Kupiga au kuongea na simu katikati ya mazungumzo; Unakuta mtu shida yake yeye anakuja kwako kuhitaji msaada au anakuuliza swali unapoanza kuongea naye ghafla anaanza kuongea na wewe huku anajibu meseji hivyoKwa lengo la kuwekana sawa, unaweza ukawa unatabia mbaya, ila hujui kama ni mbaya mbele za watu.
Mimi katika kuishi na watu mbalimbali, nimeshuhudia watu wenye tabia tofauti tofauti ila tunavumiliana tu, wakati mwingine tunarekebishana..!
Hizi hapa ni zile chache miongoni mwa nyingi ninazozikumbuka toka kwa watu niliwahi kuishi nao..
- Kutumia simu wakati wa kula. Hii nimeiweka ya kwanza kabisa kwa sababu ilikuwa tabia yangu, mama yangu kila alipokuwa akinikemea niliona kama anazingua tu! ila siku nilipokemewa ugenini ndio nikaamini kweli hii ni tabia mbaya, na nikaacha mara moja.
- Kutawala mazungumzo. Huyu alikuwa rafiki yangu, classmate, alikuwa anapenda aongee yeye muda wote, hata kama mada haijui vizuri hakupenda kuwa msikilizaji kabisa.
- Kutotambua muda wa utani. Hii niliiona kwa watu wengi sana, ila tamzungumzia jamaa yangu mmoja hivi, Rashid (R.I.P), huyu mshikaji alikuwa hawezi kuwa serious, alikuwa hajali mood ya mtu, hajali watu waliokuzunguka muda huo, yeye atakachoona kinafaa kukutania anakisema tu popote wakati wowote.
- Kutumia viwakilishi badala ya jina la mtu. Hii nayo niliiona kwa wengi, unakuta mtu analijua jina lako kabisa, lakini anakuita, wewe, huyu, yule.
- Kukosoa ovyo ovyo. Sikatai mtu kukosolewa anapokosea, ila unapokosoa hakikisha una lengo la kumuelimisha mkosolewa na sio kumuaibisha au kwa lengo la kujikweza mbele za watu, jambo la kuzingatia zaidi, lugha ya ukarimu itumike.
- Kucheka hadi kwenye serious moments. Wengine sijui huwa ni makusudi au sijui ndo hawezi kuzuia kicheko, yaani mtu hatambui nyakati za kuwa serious, kicheko kikija, yeye anacheka tu! ni kweli kuna jambo linaweza kukufurahisha peke yako na ukajikuta umeshindwa kuzuia kicheko, basi ukacheka. Huenda watu wakakuvumilia wakajua ni bahati mbaya tu! ajabu inakujua pale inapoonekana kuwa wewe sasa umekuwa ni mtu wa kuchekacheka kila muda ni wewe tu!
mkuu umepanga?wananikera sana hawa nduguKukaa au kusimama mlangoni yaani watu utadhani hawajui sehemu maalum za kukaa vile,wao ni mlangoni alafu ukiwa unapita hawakupishi wao kila muda ni kuwaambia naomba nipite tu ni inaboa mpaka basi.
Dah hapa wengi sanaMtu anakuta unasubiri kuhudumiwa iwe Dukani au mahali popote, anakuruka na kuanza kueleza shida yake km wengine waliotangulia hawana haraka
[emoji38] [emoji38]Kuna sheria isiyo rasmi miongoni mwa wanaume kwamba ukinikuta nimesimama eneo hili nikienda haja ndogo (mfano kwenye ile mifereji ya maliwatoni au masinki) wewe utasogea mbali na mimi au mimi nitasogea mbali na wewe. Wanaonikera ni yule anayekuja kukaa karibu na wewe kiasi kwamba anakuangalia dushe lako na kasi ya mkojo.
Sijui hua wanawaza nini.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]i thought niko mwenyewe.....aseee kumbe tupo wengi...umenichekesha sana mkuuTabia ya mtu ya kukatisha mbele yangu wakati natembea huwa inaniudhi sana,unakuta sehemu kama kariakoo jinsi ilivyo na msongamano wa watu tena wako speed halafu mtu anakuona unavyokuja halafu anakatiza tu mbele nusu umvae.
Yani huwa natamani kumtia mtu makofi.