Vioja vya polisi, dawa ni kubadili mfumo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vioja vya polisi, dawa ni kubadili mfumo!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by siyabonga, Sep 9, 2012.

 1. s

  siyabonga Senior Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika sasa inazidi kuwa wazi kuwa polisi wa Tanzania wanatia aibu.

  Aibu iliyofichuliwa na gazeti la Nipashe leo, utagundua kuwa kumbe tatizo ni kubwa zaidi. Hawaishii tu kuvuruga mikutano ya kisiasa na kuua raia. Lakini pia ni sehemu ya mtandao wa uhalifu na uharamia.

  Hao waliokamatwa huko Bandarini wakiiba shaba ya Zambia, kwa mujibu wa Nipashe la leo, ni aibu kubwa ndani na nje ya Nchi. Hii imekaa vema kwa sababu hata Waziri husika wa Uchukuzi, Mwakyembe, ameshuhudia.

  Kumbe tatizo ni kubwa zaidi. Dawa ni kubadili mfumo mzima, kuanzia ajira, mafunzo, uteuzi, utendaji kazi na kuwa na chombo huru cha kusimamia Polisi.
   
 2. Timoso

  Timoso Senior Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mfumo utabadilika kwa kutumia kura yako tu.. otherwise tutangojea sana. Sehemu nyingine uvumilivu ulipowashinda walitumia nguvu ya umma kubadili mfumo.
   
 3. k

  katalina JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo letu watanzania ni wepesi wa kusahau, hilo mbona cha mtoto. Kuna EPA, Watu wamechanga fedha kupitisha bajeti................etc
   
 4. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hivi sasa tunashuhudia kasi ya ajabu ya vyombo vya dola mathalani polisi na jwtz ya wizi,juma lililopita tuliambiwa wizi wa polisi pale bandarini dar,jana tumesikia wizi wa jwtz.Kwa mtazamo wangu nchi hii kwa sasa, masikini hawana chao hivyo tunahitaji mtu ama watu watakao rudisha moyo ule wa kutojilimbikizia mali miongoni mwa umma,watu ama mtu atakaye punguza gap kati ya matajiri na maskini,mtu ama watu watakao ondoa nyimbo mbaya za kupambana na maovu badala ya kutenda kwa mfano nyimbo za rushwa,wizi wa mali za umma,ubinafsi na kulindana eg.haiwezekani hata siku madiwani na wabunge wa chama tawala hawawezi kwenda kinyume na serikali hata kama kuna madhambi na uonevu dhidi ya masikini.

  Masikini ambao ndio wengi,wanatumika kifisadi eg.wanapewa sh.2000,1000 au sh.500 katika chaguzi kwa kuchagua viongozi mbalimbali.TUNAHITAJI KUFANYA MAPINDUZI YA KIJAMII[Social Revolution]ili kurudisha ari za kupenda masikini kama ilivyo asisiwa na waasi wa taifa hili.Watanzania tusitegemee asilani kundi ama kikundi cha watawala ama mataifa mengine kubadili hali ya jamii ya watanzania kwani makundi haya yana manufaa na sera zao za kukandamiza masikini.

  NI MUDA MREFU KWA MIAKA MINGI TANZANIA IMEPOTEZA FURSA YA KUWAINUA MASIKINI BADALA YAKE MATAJIRI WA KWELI[WENYE KUJALI MASIKINI]WAMEPUNGUA NA SASA WAMEIBUKA MATAJIRI WENGI WABINAFSI NA WALAFI AMBAO WANACHOCHEA MOYO WA UTAJIRI HARAMU MIONGONI MWA KADA MBALIMBALI,Mathalani mtu anahitaji anapoanza ajira yake awe na uwezo wa kununua tv,kitanda,gari,na maisha ya raha[kujirusha],sikatai fikra hizo,la hasha! Bali kwa sababu ya kudidimia kwa tawala za jamii.HIVI SASA HAPA TZ SIYO JAMBO LA KUSHANGAA KUONA WAHALIFU WAKILINDWA AMA KWA SABABU NI WATAWALA WENYEWE[RULING ORGANS],AMA NI MTANDAO WA UTAJIRI HARAMU.

