Vinasaba vyaonyesha Waingereza walikuwa weusi

Vinasaba vyaonyesha Waingereza walikuwa weusi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,672
Utafiti wa vinasaba unaonyesha hivi ndivyo Mwingereza wa zamani alivyokuwa. Alikuwa na ngozi nyeusi na nywele nyeusi zenye kujipindapinda. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika mabaki ya mifupa ya mtu yaliyoitwa Cheddar Man aliyefariki miaka 10,000 iliyopita. Mabaki hayo kaili ya binadamu ndiyo ya zamani zaidi kupatikana nchini Uingereza.
UCHUNGUZI wa vinasaba (DNA) uliofanywa karibuni umeonyesha kwamba Mwingereza aliyeishi miaka ipatayo 10,000 alikuwa na ngozi nyeusi, macho ya bluu na nywele nyeusi, ndefu zenye kujipindapinda.
Utafiti huo ulitokana na mabaki ya fuvu na mifupa kamili ya binadamu aliyekufa miaka 10,000 iliyopita aitwaye Cheddar Man ambavyo vilichimbuliwa eneo la Cheddar Gorge, Somerset, Uingereza, mwaka 1903 na ambapo mabaki hayo yanasemekana kuhusiana kinasaba na mtu mmoja kati ya kumi nchini Uingereza leo.

Mabaki kamili ya Cheddar Man yaliyofanyiwa utafiti.
Vipimo vilivyochukuliwa vinaonyesha kwamba asilimia 76 ya mtu huyo wa Cheddar, alikuwa mtu mweusi ambapo inaonyesha pia kwamba wakazi wa visiwa vya Uingereza, walikuja kupata ngozi nyeupe baadaye kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Fuvu la Cheddar Man lililofanyiwa uchunguzi mkubwa zaidi.
Wakati wa Cheddar Man anafariki, idadi ya watu nchini Uingereza ilikuwa ni 12,000 ambapo vinasaba vya mtu huyo leo hii vimepatiana katika nchi zingine za Ulaya huko Hispania, Hungary na Luxembourg.
Waingereza wa leo wakijilinganisha na Mwingereza aliyekuwepo miaka10,000 iliyopita.
Wanasayansi wanasema pia kwamba mababu wa Cheddar Man waliingia Uingereza kupitia Mashariki ya Kati baada ya kuondoka barani Afrika.
 
Hivi unaweza bashiri rangi ya macho kwa kutumia DNA... wow!!
I love science.
 
Hii ni habari njema kwa dada zetu wapenda uzungu, nawasihi wakaze buti tu kujichubua na kuvaa mawigi huenda ndani ya miaka 50 ijayo Tz ikawa ya wazungu kama Uingereza.
Ila hofu yangu kwa wale meno ya Bariadi na Kilimanjaro hawawezi badilika na kuwa wazungu-hawa watabaki kuwa weusi tu
 
mungu akamuuliza.kaini,yu wapi nduguyo?

kaini akajibu kwani umeniweka kua mlinzi wake.

mungu akamwambia damu ya ndugu yako inakulilia aldhini kuanzia sasa huta lima wa kuvuna.

kaini akasikitika na akasema,mbona umenipa adhabu kubwa hivyo!naomba nifanye nienda mbali na hapa.

mungu akamluhusu kuondoka,

kaini akahoji tena ,sasa huko niendako si wataniua?

mungu akamwambia nitakuweka alama na hakuna atakae thubutu kukua na atakae kuua atakufa mala7 yako.

kwahiyo wazungu ote ni ukoo wa kaini.wamepewa laana baada ya tabia yao ya kutuua na wamepelekwa kwenye bara lisilokua na maliasili wala rutba kwa kilimo na kwa maandiko haya ya kaini ndio yaliowafanya wazungu kuja tena kututawala na kubeba mali zetu.

wenzetu wanasoma vitabu hivi na wanapata faida hata hapa duniani ,likini sisi wachungaji wanatusomea mistari ya sadaka tu na wanajifanya kuchambua kutwa nzima.
 
Uongo, miaka 10,000 iliyopita hakuwepo mwanadamu. Hao watafiti wamepotoka au ni wajukuu wa Darwin wanaendeleza kazi ya babu yao.
 
Kwa hiyo wewe unafikiri mwanadamu alizuka mwaka gani?
Mwanadamu hakuzuka wala hakutokea tu kwa bahati mbaya. Mwanadamu ni kiumbe kilichoumbwa kwa ustadi na maarifa ya juu na Mwenyezi Mungu, Mungu wa maarifa na ujuzi. Acha mambo hayo ya kidarwin kutufananisha na sokwe. Toka uumbaji wa Adam mpaka sasa ni miaka elfu 6+
 
ukiona kizazi au jamii fulani inapigwa vita sana kujaribiwa kupotezwa ujue ndio kizazi tawala.mwafrika ni mtawala wa dunia kiasili,ndio maana kila jamii nyeupe inaogopa kuzaliana kwao.na mababu walituzaa kwakweli, si nyota ya kijani wala umati waliweza kutuzuia kuzaana.na ole wao turudie dini zetu za mizimu.na kondom zimefeli pia wamegeuza matumizi kwamba ni za ukimwi kumbe ziliundwa kudhibiti mimba.viva gozi jeusi lisilo ogopa hali yeyote ya hewa na lenye nguvu kama mashine.najivunia kuwa muafrika ila ssiipendi miongozi ya kiafrika.
 
Unajivunia kuwa muafrika au ndiyo umeshakuwa muafrika na huna jinsi? na ndiyo maana kutwa mnajifariji na story zisizo na kichwa wala miguu,badala ya kuonesha huo ubora wenu mmekazana kuambiana mlikuwa hivi mara vile.
 
ubora wangu utakuwa kwenye maisha yangu mwenyewe sio ya mtu,kila mtu na kaburi lake mkuu,kwanza mimi kisha jamii na yazungukayo.unaweza kuwa mwafrika na ukawa hupendi kuwa hivyo.mimi napenda kuwa mweusi mkulu.mwabudu mizimu original
 
Babu zake Wayne Rooney walikuwa blacks ? Hahaha
 
Back
Top Bottom