Vimemo Bandarini; Nani walikuwa wanaandika?

Vimemo Bandarini; Nani walikuwa wanaandika?

Hii inanikumbusha utetezi wa lowasa aliweka mkataba wa kinyonyaji wa Richmond kwa maelekezo ya kimemo cha mdomo.

Umeona mkuu, hiyo ndo mchezo waliokuwa wanafanya,wakati lowasa anampa maelekezo au kimemo cha mdomo Msabaha,mwisho wa siku nani wa kushika ? Kitendawili,
Cha msingi ma vimemo YAO yatatuchelewesha watajuana mwenyewe sisi tunataka kodi basi,
 
Watu kulalamika hata kisicho na kweli,
Yeye kama rais alisema waliokwepa kido waende wakalipe,majina ya watumishi waliotumia nafasi zao kusaidia watawajibishwa
So suala la vimemo aliyeandika kimemo na alikipokea watajuana sisi tunataka kodi zetu

Tufanye kwa mfano Rais au PM alimwandikia Kamishna wa kodi aondoe kontena fulani bila kulitoza jee huoni hiyo ilikuwa ni amri hata kama ilikiuka sheria? Na kama unamwajibisha huyo Kamishna wa kodi kwa kosa hilo jee hutakuwa umemwonea kama utakuwa hujamwajibisha na yule aliyetoa amri?
 
Kama ni hivyo basi juhudi hizi anazofanya na kusifiwa Mhe Magufuli zinaweza kuishia na fedheha kwake. Maana huwezi kuwa unasema unadhamira ya kupambana na ufisadi na rushwa halafu baadhi ya wahusika ukawaficha ili kuwalindia heshima huku wengine ukiwasulubu.
Tunataka MAJINA ya wote waliohusika na kuwa amuru maafisa wa TRA na Bandari kwa vimemo watende maovu.

Wewe hiyo sio dawa dawa ni kumbana tuliyempa dhamana je sheria inamruhusu kufanya kazi kwa vimemo visiofata sheria hata Kama ni cha nani? Na walitoa taarifa wakati huo? Au wslishiriki uchafuzi huo Leo ndo wanasema?
 
mzeelapa toka lini adhabu ya mlipa kodi ikawa ni kulipa ushuru?
Kisheria mtu aliyekwepa kodi anatakiwa kukamatwa, kushtakiwa na kufilisiwa mali ili kulipa fidia ya kodi aliyoikwepa Nukta.

Hiyo unayoisema ni baada ya siku 7 alizowapa,kwa kuwasaidia,
 
Last edited by a moderator:
Wahusika wanatakiwa kulipa ushuru wa makonteina yao nukta. Mambo ya vimemo, kama walivinunua au kutoa rushwa watajuana wenyewe kwani mtu hawezi kupindisha taratibu na sheria kwa vimemo.

spot on, watanzania tusiwe washabiki wa vitu visivyo na tija, sisi tunachotaka waliokwepa kodi washajulikana na sheria inasema tuwabane watulipe kodi yetu basi aliyeandika memo na muandikiwa watatafutana wenyewe uko mitaana warudishiane pesa walizopeana ili kodi yetu ilipwe tuache kushabikia vitu visicvyo na tija wala haviongez pato la tafia rais ana mambo mengi ya ku deal nayo kuliko haya tu
 
Tufanye kwa mfano Rais au PM alimwandikia Kamishna wa kodi aondoe kontena fulani bila kulitoza jee huoni hiyo ilikuwa ni amri hata kama ilikiuka sheria? Na kama unamwajibisha huyo Kamishna wa kodi kwa kosa hilo jee hutakuwa umemwonea kama utakuwa hujamwajibisha na yule aliyetoa amri?

Mkuu ukifata mchezo huo kwa wakati huu hatutafanukiwa, mfano,ukishatoa nafasi ya kusikiliza vumemo,wataesabu hayo mabilioni yanayodaiwa atasema ,nilipewa kimemo na mkapa ,kj, mkuu wa majeshi au wakuuu wa majeshi waliopita,
Utafanyaje hapo?
Kodi hazitarudi dawa ni huyo tuliyempa mamlaka yeye akafanya kazi na vimemo na hakutoa taarifa adi alipobadwa maana yake ameshiriki wizi anajua sheria zinasemaje,yeye akaonge na aliyempa kimemo watupe kodi yetu wasimtishe rais na vimemo vyao ili na wengine wajifunze,
 
spot on, watanzania tusiwe washabiki wa vitu visivyo na tija, sisi tunachotaka waliokwepa kodi washajulikana na sheria inasema tuwabane watulipe kodi yetu basi aliyeandika memo na muandikiwa watatafutana wenyewe uko mitaana warudishiane pesa walizopeana ili kodi yetu ilipwe tuache kushabikia vitu visicvyo na tija wala haviongez pato la tafia rais ana mambo mengi ya ku deal nayo kuliko haya tu

Hilo ndo la maana tukianza vimemo na vikachunguzwe kodi zetu hawatalipa au watatuchelewesha,ili siku NYINGINE ambao bado wako kwenye mtumishi hawatakubari kuingizwa mkenge wa vimemo,vinginevyo vinaandikwa na wake /mahawala wa viongozi wanagonga muhuri ndo vitupoteze muda,
 
Ingekuwa vizuri vikakusanywa ili kuwabaini walioviandika na kutambua vilisababisha madhara kiasi gani kwenye ukusanyaji kodi kisha wabanwe ipasavyo na sheria ichukue mkondo wake.

Sakata la makontena bandarini limeonyesha jinsi nchi ilivyokuwa imeoza na kuwa inapoteza fedha nyingi za umma huku nchi ikiwa inakabiliwa na ukosefu wa fedha hivyo kushindwa kuendesha huduma za jamii.

