Vimambo na vijimambo safari yangu Mtwara to Singida

Vimambo na vijimambo safari yangu Mtwara to Singida

nikisafiri afu tumbo langu likiwa empty ni kujamba kwa nguvu coz tumbo hujaa na ni shida kwangu..niwe mkweli bila msosi wa nguvu sisafiri kabisa.nikiwa nimekula vzr yaani kwenye basi naweza fanya hata vitu vingi vya kujitolea

.samahani mtoa mada ushauri wako namba 1. hauendani na mm
Hapa pia siwezi kusafiri na njaa afadhali nighairi safari!
 
Mkuu naona umezunguka mno. Ungepitia Tunduru - Songea - Njombe - Iringa - Dodoma ungefika haraka.
 
Hatimaye saa 10:13 tuliwasiliNangurukuru,hapa ndipo abiria hujipatia chakula na huduma za maliwato ipo mkoa wa Kilwa
😳😳😳😳😳😳😳😳😳
 
kweli hata mimi kula njiani naogopa aisee hapana chezea tumbo kuvuruga
 
Mkoa wa lindi aisewle,wasahihishaji hamna dogo
Hatimaye saa 10:13 tuliwasiliNangurukuru,hapa ndipo abiria hujipatia chakula na huduma za maliwato ipo mkoa wa Kilwa
 
Story ikiwa na vipicha picha kama hii inaleta uhalisia. Imebidi tuamini LAKINI HILI LA KUTOKA UBUNGO SAA NANE MCHANA NA KUFIKA MSAMVU SAA NNE USIKU NDIO LIMEHARIBU KILA KITU.
Mtoa mada yuko sahihi. Mara nyingi gari za kutoka Mtwara hadi Moro,huingia saa2 hadi saa4,ni range hiyo ya muda. Siku nyingine kipande cha Ubungo Mbezi kinaweza kula masaa 2. Pia nadhani kwa route hiyo ya Moro-Dar-Mtwara na Vice versa,kuna muda ambao madereva wamepewa kufika final point,hivyo kama kawahi,atachelewa chelewa ku- "buy time" ili kufika muda ulioruhusiwa. Kiuhalisia,umbali wa Mtwara hadi Moro,ni karibu kuliko Dar-Mbeya,Dar-Nzega,Dar-Kahama.
Haipishani sana na Dar-Njombe!
Mtwara-Dar(563km), Dar-Moro(198km literally 200km),jumla Kilometa 761.
Dar Njombe: Njombe-Makambako(60km), Makambako-Iringa(160km)
Iringa-Moro(305km),Moro-Dar(198km)
Jumla 723km(Njombe-Dar). Hivyo tofauti ya Umbali kati ya Mtwara-Moro(761km) na Njombe-Dar(723km) ni wastani wa Kilometa 38 pekee,ambazo kwa mwendo wa basi ni nusu saa au dk 45.
Ikiwa gari za Njombe hufika Dar saa 11 au 12 jioni,basi gari za Mtwara-Moro,zinapaswa kufika dk45 baadae yaani kufika Mtwara au Moro saa 12 au 1 jioni.
 
Nilidamka kongwa asubuhi mapema nikasikilizia tumbo nikaona lipo fresh,nikasogea stendi sasa kuangalia usafiri wa Singida.

Hata hivyo kilichonishangaza katika eneo hili ni wingi wa mbwa wanaorandaranda huku na huko,tena mbwa wenye afya hasa nao walipishana na watu bila hta wasiwasi wala hakukuwa na mtu aliyejali wala kuwabugudhi wanyama hawa.

Kwa mawazo yangu niliamini ni kutokana na jamii iliyopo kuwa ya wafugaji zaidi,kadhalika eneo hili malori na magari madogo yalisimama hapa kwa huduma za vyakula hasa Nyamachoma,mbwa hawa walineemeka sana na mabaki ya vyakula kiasi kwamba walinawiri kwelikweli.

Vilevile nilishangazwa na ufundi wa kuendesha gari la kuvutwa n ng'ombe,kiukwelj sio rahisi kwani mwongozaji aliweza kuwaamuru watembee,wakimbie,wasimame na kukata kona alimwongoza mnyama mmojawapo tu kulingana na wapi anataka kukata kona,ujuzi huu ni muhimu sana hasa kwa barabra iliyo bize kama ya moro-dodoma.

