Vikao vizito vya CCM kuanza leo

Vikao vizito vya CCM kuanza leo

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,365
Reaction score
27,765
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimejigamba kitatoka katika vikao vyake muhimu vya Kamati Kuu (CCM) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vinavyoanza mjini hapa leo kikiwa imara kuliko hapo awali.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye wakati akijibu swali kuhusiana na vikao vizito vya chama hicho vinavyoanza leo.

Nnauye alikuwa anaelezea maandalizi ya vikao vya kamati kuu kinachotarajia kuanza leo na halmashauri kuu ambayo itaanza kikao chake cha siku mbili kesho.

Katibu huyo amesema wajumbe wa vikao hivyo ambavyo vitatoa mwelekeo wa sura ya uchaguzi itakavyokuwa ndani na nje ya chama hicho wameshaanza kuwasili mjini hapa.

Ajenda muhimu katika mikutano hiyo ni ratiba ya uchaguzi pamoja na kuwapata wagombea wa chama hicho ngazi zote. Ajenda nyingine ni hali ya kisiasa nchini na kutolewa kwa ratiba ya uchaguzi.

Pia vikao hivyo vinatarajia kutoa ratiba ya mchakato wa uchaguzi wa Urais na wagombea wengine, kutengeneza kanuni za kuwapata wagombea.

Mambo mengine ni kupanga tarehe ya kuchukua fomu, kuzunguka kutafuta wadhamini na masuala mengine ambayo yanakigusa chama.

Mambo yanayotarajiwa kujadiliwa katika vikao hivyo ni pamoja na hatma ya makada wanaotaka kuwania kiti cha Urais ambao walitangaza nia kabla ya wakati na wakatolewa karipio na chama hicho cha kuwataka watulie na kusubiri muda mwafaka.

Tayari kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake, Philip Mangula ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM -Taifa, imeshafanya vikao vyake mjini Dodoma kupitia taarifa za utekelezaji wa adhabu kwa makada sita wa chama hicho wanaodaiwa kuanza kampeni kuwania urais mwaka 2015 kabla ya wakati.

Makada hao waliozuiwa kujihusisha na kampeni kwa miezi 12, huku mienendo yao ya kisiasa ikifuatiliwa ni January Makamba, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Mji wa Dodoma unaonekana kuwa shwari licha ya kuwa na pilikapilika nyingi na shauku ya wananchi ikiwa kubwa ili kufahamu yatakayojitokeza katika vikao hivyo.

Nje ya makao makuu ya CCM, wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo za Chama wanaonekana kuongezeka huku maatarajio yao makuu yakiwa ni kufanya biashara.

Chanzo: Habari Leo
 
CCM kinaenda kujimaliza! Wapige picha nyingi kwa kuwa yatakoyoyokea yote katika hicho kikao yatakuwa historia ya kukumbukwa kwa kuandikwa kwenye vitabu na kyzikwa kwenye makaburi ya sahau
 
sasa ni muda mwafaka kwa mpendwa wetu edward ngoyai lowassa kupitishwa rasmi kuwa mgombea wetu na kisha tumchague kuwa RAIS wa awamu ya tano kwa kishindo
 
CCM kinaenda kujimaliza! Wapige picha nyingi kwa kuwa yatakoyoyokea yote katika hicho kikao yatakuwa historia ya kukumbukwa kwa kuandikwa kwenye vitabu na kyzikwa kwenye makaburi ya sahau
Mkuu unadani ni kazi rahisi kupanda mmea kwenye rami ukamea? Ni vema mkawaza vizuri vinginevyo presha ya moyo mnayo.

ccm ni chama kikubwa hakijaanza kufanya viko leo siku zote kimekuwa kikitoka salama kabisa na maamuzi thabiti yenye tija kwa taifa.
 
sasa ni muda mwafaka kwa mpendwa wetu edward ngoyai lowassa kupitishwa rasmi kuwa mgombea wetu na kisha tumchague kuwa RAIS wa awamu ya tano kwa kishindo

Hamumtaki tena slaa?
 
Wakati muhimu,tuliokuwa tunausubiria kwa hamu sasa umewadia.
 
Mkuu unadani ni kazi rahisi kupanda mmea kwenye rami ukamea? Ni vema mkawaza vizuri vinginevyo presha ya moyo mnayo.

ccm ni chama kikubwa hakijaanza kufanya viko leo siku zote kimekuwa kikitoka salama kabisa na maamuzi thabiti yenye tija kwa taifa.
igp hiyo ilikuwa zamani CCM ya leo ni ya hovyo kuliko kipindi kingine chochote kile katika uhai na historia yake
 
Last edited by a moderator:
CCM kinaenda kujimaliza! Wapige picha nyingi kwa kuwa yatakoyoyokea yote katika hicho kikao yatakuwa historia ya kukumbukwa kwa kuandikwa kwenye vitabu na kyzikwa kwenye makaburi ya sahau
Mtalia na kusaga meno leo kesho na hata keshokutwa. Ccm itazidi kuwachapa mboko za mgongo
 
Maamuzi makini ya chama hiki kikongwe nchini kwenye vikao hivi ndio itakuwa mafanikio kwa CCM
Mi kama mwanademokrasia kila chama cha siasa nchini kijipange vizuri , wananchi wenyewe wataamua wamchague nani.
 
Ccm hata ikisimamisha jiwe lazima ishinde kwa kishindo kikuu

Washabiki mbumbumbu huwa ni mizigo kweli! Wenye chama huko Dodoma sasa hivi hawalali wanapanga mikakati mambo magumu huku mtaani "mbumbumbu" yuko usingizini anaota
 
sasa ni muda mwafaka kwa mpendwa wetu edward ngoyai lowassa kupitishwa rasmi kuwa mgombea wetu na kisha tumchague kuwa RAIS wa awamu ya tano kwa kishindo

Mgombea anayetumia fedha kununuwa uongozi ni wa kuogopa kama ukoma. Mwl.Julius K.Nyerere
 
Ccm itaongoza nchi hii hadi yenyewe itakaposema sasa basi
Not so easy!! Watanzania wa 2015 sio wale wa kupewa fulana na kanga.mjipange vinginevyo baada ya kikao hichi CCM inatoka vipande vipande Anguko la Chama dume ni sasa
 
Mgombea anayetumia fedha kununuwa uongozi ni wa kuogopa kama ukoma. Mwl.Julius K.Nyerere

Hakuna mgombea asiyetumia pesa kupata urais, hatusikilizi kelele za kitoto za kuwa fulani anacheza mpira vizuri sababu amevaa six meno, edward ni kipenzi cha watanzania sababu ni mkweli, sio mnafiki na anafanya maamuzi, hao wapinzani wake wanajua hayo ndio sababu wanashinda kumchafua usiku na mchana.
 
Back
Top Bottom