Viongozi 22 wa kitaifa CHADEMA kuzindua kampeni kanda ya Kaskazini

It's well and good for northerner to get first priority on manpower and funds during campaign but when it comes to demonstration, the lake zone gets the first priority!

This is CHADEMA's way of doing politics!

Yaani kata nne ambazo ziko kwenye eneo linalojulikana kama ‘’ngome ya CHADEMA’’ zinapewa viongozi 22 wa kitaifa na wabunge wakati wa kampeni. Mwingine anaweza kusema, this is favouritism and misallocation of party resources!

Mimi ninasema, uongozi wa juu wa CHADEMA umefikia kikomo kwa sababu umekosa focus na maarifa ya kukisukuma chama mbele zaidi.

Mimi naomba unisaidie ufafanuzi juu ya masuala matano yafuatayo:

1. Ni majuzi tu Mwenyekiti wenu aliyepita bwana Jakaya alisema katika mkutano wenu mkuu wa taifa kwamba CCM inahitaji kurudi kujijenga na kujiimarisha ngazi za chini, akiwa na maana kwamba chama chenu kimedhoofika. Kudhoofika huko amekuelezea mara kadhaa katika mazingira na pia lugha tofauti tofauti. Lakini Mwenyekiti wenu mpya Bw. Magufuli pia alitamka kwamba siasa za majukwaani muda wake umeshapita, wanasiasa wahamie majimboni mwao. Akaongeza kwamba mwenye mamlaka ya kuzunguka nchi nzima ni yeye tu kama Rais na Mwenyekiti wa chama tawala. Je kutozunguka kwake na kutoruhusu viongozi wenu wengine humo wa kitaifa kuzungukia wananchi maana yake ni kwamba chama chenu cha mapinduzi sasa kimeimarika? Nini ni 'KPIs' za kuimarika huko?

2. Kwa maelezo yako, Chadema imedhoofika. Lakini lengo kuu la CCM always limekuwa ni kuona - a weak opposition in Tanzania, upinzani uliokosa focus na direction. Kwa maelezo yako hilo limetimia. Sasa kama hilo limetimia, why are you still bothered kuja na thread kama hizi? Dhumuni ni nini hasa.

3. CCM ya Magufuli (kama kuna kitu kama hicho), inasimamia itikadi gani? Je ni tofauti na ile ya Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Nyerere? Itikadi hiyo inatekelezwa vipi chini ya Mwenyekiti wenu mpya Pombe Magufuli?

4. Kwanini msemaji mkuu wa chama chenu cha CCM - Humphrey polepole anapingana na sera ya chama cha mapinduzi ya kung'ang'ania muungano wa serikali mbili lakini anaendelea kubakia katika nafasi yake? Kwanini wengine wenye mtazamo huo wamekuwa wakiadhibiwa na chama chenu? Hili la PolePole, isn't that the 'position' of the 'opposition'? Mnaendaje kuuza sera ya serikali tatu ambayo ni sera ya upinzani dhidi ya sera ya CCM ya serikali mbili?

5. Tatizo lenu ni Lowassa na ilitumika nguvu kubwa sana kuelezea umma jinsi gani alivyokuwa ni mchafu na fisadi. Kwanini hadi leo hajafikishwa mahakamani na serikali ya CCM ili kudhihirishia umma kwamba fisadi tuliyemtaja mbele yenu wakati wa kampeni tumemkamata na kumfungulia mashitaka? Mwaka 2020 iwapo Lowassa atagombea tena kwa tiketi ya upinzani, mtawaeleza nini kuhusu ufisadi wa Lowassa kutochukuliwa hatua? Kumbuka kwamba ni majuzi tu kada wa CCM ambae pia ni Waziri wa Sheria na Katiba (Waziri Mwakyembe), ambae vile vile kitaaluma ni mwanasheria na ni yule yule aliyesimamia sakata la richmond, leo anasema kwamba mafisadi wamekwisha ndio maana mahakama ya mafisadi haivumi. Hasemi lolote kuhusu Lowassa na ufisadi, hasemi lolote kuhusu Pole Pole na Muungano wa serikali tatu, mfumo unaopingana na katiba ya JMT (1977) lakini pia ile ya Chenge. Hivi huko ndani mpo salama kweli?