  MWISHO,BILA KUJALI ITIKADI AU MITAZAMO,WATZ TUUNGANISHE NGUVU ZA UMMA KWA PAMOJA ILI KUBADILI MFUMO TAWALA UNAOKULA UTAJIRI WETU NA NCHI WAHISANI.NDUGU ZANGU WANAJF,HAYA NI MAWAZO YANGU TU,KAMA TUPO PAMOJA TUCHANGIE CRITICALLY.
   
 5. i

  iseesa JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  KUMBUKUMBU: Miaka ya 70 Hayati Baba wa Taifa alilivunja Jeshi la Polisi na Kuliunda Upya kwa kuingiza wasomi wengi waliosoma Sheria kwenye jeshi hilo. Muda unavyopita hata wasomi hao wamekuwa mafisadi na "watovu wa Sheria"!!. Sasa ni wakati Muafaka wa kuliunda tena Upya. LAKINI....Dhaifu hawezi kufanya hivyo labda ANGELIKUWA Mh LOWASA mwenye maamuzi. TAFAKARI
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,904
  Likes Received: 2,332
  Trophy Points: 280
  Sasa imedhihirika kuwa ujambazi na uhalifu mwingi unaotokea nchi ni kazi au tender za watu katika jeshi letu la Polisi.

  Kwa mtaji wa matukio tuliyoyaona hivi karibuni, tofauti kati ya jambazi na Polisi ni ndogo sana.
  Mauaji ya wananchi pale Arusha,Migodini,Morogoro, utekaji wa Dr Ulimboka, mauaji ya mwandishi wa habari Mwangosi, hivi vimekuwa vielelezo tosha kuliogopa jeshi hili kama ukoma.

  Malalamiko ya mauaji ya kisirisiri na hata wazi wazi kama yale ya wafanyabiashara wa madini jijini Dar es salaam inaifanya nibadili msimamo wangu juu ya hawa "wana usalama".

  Funga kazi ni matukio ya mwisho wa wiki ambapo vijana wa Polisi wanatengeneza "dili" la kuiba mali za watu, badala ya kuzilinda.
  Mbaya zaidi baada ya kukurupushwa na kuzidiwa kete na vijana walinzi wema, wanamteka nyara huyo kijana- kufuatana na habari alizotoa kamanda Kova.
  Naamini hao waliomteka askari huyo mwema ni Polisi vile vile wanaotaka kupotosha kesi yenyewe dhidi ya wenzao.

  Kama tulivyo zoea sasa hakuna wa kuchukua hatua, na katika kesi hizi hakuna wahalifu-Polisi hawawezi kujifunga wenyewe.

  Ushauri wa bure UKIONA POLISI UJUE AIDHA NI JAMBAZI AU POLISI KWELI-hata hivyo kimbia sana, si watu wema hao!!
   
 7. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,395
  Likes Received: 3,721
  Trophy Points: 280
  Ni sawa na mganga wa kienyeji na mchawi, wotete ni walewale
   
 8. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama polisi hawana umuhimu wowote,kwani usalama uliopo ni matunda yao.
  Mabaya machache yanayo tokea yasifanye tusahau mazuri mengi wanayo tenda.
   
 9. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ndugu hebu tutajie hayo mazuri mengi... tuone kama wewe siyo kakova
   
 10. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Nawafahamu polisi kadhaa in person wengi wao nikikutana nao anga mbaya wakanambia kimbia ntasimama na wakinambia simama ntatimua mbio,hawafai kuaminiwa hawa
   
 11. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,694
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Asilimia 90 ya police wamekondeana, don know why
   
Loading...