chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,384
- 24,939
Habari wanaBodi.
Kama ilivyo jadi kwa ndg zetu Waislam kila inapofikia majira kama haya ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani huwa kuna utamaduni wa kufuturishana, yaani mtu anajitolea kuandaa chakula kwa ajili yake na watu wengine bila kujali kwamba wanafahamiana n.k
Kwa mwaka huu naona tofauti kidogo, ule utamaduni wa kuandaa maakuli na kuyatandaza vibarazani watu wajisevie haupo.
Hii ilikuwa pona kubwa kwa watu wa kipato cha chini mathalan waliokuwa wamefunga, pia kwa watu wanaofanyia shughuli zao mbali na nyumbani hivyo kushindwa kuwahi kujumuika na familia.
Au ni hali ya kiuchumi imeathiri mpaka huu utamaduni wa Kiibada?
Je kufuturisha siyo sehemu ya Ibada kwa wale wenzetu waliojaliwa kipato kwa ajili ya wale maskini wasio nacho?
Nawatakia mfungo mwema ndg zangu waislam.
Asalam aleykhum.