Vimemo Bandarini; Nani walikuwa wanaandika?

Vimemo Bandarini; Nani walikuwa wanaandika?

Sakata la makontena bandarini limeonyesha jinsi nchi ilivyokuwa imeoza na kuwa inapoteza fedha nyingi za umma huku nchi ikiwa inakabiliwa na ukosefu wa fedha hivyo kushindwa kuendesha huduma za jamii.

Kuna watu wazito wamepoteza kazi na wengine bado wanashighulikiwa na vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake. Lakini habari zilizopo ni kuwa mengi ya makontena hayo yalikuwa yanatolewa kwa vimemo kutoka kwa wakubwa serikalini kwa maana hiyo hao wameshiriki kuhujumu nchi kwa madaraka yao na kusababisha madhara tunayoyaona ya kukosekana kwa huduma nyingi ikiwemo madawa hospitalini iliyopelekea Watanzania wengi kufariki dunia.

Je, ni nani hao waliokuwa wanaandika hivyo vimemo? Waziri mkuu kesha pewa baadhi ya vimemo hivyo, je sasa hivi si ndio wakati muafaka wa kuweka hadharani majina ya wahusika bila kujali vyeo vyao ili tuweze kumuamini yeye na bosi wake Rais Magufuli kuwa wanayofanya sio maigizo bali ni dhamira ya kweli?
Huna haja kujiuliza, wewe ona tu wafaidika wa vimemo na utajua huyo " ngazi za juu" ni nani!
 
majina yao yakishapatikana wakamatwe na waunganishwe na masamaki .
 
Hata kama vimemo hivyo vilikuwa maagizo (AMRI) toka kwenye utukufu wenyewe?

Kwa mtu mwenye akili timamu na unajifahamu unatakiwa uelewe nini maana ya amri. Huwezi kuamrishwa kuua mtu eti ni amri toka juu. Huko juu ni wapi. Je kweli kuna mtu aliyepewa memo na Rais? Naamini hakuna. nafasi ya mkurugenzi wa bandari ukianza kupokea memo, unajikuta watu wengi wanajitungia memo zao kwa jina la rais.

Huko urambo kuna mbunge na waziri aliyewahi kudai sehemu ya msitu ufyekwe ili apande mimea ya kuzalisha mafuta, akisingizia ni mradi wa rais. bahati mbaya kwake alikutana na mtu anayejifahamu na kumkatalia.
 
Vibaka wa Kikwete pamoja na Kikwete mwenyewe walihusika kufoji nchi kwani wengi wao walichukua mizigo toka bandarini kwa vimemo bila kulipa kodi.
 
...ndio maana wanaitana kwenye vikao vyao vya CC...ili kuwekana sawa....JPM yeye kama kashinda urais ...basi kashinda kama jeshi la mtu mmoja....hao wengine ni wao na ccm yao....hivyo wanakutana ili angalao wawe na sauti moja..maana tayari umma wanajua kuna umbali kati ya JPM kama rais na ccm....hili lilijionesha tangu uchaguzi....hivyo sasa wanajaribu at least kuwekana karibu...
 
Wenzako wanajadiri taifa kwanza wewe vyama,lini misukule ya vyama mtabadirika na kuliweka taifa kwanza saccoss zenu badae?

Kama uwezo wako wa kuandika ndiyo huu, elimu bure haikwepeki! Kaaa!
 
Walioandika "vimemo" watatajwa na washitakiwa mahakamani wakati wa kujitetea! Baada ya hapo, ndipo nao watapandishwa kizimbani kujibu hoja za kuhujumu uchumi kwani watakuwa wametajwa kuhusika kikamilifu!
 
Ulipo pewa kazi hukusoma sheria zilizopo? Kama vimemo vimo vina ruhusiwa ndani ya mkataba wa kazi uliyopewa basi hapo hakuna haja ya kuendelea kukimbizana katika jambo hili la kukusanya ushuru. Unapo pewa kazi fanya kazi hiyo uliyo pewa. Memo memo hizo hazina kumbu kumbu na si part ya sheria za mkataba wa kazi. Ukitumiwa memo tuma memo back kwamba kinachotakiwa ni kufuata sheria za kazi. Kwasababu umepewa memo ukaue unataka baada ya kuua ashitakiwe aliyekupa kamemo ambako kesho ukiambiwa ukaonyeshe ulisha kasahau kwenye koti na bodi kashakafulia kwenye mfuko. Acheni uhuni. Subirini mtumbuliwe tu.
 
Hahaha. Wanalumumba hawataki waandika vimemo watajwe. Unajua kwa nini? Kunavuwezekani mkubwa rais mstaafu, waziri mkuu wakuu wengine ndani ya chama km kina kinana ndio waandika vimemo. Ndio maana utasikia wakisema sisi tunahitaji kodi ilipwe hatuhitaji kujua makubaliano yao ya vimemo! Hii sheria ya wapi? Aliyekwepa na aliyesaidia au kutumia madaraka yake kusaidia kukwepa kodi wote wana kesi ya kujibu!
 
Back
Top Bottom