Vikwazo na Mafanikio

USSD

Member
Sep 19, 2021
21
55
KIKWAZO KIKUU CHA KUTOFANIKIWA NI HIKI.
Kwenye jamii yoyote ile, asilimia 10 ndiyo wenye mafanikio huku asilimia 90 wakiwa hawajafanikiwa.
Na zaidi, asilimia 1 wana mafanikio makubwa kuliko asilimia 99 iliyobaki.

JE, NINI KINATENGENEZA HALI HIYO?
Kuna njama zinazofanywa ili kuwazuia wengi wasifanikiwe na wachache tu ndiyo wafanikiwe?

Ukiiangalia na kuisikiliza jamii, unaweza kuona kama kuna njama zinazoendelea.
Lakini unapokwenda kuyaangalia maisha ya waliofanikiwa na wanaoshindwa, mambo yanakuwa hadharani.

Kuna mengi sana yanayowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Lakini kuna moja kuu ambalo ndiyo lenye nguvu zaidi.
Yaani kwa hilo moja, litaamua kama utafanikia au utashindwa.

Kabla hatujaona hilo kuu linaloamua mafanikio, hebu jipe mfano halisi, labda wako mwenyewe au wa watu unaowafahamu.

Huenda ukishasikia kilimo cha matunda fulani kinalipa ,ukaenda kulima na kupata hasara,

ukaona umepotea.

Ukasikia ufugaji wa aina fulani ,ukaingia kufuga, ukakutana na changamoto, mifugo kufa na soko kutokuwa vizuri, ukaacha.

Ukasikia biashara ya pesa inalipa sana, ukaingia kufanya, ukaliwa hela zako zote. Ukaona umetapeliwa.

Ukaendelea hivyo na kila fursa mpya unayoisikia inakuvutia na unaona hiyo ndiyo mwisho wa shida zako zote.

Lakini unapoingia, mambo yanakuwa tofauti na ulivyotegemea na unaishia kuanguka vibaya.

kama utakuwa na kitu kimoja muhimu; UNG’ANG’ANIZI.

Ung’ang’anizi ndiyo muhimili mkubwa kwako kupata mafanikio yoyote unayotaka.

Kama huna ung’ang’anizi, ninaweza kukuhakikishia bila ya shaka yoyote kwamba hutaweza kufanikiwa.

Kila fursa unayoisikia, hutaingia tu na kuanza kuchuma faida mara moja.
Lazima upite kwenye moto mkali kwanza, lazima ukutane na magumu sana kabla hujapata neema.

Asili huwa ina utajiri wa kutosha, lakini huwa inagawa utajiri wake kwa kumpima kwanza mtu kama amejitoa kweli kuupata utajiri huo. Na kama akiupata ataweza kuutunza vizuri.

Ndiyo maana biashara yoyote utakayoingia utakaribishwa na hasara.
Na kilimo au ufugaji wowote utakaoingia kwa mara ya kwanza kuna uwezekano wa kupoteza sana.

Hilo ni darasa na mtihani, ambao lengo lake ni kuchuja wale wenye mioyo myepesi, wale wanaotamani tu mafanikio na hawajajitoa kweli kuyapata.

Ukiweza kuvuka madarasa na mitihani hiyo, ambayo kwa kweli ni mingi, basi dunia itakuzawadia mafanikio ya kila aina.
Watu watasema una bahati au njama fulani zinazokuwezesha kufanikiwa kuliko wao, lakini kwa uhalisia huna tofauti kubwa na wao, ulichonacho ni ung’ang’anizi.

kila aliyefanikiwa kuna bahati fulani aliyokutana nayo kwenye safari yake ya mafanikio.

Hakuna hata mmoja anayeweza kusema mafanikio yake yametokana na yeye mwenyewe kwa asilimia 100.

Lakini bahati zinaenda kwa wale wanaodumu kwenye kitu kwa muda mrefu, kwa maneno mengine wale wenye ung’ang’anizi.

