Bususwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2021
- 429
- 1,011
Serikali mko wapi? TBS na TFDA mko wapi?
Kwanza kabisa naomba kusepa kwamba sisi Tanzania tumekua watu wa ajabu sana, kuanzia watu waliosoma na wasiosoma, wenye dhamana yakulinda afya zetu ndiyo wamekua watu wa ajabu zaidi kabisa!
Naomba niende kwenye mada moja kwa moja,
Hapo zamani tulikuwa na kinywaji cha kuongeza nguvu kijulikanacho kwa jina la Red Bull tu na hiki kinywaji kilikua kama kinywaji cha watu wenye kipato cha juu, maana bei ya Red Bull ni bora ukapiga zako bia aina ya Serengeti 2 au Castle lite 2 kwa Mangi kwa bei ya Tshs 1,500/= tu, na bado unabaki cha bakaa ya kununua chupa moja ya maji badi, na unabaki na nauli ya daladala kuweza kukurudisha nyumbani.
Sasa hivi kuna hivi vinywaji vya kuongeza nguvu vimejaa mtaani nyingine hata hazieleweki zinatoka wapi;
1. Azam Energy
2. MO Extra
3. Jembe Energy
4. Kung Fuu
5. MO Fire
Na nyingine nyingi ambazo tunaziona tu huko mtaani zinauzwa.
Pia hapo zamani tulikua na hizi pombe kali (yaani spirits) chache sana kama nitakua sahihi kulikua na Konyagi tu, baadae zikaje hizi K Vant, Vodka, Vladimir na Zed na nyingine nyingi, lakini sasa hivi kuna spirits nyingi mno, yaani hadi majina mengine huwezi hata kuyajua! Naomba twende kwenye matatizo ya hizi pombe kali na hizi spirit sasa.
Tuanze na Spirit
Vijana wengi sana wanakunywa hivi vinywaji kuanzaia asubuhi na mapema kabisa, kijana anaanza kulewa asubuhi na mapema je, ataanda kujenga taifa lake saa ngapi? Atapata muda wakuzalisha nakuweza kupata pesa kwa ajiri ya mahitaji yake saa ngapi? Hapa kuna shida, matokeo yake vijana wanaanza kuwa panya boi tu huko mtaani.
Madhara ya Spirit
- Vijana kulewa mapema nakuacha kufanya kazi za ujenzi wa taifa letu la Tanzania.
Kwenye hizi energy drinks hapa napo kuna shida sana, vijana asubuhi na mapema wanapiga vinywaji vya kuongeza nguvu na wanaingia kuendesha vyombo vya moto hasa boda boda na magari ya abiria, hivi kweli wataendesha kwa umakini?
Madhara ya energy drinks;
- Mapigo ya moyo kwenda mbio.
- Kukosa usingizi kwa muda.
Nini kifanyike?
Tuweke bei kubwa kwenye hivi vinjwaji ili vijana washindwe kumudu kununua. Mfano wangapi wanatumia Red Bull au Windhoek, hii itasaidia kuliponya taifa.
Mfano boda boda achanganye energy drink na gin, si ataendesha boda bila kufata sheria na matokeo yake anapata ajali nakufa au kuwa na kilema cha kudumu?!
Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app