Kuna watu wazito wamepoteza kazi na wengine bado wanashighulikiwa na vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake. Lakini habari zilizopo ni kuwa mengi ya makontena hayo yalikuwa yanatolewa kwa vimemo kutoka kwa wakubwa serikalini kwa maana hiyo hao wameshiriki kuhujumu nchi kwa madaraka yao na kusababisha madhara tunayoyaona ya kukosekana kwa huduma nyingi ikiwemo madawa hospitalini iliyopelekea Watanzania wengi kufariki dunia.

Je, ni nani hao waliokuwa wanaandika hivyo vimemo? Waziri mkuu kesha pewa baadhi ya vimemo hivyo, je sasa hivi si ndio wakati muafaka wa kuweka hadharani majina ya wahusika bila kujali vyeo vyao ili tuweze kumuamini yeye na bosi wake Rais Magufuli kuwa wanayofanya sio maigizo bali ni dhamira ya kweli?
 
sakata la makontena bandarini limeonyesha jinsi nchi ilivyokuwa imeoza na kuwa inapoteza fedha nyingi za umma huku nchi ikiwa inakabiliwa na ukosefu wa fedha hivyo kushindwa kuendesha huduma za jamii.

Kuna watu wazito wamepoteza kazi na wengine bado wanashighulikiwa na vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake. Lakini habari zilizopo ni kuwa mengi ya makontena hayo yalikuwa yanatolewa kwa vimemo kutoka kwa wakubwa serikalini kwa maana hiyo hao wameshiriki kuhujumu nchi kwa madaraka yao na kusababisha madhara tunayoyaona ya kukosekana kwa huduma nyingi ikiwemo madawa hospitalini iliyopelekea watanzania wengi kufariki dunia.

Je, ni nani hao waliokuwa wanaandika hivyo vimemo? Waziri mkuu kesha pewa baadhi ya vimemo hivyo, je sasa hivi si ndio wakati muafaka wa kuweka hadharani majina ya wahusika bila kujali vyeo vyao ili tuweze kumuamini yeye na bosi wake rais magufuli kuwa wanayofanya sio maigizo bali ni dhamira ya kweli?

wewe unatuletea mambo ya vimemo hapa? Vimemo vinavyoandikwa na wake za viongozi na mahawala zao ndo vitupoteze muda,hao viongozi wa tra na bandali kuna sheria inayosema ufanye kazi na kimemo? Ilivyofanyika kwenye richmond kimemo cha maneno kutoka kwa lowasa kwenda kwa msabaha?
Huo upuuzi usisikilizwe watajuano huo na vimemo vyao sisi tunataka kodi kwa maendeleo ya wananchi basi,
 
Baraza jipya asirudi waziri yeyote wa zamani.maana ukiwachunguza wote wana majipu.mengine makubwa wengine vijipu uchungu.waapi mzee wa Kyera na wa Kaliua.kama wangekuwa waungwana wangetoa ata tamko kali kukemea uozo but where?
 
Ingekuwa vizuri vikakusanywa ili kuwabaini walioviandika na kutambua vilisababisha madhara kiasi gani kwenye ukusanyaji kodi kisha wabanwe ipasavyo na sheria ichukue mkondo wake.

Hakuna wakakusanyane wao rais anakazi nyingi sisi tunataka kodi zetu basi,
 
Hilo ndo la maana tukianza vimemo na vikachunguzwe kodi zetu hawatalipa au watatuchelewesha,ili siku NYINGINE ambao bado wako kwenye mtumishi hawatakubari kuingizwa mkenge wa vimemo,vinginevyo vinaandikwa na wake /mahawala wa viongozi wanagonga muhuri ndo vitupoteze muda,

Kwa hiyo tatizo linaweza kuendelea, kontena zitapita kwa vimemo na ikigundulika basi unamwambia alipe kodi inayotakiwa basi. Lazima kama watu walitumia madaraka yao kulazimisha sheria ipindishwe wawajibishwe sio kuachwa tuu.
Kumbuka wapo walio agiza mambo hayo yafanyike na walikuwa na mamlaka ya kuangalia ajira za hao waliowaamuru kufanya hivyo
 
Wahusika wanatakiwa kulipa ushuru wa makonteina yao nukta. Mambo ya vimemo, kama walivinunua au kutoa rushwa watajuana wenyewe kwani mtu hawezi kupindisha taratibu na sheria kwa vimemo.

Very good! Sisi tuhangaike na yule aliyeruhusu. Mambo ya nani alitoa kijimemo sisi hayatuhusu. Huyo aliyepokea kimemo na kukifanyia kazi wakati akifahamu anavunja sheria, hiyo ndo balaa kwake.
 
Kuung'oa mbuyu lazima uchimbe eneo kubwa ufuate mizizi yake.. Natamani waanze na waliokuwa na dhamana hiyo (Mawaziri na Manaibu) walikuwa wapi wakati madudu hayo yanafanyika?
 
Nadhani ni Lowassa, maana hata kwenye sakata la Richmond vimemo vyake vilitawala
 
Lakini sidhani kama container zote izo zaidi ya 2000 zimetolewa kwa memo mzee
 
Very good! Sisi tuhangaike na yule aliyeruhusu. Mambo ya nani alitoa kijimemo sisi hayatuhusu. Huyo aliyepokea kimemo na kukifanyia kazi wakati akifahamu anavunja sheria, hiyo ndo balaa kwake.

Hata kama vimemo hivyo vilikuwa maagizo (AMRI) toka kwenye utukufu wenyewe?
 
Vimemo vilitoka kwa kina Mwigulu na saada mkuya....
 
Back
Top Bottom