Je wewe upo tayari kung’ang’ana kwenye kile unachokitaka kwa muda gani bila kukata tamaa?
Muda wa chini kabisa ni angalau miaka 10.
Hii ya kila mwaka kuanza na kitu kipya haiwezi kuwa na manufaa kwako, zaidi tu ya kujifurahisha.

Mafanikio ya kweli ni matokeo ya kung’ang’ana kwenye kitu kwa muda mrefu.
Kujitoa kweli na kuiambia dunia nitapata ninachotaka au nitakufa nikiwa nakipambania.

Hakuna chochote duniani kinachoweza kuchukua nafasi ya ung’ang’anizi.

Kipaji hakiwezi, dunia imejaa wengi wenye vipaji ila hawajafanikiwa.

Akili haiwezi, wapo wengi wenye akili sana ila hawana mafanikio.

Elimu haiwezi, dunia imejaa wasomi wengi wasio na mafanikio.

Ni ung’ang’anizi na maamuzi pekee vilivyo muhimu kwenye mafanikio.

Kauli mbiu ya Endelea na mapambano imetatua na itaendelea kutatua matatizo mengi ya wanadamu.

EPUKANA NA TABIA MBOVU ZINAZOKWAZA MAFANIKIO YAKO
Tabia ndio zenye nguvu kubwa ya kujenga au kubomoa mafanikio yako.

Mafanikio au kushindwa siyo tukio. Hakuna mtu anaamka siku moja na kujikuta amefanikiwa au ameshindwa.

Mafanikio au kushindwa ni mchakato, ambao unatengeneza kwa muda mrefu. Kitu chochote ambacho kinatengenezwa kwa mchakato kinaathiriwa sana na tabia ambazo mtu anakuwa nazo.

Unajionea hapo jinsi tabia zako zilivyo na athari kwenye mafanikio yako.
Ulivyo leo ni matokeo ya tabia ulizokuwa nazo huko nyuma.
Na kama utaendelea na tabia hizo, utaendelea kupata matokeo kama unayopata sasa.

Kadhalika matokeo unayoona kwenye maisha yako, mbegu yake ni tabia ulizonazo.

Kama hujapata kile unachotaka au kufika unakotaka, kuna tabia ulizonazo sasa ambazo ni kikwazo kwako.

Bila ya kuvunja tabia hizo, itakuwa vigumu sana kwako kufanikiwa.

Nimeziona tabia zifuatazo kuwa kikwazo kwa mafanikio.

Uvivu, uzembe, ulevi, uzinzi, , wizi, dharau, kiburi, ujuaji, hasira, kutokujifunza, kukosa uaminifu, tamaa na kutokujali wengine.

Kama una tabia yoyote kati ya hizo, unapaswa kuivunja mara moja ili isiwe kikwazo kwa mafanikio yako.
Hata ikitokea umefanikiwa ukiwa na tabia hizo mbaya, anguko lako linakuwa kubwa na kinaloumiza zaidi.

Ili kuepukana na haya , zingatia misingi ifuatayo

I. BADILI MTAZAMO WAKO.

Mtazamo ulio nao ndiyo mzizi wa tabia ulizonazo.

Huwezi kubadili tabia bila kubadili mtazamo.

Mtazamo ni ile imani unayokuwa nayo kwako mwenyewe, ni vile unavyojiona ndani yako.

Kwa tabia mbovu ulizonazo, una mtazamo fulani unaozizalisha.
Wengi wana mtazamo wa kurithi, kwamba tabia hizo wamerithi kutoka kwa wazazi wako.

Unakuta mtu ni mlevi na anakuambia kwetu tuna asili ya ulevi.

Au ana hasira asizoweza kudhibiti na kusema sisi huwa tuna hasira sana.

Mitazamo ya aina hii inazihalalisha tabia mbaya na kuzifanya zionekane ni sugu.