Nisaidie na majibu/ufafanuzi tafadhali.
 
Propaganda za kijinga kama hizi peleka kwenu Bahi watakyelewa
Unataka kutuambia Chadema Ina viongozi ishirini na mbili tuu
Mbona hujaeleza sehemu nyingine zilizo na. uchaguzi je hakuna viongozi waliokwenda?

Very childish usidhani utaibomoa CDM kwa karata za ubaguzi kama mlivyofanya NCCR na CUF
 
Tutajitokeza kwa wingi ili kumshangaza Gambo kuwa vitendo vyake anavyomtendea lema vinawachukiza wananchi
Kujitokeza kwenye mkutano ni haki yako ya msingi lakini kuwaweka wananchi wote katika fikra zako sio haki yako.
 
kwan huu uko huko 2 kaskazn? mm mwanaharakati wa mabadiliko lkn kwa huu utaratibu sio mzr sana,viongoz wote kujaa huko kaskazn il hal dodoma,ruvuma irnga na maeneo mengne upinzan uko week huko ndo mlipaswa kupeleka nguv nying kuliko huko kaskazn ambako tayar upinzan umekubalika! ndg Mbowe pitia jf uone watu wanavyokoment juu ya chama cdm na ukawa kunakoment n chachu kwa uhai wa chama na ukawa kwa ujumla co kila ki2 kinachoandikwa hum n hasi kwa cdm na ukawa la hasha!

Hivi kama mtu unayejitambua unafanyiaje kazi ripoti ya upamde mmoja??? Je umeuliza kanda ya kusini viongozi wangapi wamepelekwa?? Je umeuliza kanda ya ziwa wabunge wangapi wamepelekwa??? Unapata wapi basis ya kusema tumeweka nguvu kubwa kaskazini eti kisa wabunge 22 wakati tuna wabunge zaidi ya 70....
Ni heri muwe na subira taarifa kamili mpate za kanda nyingine au makao makuu ndio mje na conclusion kma kuna upendeleo kaskazini ama lah.
 
Waulize watu wa lake zone!
Mkuu una heshima sana kwenye hili jukwaa hta kma tinatofautiana misimamo na itikadi ila naheshim maoni yako ILA unapoelekea unajishushia credibility yako humu jf maana unapeleka mawazo yako kwenye ukanda na ukabila ?? Really?? Thats so low of you.... hizi propaganda za kugawa watu kikabila na kikanda zinawatesa sana waganda na wakenya pia wanyarwamda naomba tusipande hiyo mbegu hapa kwetu maana gharama ya kurudisha umoja na mshikamano ni kubwa sana ambayo hta south sudan wameshindwa kabisa.
 
mikakati mibovu halafu utasikia wanalalamikia tume,kun haja gani ya kupiga kampeni''kwenu''unakobalika badala ya kwenda usikokubalika ili uuze sera na ujiwekee akiba ya baadaye ,makosa yaleyale ya kupita na helicopta wakati wengine wakikata mbunga barabarani.
Sasa kama wamekosea ccm mnalialia nin?si mfurahie,yaani mnamwambia adui mbinu ya kutumia!
 
safi sana,kaskazini wanajitambua na watakuwa mbele daima.hiki ni kipindi cha sikukuu na watu wengi wapo kwao vijijini kwa ajili ya mwaka mpya na wanachama wa huko wameona ni vizuri kuwatumia viongozi wao wenye ushawishi katika maeneo yao,nawapongeza kwa hilo na kila la kheri
 
Viongozi 22 wa kitaifa wa Chadema wanatarajia kushiriki uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne za mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro kuanzia kesho.

