Unaposema kipi ni kizuri una maana gani?, maana hayo ni makampuni 2 tofauti. Ninachoweza kuchangia hapa ni kuwa Startimes wako kwa mgongo wa TBC hivyo kwa channel za Bongo utapata TBC 1&2 Channel Ten na Sibuka (hii ni mpya), ila kuna channel nyingine nyingi za nje. Kwa upande wa Ting wao ni kwa mgongo wa AGAPE TV, mbali na Agape utapata pia Local channel karibu zote za Bongo. Pia nao wanazo channel za nje nyingi tu. Kwa upande wa service, nafikiri si mbaya hasa kwa kulinganisha na viwango vyetu.