Vile mashauzi yalivyoniumbua

1. Wakati tupo shule sekondari nimesoma day. So mida ya jion ilikua tukitoka tunakua tumerundikana wengi sana hapo nje ya geti, wa kupanda vibasi wanapanda, na wengine mdogo mdogo kwa miguu nk. Sisi wa miguu tulikua tunapenda ikipita gari tunaikimbilia tunadandia kwa nyuma then mbele kidogo tunaruka:

Kisa a) Siku hiyo imepita pick up moja ipo speed kiasi nikaona niwaonyeshee mbwembwe wenzangu. Basi nikaanza kuikimbiza ile gari, kumbe mwenye gari nae aliniona akapania kunikomesha maana wenye magari walikua hawapendi kabisa hiyo tabia. Basi ile nakaribia kuishika bodi ya gari dereva akafunga breki ghafla! Kwa kasi niliyokua nayo nilijikuta najibamiza uso nyuma ya ile gari paa! Turu hilooo... aisee niliaibika sana watu walinicheka mnoo.. ila sikukoma

Kisa b) Siku nyingine mimi na jamaa yangu tukadandia tena gari nyingine kwa mtindo ule ule. Baada ya kudandia saa ngapi dereva hajaanza kuchochea mwendo halafu anaelekea uelekeo tofauti na tunapoenda sisi! Tukashauriana turuke hivyo hivyo. Aisee tulianguka kama mafurushi ya mahindi tukaburuzika kwenye vumbi magoti na mikono imechubuka balaa.

2. Kuna wakati nilikua nafanya kazi kwenye kaduka flani ivi. Hiyo sehemu kuna fremu nyiingi za maduka zimejipanga so watu ni wengi. Akapita mdada ana bonge la trako ila sasa nguo yake ikawa imekaa vibaya kwa nyuma. Alivaa sketi ndefu, ila transparent kabisa. Kwa ndani ilikua na kitambaa kizito, ila sasa hicho kitambaa kizito ni kama kilinasia kwenye chupi huku juu (labda wakati wa kuvaa au toilet), kwahiyo chupi, tako na mapaja yote kwa nyuma yakawa yanaonekana laivu! Mimi ki jentroman nikatoka nikawa namuita "We anti..! Dada...! Sister...!" Mwenyewe akageuka, akaniangalia, akaachia boooonge la sonyo kisha akaendelea zake kutembea kwa madaha!! Sasa watu wote wakanigeukia mimi wakawa wananicheka aisee niliaibika mnoo.. nikarudi zangu nimejikunyata kama kuku alienyeshewa na mvua.

3. Siku hiyo bana jamaa kaja na pikipiki XL 125 mtaani, kidume nimeshapewa theories jinsi ya kuendesha nikajidai naweza. Jamaa kaniuliza mara mbilimbili nikamwambia niko vizuri hivi ni vitu vidogo kwangu. Nikakamata chuma pale, piga kiki jino moja kitu kikaitika, shika klachi, vuta mafuta ya kutosha, pachika gia then nikaachia klachi kama nilivyosikia kwenye stori kijiweni. Maamaeee..! Kitu ilipaa tairi ya mbele nikayumba mara mbili ya tatu niliona vumbi tuu...
 
😂😂😂😂dahh
 
Ilikuwa miaka ya 90s kama unatokea ndanda unaelekea mikoa ya Lindi na Mtwara kama km 10 Kuna kijiji kinaitwa nangoo.Daraja lilizolewa na maji wananchi wakakaa pembeni ya barabara wakisimamisha magari ili kuwapa tahadhali.Kuna gari land cruiser ya wazungu walisimamishwa sana ili wapewe tahadhali lakini walidharau huku wakiwapungia mikono wananchi...hamadi wakiwa speed waliruka katika gema la daraja na kupata ajali mbaya iliyoondoka na uhai wa wazungu wote wanne.
 
Mimi sijawahi kwa sababu siringiagi watu so nashtuliwa mapema
Ila kuna siku nilishuka kwenye kausafir fulani na huyo niliyemfuata ndio aliniabisha mbaya.

