
Rais alisema: “Wakati Watanzania tunaomba usiku na mchana mvua iweze kunyesha ili mazao yaweze kustawi, wapo wenzetu ambao wanaomba jua liwake mwaka mzima.”
“Acheni kuishi kwa mashaka, ukiona wingu jeusi unaanza hofu, kila siku adui yako wewe ni mvua, tafadhali hamieni kwenye maeneo salama yatakayotengwa,”alisema Kikwete.
Mkuu huyo wa nchi aliongeza kwamba, katika maeneo mengine mafuriko yametokea kwa sababu watu wamejenga kwenye maeneo ya wazi na maeneo ya barabara.

“Maeneo hayo yakijengwa maji yanatafuta sehemu ya kupita, yakishindwa yanabomoa nyumba na miundombinu mingine,” alisema Kikwete.Alisema yote hayo yanafanyika huku viongozi wakiwemo watendaji wa mitaa na kata, wakiwa wanaangalia.
“Watu wanajenga na kuziba barabara, wengine wanajenga kwenye viwanja vya wazi kuna madiwani, watendaji wa kata na watendaji wa serikali za mitaa lakini hawachukui hatua zozote,” alisema Kikwete.
Rais Kikwete alisema hata kwenye maeneo hayo yanapotokea maafa, kazi ya uokoaji inakuwa ngumu kwa sababu maeneo yote yamejengwa nyumba.Alisema serikali itahakikisha waathirika wa mafuriko hayo wanapata huduma zote za kibinadamu zinazohitajika wakiwa katika vituo vya huduma.
Kabla ya kuzungumza na waathirika hao, Rais Kikwete alikagua maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyokumbwa na mafuriko hayo kwa kutumia Helkopta. Nukuu zote ni kutoka gazeti la Mwananchi...23/12/2011
Katika haya ambayo JK amesema nina maswali mengi sana kwa kiongozi wa nchi mwenye dhamana kubwa sana ya usalama na mali ya wananchi wake. Mfano:

1. Je kama rais wa nchi anatakiwa kuwaambia watu wake waache kuishi kwa mashaka au alitakiwa kuwabana viongozi wenzake wanaosababisha kuruhusu watu kujenga mabondeni na ujenzi holela mijini na kwingineko?
2. Kama kiongozi wa nchi alitakiwa kuja kwa watu wenye msiba na mizaha ya kuwaambia watu wanaomba jua liwake mwaka mzima au kuwaambia serikali yenu ina kiasi kadhaa cha fidia kwa hasara mliyopata pia serikali yenu itahakikisha mnahamia mahala salama ambako serikali inaenda kujenga nyumba za gharama nafuu?


3.Je rais wa nchi anatakiwa kulalamika kwa maji kukosa njia ya kupita au alitakiwa kuchukua hatua juu ya wote walio chini yake waliosababisha kuwaacha wananchi hadi wajenge kwenye njia ya maji? Rais analalamika kama vile kwa muda wa zaidi ya miaka 10-15 hakuwepo nchini na sasa amerudi amekuta mafuriko na akagundua haya yote anayolalamikia!!
4. Je ni sahihi rais wa nchi kwenda kwenye tukio kama hili na kuanza naye kulalamika kama mtu asiye na mamlaka kuwa viongozi wake wa chini hawachukui hatua juu ya wote wanaojenga kiholela na kwenye njia za maji au alitakiwa kuagiza (na kusema kweli siyo sasa ila alitakiwa amekwisha agiza siku nyingi) kuwa viongozi wasiotimiza wajibu wau hawana kazi badala ya kulalamika tu?
5. Je inatosha kuwaambia watu wahame mabondeni hali rais akijua kuwa ujenzi wa makao mapya unahitaji pesa na huenda sisi wananchi wake hatuna uwezo wa kujenga hizo nyumba mara moja kama wafanyavyo mafisadi? Au bado anafikra kuwa watu wanao jenga mabondeni wanapenda kufanya hivo au anadhani yuko sahihi kusema kuwa watu wanaoishi kwenye nyumba za makuti wanafanya hivo kwa vile wanapenda kuishi kwenye nyumba hizo za makuti???
Binafsi natamani kusikia serikali imetimiza wajibu wake kwa rasilimali tunazochangia kwa kupitia kodi mbalimbali tunazokatwa ili iwahudumie watu na si tu kusikia kila kukicha jinsi mabilioni yanavyoibiwa kama hii nchi haina mwenyewe hivi!!!! Ni huzuni kubwa sana kwa watu tunaochambua mambo ungetegemea rais aje na majibu au maazimio ya nguvu na kila kiongozi angehangaika kutimiza maagizo ya rais maana kama hutimizi maagizo mema ya mkuu wa nchi utatimiza ya nani tena!!
Nadhani tuko at cross-road (njia panda) sijui tufanye nini maana dola ukiwambia hivi au vile wao wanasema uchochezi. Huenda hata haya ninayosema hapa wengine watasema ni uchochezi. Au wapo wengine wetu watayabeza tu kwasababu tunahoji ukweli fulani

Niseme tena Viongozi wetu mnadhamana kubwa ktk nchi ACHENI KULALAMIKA KAMA WATU WASIOJUA LA KUFANYA CHUKUENI HATUA MADHUBUTI KWA MASLAHI NA MAENDELEO YA TAIFA LETU
Nawasilisha
 
Hana ubavu wa kuhamisha mtu yoyote kwani wale wahanga wa gongo la mboto wameshalipwa?
Hii serikali ya kimagirini tamko lishatoka lakini utekelezaji hamna na hamna fungu la fedha kwa ajili ya hilo zezi la kuwahamisha watu.

Kwa jinsi navyoyafahamu mabonde hatarishi ya jiji la Dar tukianzia na jangwani kwenyewe pale pana wakazi wangapi?
Bonde la mkwajuni.......?
Bonde la msimbazi.........?
Tandale............?
Kigogo..............?
keko................?
yombo.......?

Na kuna maeneo mengi tu kama mvua zikinyesha basi wanakuwa katika wakati mgumu.
Nadhani kwenye sensa ya 2012 nadhani jiji la Dar linaweza kuwa na wakazi karibu milioni 8, 9 au 10

Asilimia 60 kati ya wakazi hao wanatoka humu humu kwenye mabonde, JK na serikali yako hamna mtakachokifanya zaidi ya kuongea tu na kunukuliwa katika vyombo vya habari rais nae kasema, basi imetoka hiyo.
 
Back
Top Bottom