Baada ya kuulizia usafiri nikabaini kwamba ni lazima kusubiri magari toka Morogoro na nilikuwa na haraka basi nikapanda gari ndogo hadi dodoma nilipobahatika kupata basi la Nyehunge,shida ikaja pale kuingia garini na siti hamna,sikujali nilikuwa na haraka nikakaa tu pale mbele.

Safari hii dereva alikuwa ni kichaa haswa,muda wote VTS ilikuwa ikipiga kelele tu,naye alipunguza mwendo kidogo kisha ikizima anakanyaga mafuta basi ni kelele tu na ilikuwa na sauti kubwa kiasi.

Baada ya kuacha mzani hatukwwnda sana trafiki akaipiga mkono wakashuka pamoja na dereva wakaongea kidogo kisha safari ikaendelea,nadhani Rushwa ilifanya kazi yake.

Saa nane tayari tulikuwa ndani ya stendi ya Misuna,hii stendi naipa Kongole halmashauri ya manispaa ya Singida.

USHAURI WANGU.

Kutokula kabisa safarini ni hatari kwa afya,ni rahisi zaidi kupata shida kama vile kuharisha usipokula kuliko ubapokula.

Ni vizuri kumeza dawa za flgil unaposafiri hata kama huumwi,meza tu kwa tahadhari ukizingatia vyakula vingi njiani si salama,ukiweza beba chakula chako toka nyumbani.

Wahusika mtuondolee adha ya kurundika abiria kwani ni hatari kwa usalama vilevile haipendezi kwa sifa za kampuni.

Hizi VTS zinatoa alam mara spidi ifikapo 85+kph waongeze angalau 100kph,hii ni biashara na huu ni uchumi ni kuchelewesha maendeleo tu haiwezekani basi zitembee sawa na lori la mizigo inachosha.

Trafick punguzeni rushwa fanyeni kazi,madhara ya rushwa hizi ni makubwa endapo vyombo hivi vitapata ajali,fanyeni kazi kama ni njaa kila mtu ana njaa jikazeni kizalendo.
Nani kakudanganya kwamba flagyl ni dawa ya kuzuia kuharisha?
 
Hahah
Asubuhi ya terehe 29 nikaamka salama tayari kwa safari ya kwenda,Singida lakini nilihisi hali ngeni tumboni.

Tumbo lilichafuka nikakimbilia kumeza dawa za kuzuia kuendesha(sio flagil) hatimaye likatulia,nikawasili stendi kukata tiketi ya basi la POLEPOLE likitokea Dar es salaam,gari iliwasili saa saba mchana.

Ilikuwa ni gari chakavu kweli kweli lakini ilikuwa imejaza abiria wa kutosha,vyuma vilijitokea katika baadhi ya siti,nyaya na mikanda ilikuwa mibovu.

Hakika yule dereva alikuwa rafu kweli kweli,mwendo ulikuwa ni mkali aliovertake hovyo akipiga breki hovyo kiasi cha kusumbua mno abiria mara kadhaa alilazimisha magari mengine kusogea pembeni wakati akiovateki angalabu tulikaribia kuumana uso kwa uso na lori la mafuta.

Jirani yangu alikaa dada mmoja mrembo wa haja,hazikupita dakika thelathini akauliza kama nina dakika ili aweze kupiga simu,nikakubali na kumpa simu mara baada ya kumaliza alishukuru na safari ikaendelea.

Tabia ya dada huyu ilinishangaza kidogo,alikuwa anakula kila kituo tunchosimama mara chipsi,mahindi,karanga,juisi,mayai,nyama choma na hata karanga.

Kama ilivyo ada abiria walirundikwa wa kutosha katika varanda na bado waliendelea kupakia na kushusha vituo mbali mbali.

Trafiki waliendelea kupewa elfu tano tano kila walipopiga mkono,hakuna trafiki aliyeingia ndani zaidi ya kumalizana na konda kibingwa.

