Vimemo Bandarini; Nani walikuwa wanaandika?

Vimemo Bandarini; Nani walikuwa wanaandika?

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,948
Reaction score
74,431
Sakata la makontena bandarini limeonyesha jinsi nchi ilivyokuwa imeoza na kuwa inapoteza fedha nyingi za umma huku nchi ikiwa inakabiliwa na ukosefu wa fedha hivyo kushindwa kuendesha huduma za jamii.

Kuna watu wazito wamepoteza kazi na wengine bado wanashighulikiwa na vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake. Lakini habari zilizopo ni kuwa mengi ya makontena hayo yalikuwa yanatolewa kwa vimemo kutoka kwa wakubwa serikalini kwa maana hiyo hao wameshiriki kuhujumu nchi kwa madaraka yao na kusababisha madhara tunayoyaona ya kukosekana kwa huduma nyingi ikiwemo madawa hospitalini iliyopelekea Watanzania wengi kufariki dunia.

Je, ni nani hao waliokuwa wanaandika hivyo vimemo? Waziri mkuu kesha pewa baadhi ya vimemo hivyo, je sasa hivi si ndio wakati muafaka wa kuweka hadharani majina ya wahusika bila kujali vyeo vyao ili tuweze kumuamini yeye na bosi wake Rais Magufuli kuwa wanayofanya sio maigizo bali ni dhamira ya kweli?
 
Huu mziki ni mkubwa...vuteni pumzi ya kutosha
 
Huu mziki ni mkubwa...vuteni pumzi ya kutosha

Kuyaficha hayo majina kutaondoa maana nzima ya operesheni hiyo. Inaweza kujengeka dhana kuwa kuna watu wanaonewa na wengine wanabebwa ili kificha maovu yao.
 
huo mziki ndio mtajua kwamba,ccm ni ileile ya kulindana labda yawe majina ya wapinzani lakiini kama ni ya wana ccm itakuwa ndoto
 
huo mziki ndio mtajua kwamba,ccm ni ileile ya kulindana labda yawe majina ya wapinzani lakiini kama ni ya wana ccm itakuwa ndoto

Kama ni hivyo basi juhudi hizi anazofanya na kusifiwa Mhe Magufuli zinaweza kuishia na fedheha kwake. Maana huwezi kuwa unasema unadhamira ya kupambana na ufisadi na rushwa halafu baadhi ya wahusika ukawaficha ili kuwalindia heshima huku wengine ukiwasulubu.
Tunataka MAJINA ya wote waliohusika na kuwa amuru maafisa wa TRA na Bandari kwa vimemo watende maovu.
 
Wahusika wanatakiwa kulipa ushuru wa makonteina yao nukta. Mambo ya vimemo, kama walivinunua au kutoa rushwa watajuana wenyewe kwani mtu hawezi kupindisha taratibu na sheria kwa vimemo.
 
Nimejenga imani kubwa sana kwa Dr Jpm naamini hakuna jiwe litasalia bila kugeuzwa.
 
Wahusika wanatakiwa kulipa ushuru wa makonteina yao nukta. Mambo ya vimemo, kama walivinunua au kutoa rushwa watajuana wenyewe kwani mtu hawezi kupindisha taratibu na sheria kwa vimemo.

Nawakumbusha MKUTANO wake na sectar binafsi alisema
"WATU WALIPE KODI MAKUBALIANO YAO YALIYOKUWA YANAKIUKA SHERIA YEYE HAYAJUI ,SHERIA KWANZA MAKUBALIANO YA MAJIZI BADAE"
 
Ngoja nikae kwenye hiki kijwe naweza kupata mawili matatu ya kusimulia kwenye kinywaji
 
Kama vimemo havitakuwepo physical,huwezi kutaja mtu eti kaandika kimemo wakati hata kimemo chenyewe hakipo,
 
Wahusika wanatakiwa kulipa ushuru wa makonteina yao nukta. Mambo ya vimemo, kama walivinunua au kutoa rushwa watajuana wenyewe kwani mtu hawezi kupindisha taratibu na sheria kwa vimemo.

mzeelapa toka lini adhabu ya mlipa kodi ikawa ni kulipa ushuru?
Kisheria mtu aliyekwepa kodi anatakiwa kukamatwa, kushtakiwa na kufilisiwa mali ili kulipa fidia ya kodi aliyoikwepa Nukta.
 
Last edited by a moderator:
Kama ni hivyo basi juhudi hizi anazofanya na kusifiwa Mhe Magufuli zinaweza kuishia na fedheha kwake. Maana huwezi kuwa unasema unadhamira ya kupambana na ufisadi na rushwa halafu baadhi ya wahusika ukawaficha ili kuwalindia heshima huku wengine ukiwasulubu.
Tunataka MAJINA ya wote waliohusika na kuwa amuru maafisa wa TRA na Bandari kwa vimemo watende maovu.

Watu kulalamika hata kisicho na kweli,
Yeye kama rais alisema waliokwepa kido waende wakalipe,majina ya watumishi waliotumia nafasi zao kusaidia watawajibishwa
So suala la vimemo aliyeandika kimemo na alikipokea watajuana sisi tunataka kodi zetu
 
Hii inanikumbusha utetezi wa lowasa aliweka mkataba wa kinyonyaji wa Richmond kwa maelekezo ya kimemo cha mdomo.
 
Hapa ushauri,
Wakisikiliza vimemo watatuchanganya au kutuchelewesha kuripa kodi zetu, wao waliopokea na waliandika watajuana mwenyewe sisi hauna muda tunataka kodi yetu kwa maendeleo ya wanyonge,
 
Back
Top Bottom