Vikao vya Bunge na anguko la CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vikao vya Bunge na anguko la CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Matteo, Jun 17, 2011.

 1. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kikao kengine cha Bunge la kumi, hiki kikiwa ni kikao cha kupitisha Bajeti ya Taifa letu. Mijadala kwenye Bunge inaonekana kupamba moto sana, Wabunge wa CCM wakionekana kuunga Mkono kwa asilia miamoja na kuisifia Bajeti, kuwa ina lengo mahususi la kumwokoa mwananchi wa kipato cha chini. Nimekua nikifuatilia kwa ukaribu Bunge hili la Bajeti na mathalani siku nilizopata muda wa kuliangalia Bunge, ni wazi unaona jinsi CCM kama isipo badilika itakavyo angukia pua kwenye chaguzi zijazo, wabunge wengi wa CCM wamekua ni kama hawasomi alama za nyakati na ambao ama ni wavivu kufuatilia mfumo mzima wa maisha ya wananchi (kwa kufanya Utafiti, kupitia kwenye mitandao jamii au kwa kuongea na wananchi hasa vijana) au basi ni sikio la kufa lisilo sikia dawa.  Anguko lao lipo hapa; pale wanaposimama wabunge wa upinzani na kupinga Bajeti, na wakitoa mapungufu yaliyo kwenye hiyo Bajeti kwa hoja na mifano (Rejea marekebisho ya Mh. John John Mnyika kwenye Mpango wa maendeleo wa Miaka Mitano), kisha, rejea alivyokua akiikosoa Bajeti na Kutoa sababu ya kuto kuunga kwake mkono hiyo Bajeti, na kuwakosoa baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa wakisema wazo la posho ni la Serikali, ili hali halikua kwenye Ilani ya CCM, ila lilikuwepo kwenye ilani ya CHADEMA, ilo andikwa kabla ya MPango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, na kwa akili ya kawaida unaweza kuona nani kaiba wazo la mwenzake na bila ya kuonyesha shukrani. Badala ya wabunge wa CCM kupinga kile wanacho kisema wanzao wa chadema kwa facts na kutuaminisha kuwa Bajrti haina mapungufu yanayo bainishwa na wapinzani wao wanajibu kwa Vijembe, kebei na ngebe. Mimi ningependa kuwambia wabunge hawa wa Chama Tawala kuwa, wapiga kura miaka hii wanabadilika toka tabaka la wazee kuja kwa vijana, na vijana hawa sikuhizi kwa makundi wanaangalia na kufuatlikia mijadala hii kwa makini na kibaya zaidi wanachambua, karibu kila mnacho kiongea, na kwa taarifa yenu, wengi wenu huwa wanawadharau hasa pale mnapo beza michango yenye maana ya wapinzani.  Kama, wabunge hawa wa CCM wamekua makini kwa miaka ya hivi karibuni watagundua kuwa vijana wengi wamechoka na ngonjera za Amani na Utulivu, wakiona ngonjera hizi kwa kiasi kikubwa zinawafaidisha viongozi hasa mafisadi zaidi ya wao vijana na wananchi wa kawaida, mfano pale Kiongozi anapoamua kuwa fisadi na kuamua kujilimbikizia mali na pale vijana wanapo taka kuandamana kupinga vitendo hivi vya kifisadi wanaambia kuwa ni wavunjifu wa amani, haiingi