Kampeni hizo zitazinduliwa kwenye Kata ya Duni, mjini Babati ambako chama hicho kimemteua Ally Muhidini kugombea udiwani.

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema watazindua kampeni kwa kila kata ikiongozwa na viongozi wa kitaifa na wabunge.

Golugwa amesema wabunge 22 wa Chadema Kanda ya Kaskazini wamepangwa kusimamia kata hizo na kwamba wanne watakuwa katika kata moja. Pia, madiwani 352 wa chama hicho katika kanda hiyo watashiriki kwenye kampeni.

“Tumejipanga kushinda kata zote, katika uchaguzi uliopita tulishinda kata moja tu kati ya hizi nne,” amesema.

Golugwa amesema uzinduzi wa kampeni kwenye kata nyingine tatu utatangazwa baadaye. Hata hivyo, amesema wameshaanza kampeni za nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha Januari 22 wanashinda viti hivyo.

CHANZO: Gazeti la Mwananchi
Hii nayo habari ya kuletwa hapa??Rubbish!!
 
Chadema kama Institution inahitaji kujifanyia Self Assessment maana kwa sasa inaonekana kuwa Chama ni viongozi hao wachache walio karibu na Mwenyekiti. Pasipo kuziba makovu ya uchaguzi wa ndani wa chama chenu, Mbowe na timu yake wasijidanganye kuwa kutakua na kusonga mbele. Watabakia viongozi wa majukwaani na matamko kama wanavyoambiwa. Hivi kwa nini baadhi ya hizo resources zisitumike kufanya mikutano ya hadhara ya kujitathmini? wako wapi wale maelfu ya vijana waliokua wanasukuma magari ya viongozi wakati wa kampeni ya kumnadi mgombea wao? Hivi ni kweli hawana kitu wala hisia yoyote kwa wakati huu? Kwa nini Mbowe na kundi lake hawaigi hata machache yanayofanywa na wapinzani wao? Tumeona Mwenyekiti wa CCM akiongea kwenye mkutano wao mkuu juu ya mabovu ya chama chao na kutangaza wazi kuwa vyeo kama vya Makamanda wa Vijana ( ambao ni wazee wakutupa anyway) na wenyeviti wa wenyeviti ni abomination, pasipo kujali kuwa hao waliovishika wananguvu kiasi gani ndani ya chama chao. The time has come when Mbowe and Chadema wafahamu kuwa kujifunza hakuna mwisho. Leo hii tamko la mikutano mikubwa kwa kugombea udiwani? mbona hao watu waliweza kuteka hizo nafasi pasipo nguvu za the so called the giants. Its just that kwa sisi tunaosoma sana kila habari matangazo ya Chadema ni kama an anti climax. Najua kuna wanaoweza kusema dada anatafuta kick aonekane, si kweli, tuambiane ukweli jamani hata kama sisi ni marafiki, au ndugu ili tupate kuwa bora zaidi kila siku. kwa sasa hivi tutake tusitake Chadema siyo news kwa anybody including Chadema wenyewe maana tunao mtaani na tunawasikia wanavyolalama.
Ninakubaliana na angalizo lako ambalo msingi wake ni siasa za kitaifa kwa faida ya taifa.
 
Cha zaidi ni ufujaji wa mali za chama tu!! Viongozi 22, madiwani 350+ nk. Hapo per diems zao zikoje!? Si ajabu wakatumia chopper, ukiacha mashangingi watakayotumia!!!

Hiki chama kijitafakari sana, haiwezekani chama hakina hata jengo la makao makuu, kinaishi kwenye pagale kinamisuse resources namna hii eti kwa ajili ya madiwani tu na wanachama wanakichekea!!!
Nimeshangazwa sana na uamuzi huu!
 
Back
Top Bottom