Mh. Nyerere, Mbunge wa Musoma Mjini (CHADEMA) amewakemea makada wa CCM wa Musoma mjini kwa kitendo chao kiovu, cha kuwashawishi wafanyabiashara katika soko kuu la Musoma Mjini wasipishe ukarabati wa soko hadi watakapolipwa fedha ya faida ya siku kwa siku zote watakazokuwa hawapo.
Ushawishi kama huu wa kuzuia shughuli za maendeleo ni hujuma kwa wananchi,ni jinai na pia ni kukosa uzalendo alisema mbunge huyo. Aliongeza kwamba kama wameshindwa siasa wasililete uchochezi na badala yake wakafanye kazi ili waweze kuzitunza familia zao. Ikibidi wakigeuze chama chao kuwa SACOS kinaweza kuwasaidia wananchi zaidi kuliko propaganda uchwara wanazopiga sasa.