Vunja kabisa kila mtazamo ulionao unaohalalisha tabia zako mbaya.

Tambua wewe ndiyo mwenye nguvu na mamlaka ya kujenga mtazamo na maisha yako kwa ujumla.

Usijichukulie kama mtu mwenye hatia na dhaifu, bali jichukulie kama mtu mwenye mamlaka ya kuyabadili maisha yako.

Jua unaweza kuwa vile unavyotaka na haijalishi umetokea kwenye mazingira gani, una nguvu ya kuyabadili maisha yako.

Jenga mtazamo sahihi na utaweza kujenga tabia sahihi.

II. HAKIKISHA UNAJENGA TABIA NYINGINE NZURI YA KUCHUKUA NAFASI YA TABIA HIYO

Kama unataka kuvunja tabia mbaya, hakikisha unajenga tabia nyingine nzuri ya kuchukua nafasi ya tabia hiyo.

Ukiondoa tabia na kuacha uwazi, utajikuta unarudi kwenye tabia hiyo au tabia nyingine mbaya.

Kama unataka kuacha ulevi, unapaswa kuutumia ule muda uliokuwa unalewa kufanya mambo mengine yanayokuweka bize.
Inaweza kuwa kujifunza au kushirikiana na wengine wanaofanya mambo mazuri.

Asili haipendi utupu, ukivunja tabia na kubaki na muda ambao ni tupu, unatoa nafasi kwa tabia hiyo au nyingine kuchukua nafasi hiyo.

III. BADILI MAZINGIRA YAKO.

Huwezi kuvunja tabia kwa kuwa kwenye mazingira yale yale yanayochochea tabia hiyo.
Badili mazingira yako ili uwe mbali kabisa na tabia unauotaka kuivunja.

Epuka makundi ya watu walio na tabia unayotaka kuvunja, maana wale unaokuwa nao wana ushawishi mkubwa kwako.

Kama unataka kuacha ulevi, achana na marafiki zako ambao ni walevi.

Na usiende kufanyia vikao eneo la baa au kuwa na pombe ndani kwako.

Usijidanganye kwamba wewe ni imara na unaweza kukataa.

mazingira na wanaokuzunguka wana ushawishi mkubwa sana kwako.

Jipunguzie vishawishi kwa kubadili mazingira yanayochochea tabia unayotaka kuvunja.

IV. VUNJA KILA AINA YA DARAJA. DARAJA KATI YAKO NA TABIA MBAYA

Kuna daraja kati yako na tabia mbaya ambayo ni kikwazo kwako, vunja madaraja yote.

Kama umekuwa na tabia ya uzinzi, una michepuko, vunja madaraja yote na michepuko hiyo.

Kosana nao kiasi kwamba hata siku ukirudi kuwaomba msamaha hawawezi kukuelewa kabisa.

Kuvunja tabia ni vita, unachotaka ni ushindi, hivyo kila silaha inayoweza kukusaidia, itumie.

V. JENGA UWAJIBIKAJI AMBAO UNAJUA USIPOFANYA KUNA KITU UTAPOTEZA

Peke yako ni rahisi kurudi nyuma.

Unapokuwa na mtu wa kukuwajibisha unajisukuma zaidi kwa sababu unajua kurudi nyuma kutakugharimu.

Tafuta mtu unayemheshimu na mwahidi nia yako ya kuvunja tabia mbaya uliyonayo.

mweleze hatua unazokwenda kuchukua.
Kisha mpe adhabu ambayo atakupatia unapokwenda kinyume na ulivyoahidi.

Inaweza kuwa ni umlipe kiasi kikubwa cha fedha ambacho kitakuuma sana.
Au inaweza kuwa ni yeye kukudhalilisha kwa namna fulani.

Jenga uwajibikaji ambao unajua usipofanya kuna kitu utapoteza na hilo litakusukuna kufanya.