akili ni nani hasa anae vunja amani hapa? Anae andamana kupinga ufisadi au fisadi??? Hili la Vijana kuzichoka ngonjera za Amani na Utulivu, zinajidhiirisha kwenye mijadala mbalimbali inayo husu mstakabali wa Taifa letu, Mfano dhahiri, ukiwa mjadala ulokuwa ukihusu katiba uliofanyika UDSM, pale mtu alipo kuwa akisimama na kujaribu kuwahadaa vijana na ngonjera tajwa hapo juu, Vijana walikuwa wakimzomea na kumtaka asiendelee kuongea.  Kwakuwa nchi hii ni yetu wote na sio ya wabunge wa CCM, wito wangu kwao ni kuwa wawe makini kubaini mapungufu ya kwenye bajeti ili iwe yenye tija kwetu, wasijifanye ni vipofu wa ukweli ama waliolishwa unga wa ndere, pale wanapo kiona cheusi kama cheupe na cheupe cheusi. Wajue kuwa ukweli wa hoja haupingwi kwa vijembe bali hoja nzito zenye kuudhirisha ukweli usio kuwa na mawaa, na kama kweli mnataka tena kurudi Bungeni, semeni na tendeni yale ya kuwapendezesha wananchi. Miaka yote tumekua tukiwashuhudia mkiipamba Bajeti kuwa imelenga kumsaidia mwananchi masikini, ila hali ya huyo mwananchi inazidi kuwa mbaya, kila kukicha,(Rejea, takwimu za kiwango cha Umaskini Tanzania) sasa mi sijui huwa mnatukejeli au??? Si ninyinyi mlio sifu ujenzi wa Shule za kata, mkasema Serikali imekusudia kufuta Ujinga na kuongeza udahili wa wanaojiunga na Elimu ya Sekondari, kilicho tokea mnakijua, wakati mnasifu shule za kata sina uhakika kama kuna Mbunge alikua na mtoto wake kule, sasa kama hizi si dhihaka kwa wananchi ni nini?? Mnapitisha msicho kiamini kwa ajili ya maslai yenu. Sina uhakika kama hadi tusubiri mpaka kiama ila muhukumiwe ninyi wabunge wa CCM, tutawahukumu hapahapa duniani na siku si nyingi na Mkifa mtahukumiwa mara ya pili na Mwenyezi MUNGU kwa dhihaka mnayotufanyia, Sauti za akina Mama wanaohangaika, Wazee wasiokuwa na msaada, vijana mliowalaghai wakapata daraja la sifuri zinawalilia, zisikieni kwa makini, ni sauti za kuhuzunisha, zilizo kata tamaa, hawajui kesho yao ni nini ili hali ninyi na familia zenu mnaweza kupanga maisha ya miaka kumi ijayo, mnawapeleka watoto wenu Ulaya, ili waziepuke sufuri, endeleeni na kebehi nanyi muda si mrefu wananchi watawakebehi, waswahili husema hakuna marefu yasio kuwa na ncha. Natoa wito kwa vyama vya wapinzani hasa CHADEMA, wafunge milango ya kuwapokea wanasiasa wanaotoka Chama Cha Mapinduzi, hasa kwenye zama za anguko lao ambalo halipo mbali.  Mungu Ibariki TANZANIA, Mungu Ibariki AFRIKA.
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nashukuru mkuu kwa good analysis, sina comment zaidi ya kuongeza kidogo tu kuwa wakiona kitu kilchoanzishwa na wapinzani kimepata mashiko kwa wapiga kura wao huwa ni wabingwa wa kubuni propaganda za kuwahadaa ili waonekane wazuri, mfano mzuri ni operation vua gamba.
   
