Chadema kama Institution inahitaji kujifanyia Self Assessment maana kwa sasa inaonekana kuwa Chama ni viongozi hao wachache walio karibu na Mwenyekiti. Pasipo kuziba makovu ya uchaguzi wa ndani wa chama chenu, Mbowe na timu yake wasijidanganye kuwa kutakua na kusonga mbele. Watabakia viongozi wa majukwaani na matamko kama wanavyoambiwa. Hivi kwa nini baadhi ya hizo resources zisitumike kufanya mikutano ya hadhara ya kujitathmini? wako wapi wale maelfu ya vijana waliokua wanasukuma magari ya viongozi wakati wa kampeni ya kumnadi mgombea wao? Hivi ni kweli hawana kitu wala hisia yoyote kwa wakati huu? Kwa nini Mbowe na kundi lake hawaigi hata machache yanayofanywa na wapinzani wao? Tumeona Mwenyekiti wa CCM akiongea kwenye mkutano wao mkuu juu ya mabovu ya chama chao na kutangaza wazi kuwa vyeo kama vya Makamanda wa Vijana ( ambao ni wazee wakutupa anyway) na wenyeviti wa wenyeviti ni abomination, pasipo kujali kuwa hao waliovishika wananguvu kiasi gani ndani ya chama chao. The time has come when Mbowe and Chadema wafahamu kuwa kujifunza hakuna mwisho. Leo hii tamko la mikutano mikubwa kwa kugombea udiwani? mbona hao watu waliweza kuteka hizo nafasi pasipo nguvu za the so called the giants. Its just that kwa sisi tunaosoma sana kila habari matangazo ya Chadema ni kama an anti climax. Najua kuna wanaoweza kusema dada anatafuta kick aonekane, si kweli, tuambiane ukweli jamani hata kama sisi ni marafiki, au ndugu ili tupate kuwa bora zaidi kila siku. kwa sasa hivi tutake tusitake Chadema siyo news kwa anybody including Chadema wenyewe maana tunao mtaani na tunawasikia wanavyolalama.
..mikutano ya hadhara si imezuiwa?
..hatuwezi kudai cdm wafanye mikutano ya hadhara wakati hatukuwaunga mkono walipotangaza operation ukuta.
..pia hili tangazo limetolewa na katibu wa cdm kanda ya kaskazini. Ukumbuke cdm imegawanywa kikanda hivyo kila kanda ina uhuru ktk maamuzi na vipaumbele vyake.
..binafsi ningekuunga mkono kama ungewachagiza viongozi wa kanda nyingine nao wajizatiti ktk kampeni hizi zinazokuja.
..vilevile ungependekeza cdm kiwape resources( siyo watu) za kutosha ili kuendesha kampeni za uchaguzi mdogo.
..i dont think it is feasible kwa sasa hivi, ukizingatia ubaguzi dhidi ya wanaotoka kanda ya kaskazini, kupeleka viongozi toka kanda hiyo kwenda kufanya kampeni maeneo mengine ya Tz.
..katika uchaguzi mdogo wa kalenga cdm ilipeleka wapiga kampeni na wasimamizi toka arusha. Matokeo yakw ccm wakaanza kampeni za ubaguzi kwamba cdm haiwaamini wana iringa/kalenga.
..mwisho nakuunga mkono kwamba cdm inahitaji mawazo na mbinu mpya. Vilevile inahitaji ianze sasa hivi kutafuta a viable presidential candidate for 2020.