VI. WEKA KUSUDI LA MAISHA YAKO

Kuhangaika na tabia mbovu ni kiashiria kwamba bado hujalijua kusudi la maisha yako.
Maana unapolijua kusudi, unagundua jinsi muda ulivyo mfupi.
Muda wako wote unaupeleka kwenye kuliishi kusudi lako na unakuwa huna muda wa kupoteza.

Jitafakari kwa kina mpaka ulijue kusudi lako, kisha tumia kila dakika ya maisha yako yaliyosalia hapa duniani kuliishi kusudi lako.

Kadiri kusudi lako linavyokuwa kubwa, ndivyo unavyosukumwa kuachana na tabia mbaya zinazokuwa kikwazo kwa kusudi ulilonalo.

VII. KUWA NA LENGO LAKO KUBWA.

Ndoto kubwa kabisa, ndoto zinazokutisha wewe na wengine ni kinga dhidi ya tabia mbovu.

Mfano kama ndoto yako ni kuwa bilionea, hutapata muda wa kulewa kila siku.

Ndoto hiyo itanyonya muda wako wote, mpaka utakosa muda wa kupumzika au kuwa na wale wa karibu.

Kama tabia mbaya zinakusumbua, chukua lengo lolote ulilonalo sasa, lizidishe mara kumi na waahidi watu kwamba lazima utafikia lengo hilo.

Waambie watu wazi kabisa kwamba utafikia lengo lako kubwa.
Unajua nini kitatokea, watakukatalia, watakupinga, watakudhihaki na kila mara watakapokuona ukifanya tabia zisizo sahihi, watakukebehi.

Hayo tu yanayosha kukuondoa kwenye tabia mbaya na ambazo ni kikwazo na kukuweka kwenye tabia nzuri za kukufikisha kwenye ndoto zako kubwa.

VIII. AMBATANA NA WATU SAHIHI.

Unapaswa kuambatana na watu sahihi, watu wenye tabia njema na watu ambao utajisikia aibu sana pale watakapojua tabia zako mbaya.

Wale wanaokuzunguka wana ushawishi sana kwenye tabia unazokuwa nazo, hivyo wachague kwa usahihi.

Pia kuwa na menta na/au kocha anayekusaidia kuondoka kwenye tabia mbaya na kujenga tabia nzuri kwa mafanikio yako.

IX. KUWA NA HURUMA NA MAISHA YAKO, USITAKE KUFANYA YAWE MAGUMU KULIKO YALIVYO.

Maisha yakiwa rahisi, huwa tunatafuta njia ya kuyafanya kuwa magumu zaidi.

Na hilo liko wazi, tabia nyingi mbaya na zinazotukwamisha, huwa tunazijenga pale maisha yanapokuwa rahisi.

Mtu anapokuwa hana fedha, anakuwa haba mambo mengi, lakini akizipata fedha ndiyo kila kitu kibaya kinamhusu, ulevi, uzinzi, dharau, kiburi n.k.

Yaonee huruma maisha yako, usitake kuyafanya yawe magumu kuliko yalivyo.

X. WENGI HATUPENDI KUKIRI KWAMBA TABIA TULIZONAZO NDIYO KIKWAZO KWETU.

Huwa ipo kauli kwamba mtu mmoja alikuambia una tatizo, huenda yeye ndiye mwenye tatizo.
Watu watatu wakikuambia una tatizo, huenda kuna njama wanafanya dhidi yako.
Lakini watu 10 wakikuambia una tatizo, basi ni kweli una tatizo.

Tabia mbovu zimekuwa kikwazo kwa wengi kwa sababu ya ubishi.

Wengi hawapendi kukiri kwamba tabia walizonazo ndiyo kikwazo kwao.

Na hupenda kutumia kauli za kuwafariji, wakitaja watu wengine waliofanikiwa wenye tabia kama zao.
 
Nice...nimekuelewa Sana na nimejifunza kitu kikubwa be blessed
 
Andiko zuri sana ndugu
barikiwa.
 
Back
Top Bottom