 3. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Makala safi sana hii.. Keep it up.
   
 4. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Shukra mkuu, umenena vyema ni jukumu letu kuongoza mapinduzi ya kweli katika kumkomboa Mtanzania, kila mmoja kwa nafasi yake aungane na wapambanaji Chadema kwani ndio wameonyesha nia ya kweli kumkomboa mtanzania maskini.
   
 5. c

  chiwanda Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunakushukuru mkuu kwa kutuongezea ujuzi wa namna ya kukabiliana na chama ambacho uhai wake umebaki miaka 4na miezi kidogo tu.
   
 6. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Hapo Umenena Haswa Mkuu,. ni dhahiri tutaona wengi wakiomba kuingia kwenye Safina pale mwisho wao utakapofika
   
 7. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,453
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Anguko liko dhahiri siku za mbeleni. Ndani ya chama hajajitokeza watu jasiri wa kumfunga paka kengele,sio kwamba wabunge wa CCM hawayaoni,wanayaona sana.Lakini wamekula kiapo cha kutokwenda kinyume na serikali yao ndani ya bunge kwa gharama zozote na kwa hali yoyote.Hatari yenyewe bunge litageuka kichaka cha kubomoa haki na demokrasia.Sioni wapinzani bungeni kuishinda serikali hilo halipo kabisa kwani idadi yao ni ndogo mno.Kura zao ni kiduchu.Lakini malipo halali ni 2015.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  wabunge wa CCM ni janga la TAIFA. wanakula kodi bure bila mchango wowote wa maana
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ninakila sababu ya kuamini wazo kuwa ccm inaenda kufa na bila shaka tutaizika bahari ya Hindi ikaliwe na pweza na nyangumi.....
   
 10. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kutazama wanatazama lakini hawaoni. WANASIKIA KWA MASIKIO YAO LAKINI HAWAELEWI. Hadi anguko lao litakapiowajia kwa ghafla na kuangamia. Poleni sana ccm
   
 11. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Soon Safina ifungwe pliz
   
 12. oba

  oba JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Napata kigugumizi kuelezea vile ninavyomtafsiri mtu anayeona nyumba yake inajengwa hovyo kisha anasema endeleeni tu, ni ****? hivi baba mzuri wa familia aweza kumwona house girl akiharibu watoto wake lkn akamwambia endelea na kazi, well done?
  Sasa inakuwaje mheshimiwa mbunge unachambua hoja vizuri na kueleza mapungufu unayoyaona katika eneo fulani, na scientifically ukajiridhisha kuwa kuna jambo la kurekebisha lkn ukahitimisha na naunga mkono hoja, una akili kweli? je una sifa ya kurudishwa bungeni kuwakilisha wananchi wako?mmh naona shaka sana
   
 13. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ONYO
  >Kuanzia kikao kijacho ni marufuku kwa mbunge yeyote kuunga mkono hoja wakati muda wote anatumia kuipinga
  >Endapo atatokea mbunge kusimama na kuunga mkono hoja na kuipinga katika mjadala wake tutamzomea huku huku
  kwenye runinga tunapowaangalia mnapowashambulia wapambanaji wa CHADEMA utadhani wao ndio Chama Tawala.
  >Ole wake atakaye jeuka.
   
 14. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  acha bangi!
   
 15. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Safi mkubwa,hilo ulilolielezea hapo lipo karibu sana, anguko lawalidhani litakuja miaka 100 ijayo, no!ni hapo 2015 tu, tunaanza nao kwenye serikali za mitaa kwa nguvu zote mwaka 2014 the tunaruka nao 2015.IMEKULA KWAO.
   
 16. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo la wabunge wetu wanaongozwa na itikadi za vyama vyao hivyo wanaogopa kuwajibishwa na chama endapo watapinga hoja. Lakini pia wanaona wakipinga hoja wataonekana wanaungana na wabunge wa chadema na wa upinzani kwa ujumla.
   
 17. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  iasikitisha sana. i was watching today, inatia kichefuchefu. yani bora wakae kimya!
   
 18. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,170
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  mkuu ccm nzima ni janga la TAIFA. Wanakula kwa mikono miwili tena bila kunawa! A gluton behaviour..¥ßíòøê¤!....
   
 19. MANI

  MANI Platinum Member

  #19
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Yana mwisho haya maana watanzania tunawaona ukifika wakati wa kuchagua tutajua nini la kufanya.
   
 20. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Tatizo si wanachakachua kura zetu jamani tufanyeje? Maana siyo kwamba wananchi hawajaamka na hawajagundua kuwa CCM ni Janga la TAIFA, lakini hapo kwenye kura na hiyo NEC yao ya bwana kivuito wa TZ
   
Loading...