Sijui alikuwa anat'xxxxxxxmba basi alitoka tu njee ile nahamu ya yeye kuja woi.

Siamekuja kaifungia duidu yenye mavu,,,,,,,zi kibao juu ya mkanda alivyokuwa anakuja watu walicheka hadi nikamwona nami nikaanza kucheka nika snap photo akaja nikamwonyesha akairudisha mahali usika akacheka akaona aibu sana . Ila ilikuwa raha sana .
 
🤣🤣
 
Atakaeelewa alichoandika huyu dada naomba anifafanulie. Sijui ni balimi ndio zinanichanganya?
 
that's too bad aiseeh'..!!
 
Hahahhaaa....
Sasa ndugu yangu ulitaka ujifunze pikipiki kwa theory seriously.???
 
Last year kuna mdada wa makamo kama late 30s ivi au 40s kwa makadirio nilikaa nae seat moja kwa daladala alivaa top na mini skirt wakati anajirekebisha nguo yake shanga zilikatika zile particles zikamwagika zilikuwa shanga nyingi sana…aliona aibu sana thou alinisalimia wakati wa kupanda…alijiskia vibaya sana…japokuwa baada ya hapo ilikuwa ni story nyingine inayohusiana na kula kimasihara[emoji23][emoji23]
 
Wa Africa tofauti na wanawake wa kizungu wao madem wa kizungu ukiwaita Wana kuja kukusikiliza hawa ogopi na hawana wasiwasi Kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo kubwa wanawake wa kibongo kila dakika alipo hasa mabinti, anawaza, K yangu hivi K yangu vile,, yaani mawazo hayaendi mbali,,
Wanawake wa kizungu hilo hawana
 
Hujui kuandika ?
 
Enzi hizo niko sekondari kuna ile tabia ya wadau kupenda sifa, kutaka umati utambue uwepo wa mtu fulani.. mwamba akapita nje ya darasa akaona wadau tumetulia class akaanza mbwembwe zake toka akiwa nje, kuingia ndani akaona dawati moja liko mbele hakuna mtu aliyekaa mdau akajikusanya kukaa kwa sifa zote.. akajikuta yuko chini dawati liko vipande vipande jamaa ni mfupi, mnene.. zile mbio alizotoka nazo pale hakuwahi tena kupita darasa letu maana sio kwa aibu ile..
 
Nilipokuwa A-level siku moja asubuhi nilipoamka nilienda kuanua nguo nilizofua ,halafu nikaenda darasani ,wakati nafanya representation nikaingiza mkono mfukoni nichukue leso nijifute uso si nikatoka na boxer iliyoko mfukoni kumbe kwenye zile haraka za kuanua nguo asubuhi niliweka mfukoni,ni aibu balaa darani wakawa wanacheka balaa
 
Wakati nipo mdogo nasoma shule ya msingi, msimu Kama huu wa sikukuu mama alimpa pesa baba mdogo anisindikize sokoni kununua nguo,tunapita mtaa Fulani nyuma yangu mpiga debe ananiita "wee dogo,wee dogo" Mimi nashupaza shingo najua wahuni tu sigeuki,jamaa mpiga debe akaja Hadi kunigusa bega "we boya we boya mnapotezana mwenzio kakata Kona" haha kugeuka bamdogo yuleee Kona nyingine,watu wengi tungepotezana kweli...tangu hapo nikiitwa nageuka...
 
Hii kusalimia wamama hata mimi sipendi, unaweza jikuta umekisalimia kitoto kidogo chenye umbo kubwa.
Kitaa nilichohamia nikitoka kwangu nyumba ya tatu kuingia Barbara kubwa asubuhi wa mama wapo nje wanafanya bizness zao,week ya Kwanza yote nilikua naaamkia,Kuna siku nimeamkia bwana napiga hatua tatu mbele nasikia wanasemezana kwa sauti ya chini "huyu Kaka si mtu mzima kabisa anaamkia amkia tu " hahaha NIMEBADILI NJIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…