Hali yangu ilianza kubadilika,kwani tumbo lilizidi kuchafuka ajabu,nilijikaza huku kijasho kikinitoka nikajisemea "niliyokuwa nasikia kwa wengine yananikuta leo"..

Hali ilizidi kuwa mbaya kiasi kwamba uvumilivu ulinifika kikomo,jasho lilinitoka na nilitetemeka kwa mbali nikaona huku ndiko kudhalilika kwenyewe sasa..

Nikamwita konda kumweleza hli yangu akapuuzilia mbali akasema ngoja tufike dodoma,baada ya robo saa hivi nikamweleza kuwa sitoweza tena hivyo wafanye utaratibu wa kuniacha zahanati au stendi,pia niliwaomba wanirudishie nauli nusu..

Waligoma katakata nikaona nitadhalilika kwa sasa nikawambia wanishushe tu,nikashukia Kongwa na kuwahi zahanati...

Baada ya kupewa dawa nikaenda kuripoti polisi juu ya suala la wenye gari kutochukua hatua yoyote kwa abiria aliyeugua,walitoa ushirikiano na nikalala Kongwa kusubiri siku inayofuta.....

Inaendelea.....
Hahahaha hii iliwah kunitokea tumbo lilinivuluga baada ya kunywa juice iliyo expire niliyo nunua njian nlikua natoka arusha to mwanza aseee cto sahau ndomaana usafiri wa basi kwangu sina habari nao.
 
Mtoa mada yuko sahihi. Mara nyingi gari za kutoka Mtwara hadi Moro,huingia saa2 hadi saa4,ni range hiyo ya muda. Siku nyingine kipande cha Ubungo Mbezi kinaweza kula masaa 2. Pia nadhani kwa route hiyo ya Moro-Dar-Mtwara na Vice versa,kuna muda ambao madereva wamepewa kufika final point,hivyo kama kawahi,atachelewa chelewa ku- "buy time" ili kufika muda ulioruhusiwa. Kiuhalisia,umbali wa Mtwara hadi Moro,ni karibu kuliko Dar-Mbeya,Dar-Nzega,Dar-Kahama.
Haipishani sana na Dar-Njombe!
Mtwara-Dar(563km), Dar-Moro(198km literally 200km),jumla Kilometa 761.
Dar Njombe: Njombe-Makambako(60km), Makambako-Iringa(160km)
Iringa-Moro(305km),Moro-Dar(198km)
Jumla 723km(Njombe-Dar). Hivyo tofauti ya Umbali kati ya Mtwara-Moro(761km) na Njombe-Dar(723km) ni wastani wa Kilometa 38 pekee,ambazo kwa mwendo wa basi ni nusu saa au dk 45.
Ikiwa gari za Njombe hufika Dar saa 11 au 12 jioni,basi gari za Mtwara-Moro,zinapaswa kufika dk45 baadae yaani kufika Mtwara au Moro saa 12 au 1 jioni.
Safi sana mkuu kwa kuja na takwimu hizo,again hii inatudhihirishia kuwa nchi yetu kwenye suala hili la barabara bora tupo bado sana,wanasiasa wetu wanatulisha matango,mfano kutoka Windhoek hadi Katima Mlilo(kwenye border na Zambia na Botswana )ni kama 1400km na mwendo wa bus ni chini ya masaa 14 na kwa gari ndogo ni pungufu ya hapo,na pia kutoka Martin Drift kwenye border ya SA hadi Kazungula (border na Zambia )ni kama 1300km na mabus yanatumia chini ya 14hrs na gari ndogo ni chini ya hapo,sasa mtu kusafiri kutoka Mtwara hadi Singida for two days hii ni crazy !! umbali wa Njombe to Dar ni 723km bus inachukua nusu siku kusafiri umbali huo(huu ni almost wa umbali kati ya Cape Town na Port Elizabeth ndani ya SA)na gari ndogo unachukua saa 8tu na mapumziko kibao njiani;tunakokwenda ni mbali zaidi na unafiki wa viongozi wetu ukome,ubora wa barabara zetu ni duni mno.
 
Kabisa n kile kipnde ch mbezi kilikul 2 hours kweli plus kuokoteza abiria

Back
Top Bottom