Bitoz
JF-Expert Member
- Aug 27, 2015
- 30,823
- 126,552
Week end hii unaibuka kiwanja gani mwanangu ?Au hutaki tukale gambe ?
Enewea...Uswahilini sehemu kama za Kiwalani, Temeke taa nyekundu, Keko, Mwanayamala, Manzese, Mabibo, Kigogo,Buguruni kisiwani n.k kuna vitu vya kufurahisa na kuchekesha licha ya visa na mikasa lakini utapapenda!!!
1/ Kila ukoo umetoa msomi aliyefeli(ZIRO)
Karibu kila koo ya uswahilini ambayo ina wahitimu wa sekondari huwezi kosa aliyepata sifuri na kama hakuna basi utakuta ni divisheni 4 za mwisho mwisho.....Chezea St. Kayumba wewe?
2/ Kila nyumba ina biashara
Karibu kila nyumba ina mfanyabiashara mfano muuza genge,muuza karanga,mchoma vitumbua,wauza gongo n.k ukiona nyumba ipo kimya basi jua humo ndani kuna kibaka,teja au muokota chupa za plastic......Full watafutaji!!!
3/ Kuharisha siyo ugonjwa
Kutukana na kutawaliwa na uchafu wa kila aina, tatizo la tumbo la kuhara ni kitu cha kawaida mtu anaharisha siku 3 kisha laifu linaendelea kama kawa.....Kipindupindu ni rafiki yetu bwana!!!!
4/Jero tu unakula kuku
Uswahilini raha bwana ukiwa na hero tu unaonja nyama ya kuku(vishombo) kama vile utumbo, miguu, vichwa n.k...Ukiwa na buku unashiba supu ya makwasukwasu....Ni raha tu !!!
5/Babu jambazi, baba kibaka + mjukuu mwizi
Waliosema maji hufuata mkondo hawajakosea...Uswaz bhana unaweza kukuta familia nzima wamerithishana ujuzi wa kufanya uhalifu...sijui uzao wa panya road utaleta kizazi gani !!!
6/ Full vibanda umiza
Kama wewe ni shabiki wa soka na unapenda kucheki game basi njoo vibanda vya uswahilini ...kuna visa na maudhi na usipokuwa mvumilivu unaweza kuua mtu !!!
7/ Nyumba 1 watu kibao
Sio jambo la kushangaza kukuta kanyumba kadogo uswaz kamejaa wapangaji kibao...baba,mama,watoto chumba kimoja na bado kuna vita ya kugombea tundu la choo baina ya wapangaji.....Ukipiga filimbi ya mwizi idadi ya watu wanaoibuka kutoka mahomu utashangaa !!
8/ Kila siku ni week end
Uswahilini wanapenda starehe bwana asikwambie mtu,wanafunzi hawapendi shule, wazazi walevi wa mataputapu, Vijana ni mwendo wa viroba feki na ganja + unga ,Sio jambo la ajabu kuwakuta waswaz washalewa saa 2 ya asubuhi tu....Kila siku ni week end anytim !!!
9/Chimbuko la wasanii&wanamichezo
Uswaz kunaongoja kwa kutoa wasanii wakali mfano Diamond vilevile wanamichezo wengi pia wametokea uswahilini....yaani full vipaji.....Hata Bitoz anayesumbua Chit Chat ni mtoto wa Uswahilini !!!
*** Think Big ....ota kidogo !! ***
The Bitoz