Vijimambo vya wanaume vinavyowakera wanawake...!

Vijimambo vya wanaume vinavyowakera wanawake...!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
Jealous-woman.jpg


Kwa kawaida wanaume na wanawake wanazo tofauti za kimaumbile. Kuna wakati tofauti hizi huweza kusababisha ufa kwenye uhusiano na hata kuangusha kabisa ndoa. Leo nimeona ni vyema kwa wanawake kujua baadhi ya tofauti hizo ili ziwasaidie kuimarisha mahusiano yenu au ndoa zenu:

1. Mwanaume huwa hataki kuambiwa jambo wakati anafanya mambo yafuatayo. Wakati anaangalia mpira kwenye TV ambapo timu yake inacheza, wakati anakula, wakati ndio kwanza tu ametoka kwenye shughuli zake ameingia nyumbani na wakati anasoma kitu iwe ni gazeti, kitabu au taarifa yoyote. Kama mwanamke asipofahamu jambo hilo anaweza kushangazwa na mumewe kwani atakuwa anamsikiliza nusunusu, kwa hiyo mawasiliano yatakuwa hayajakamilika. Wakati mwingine mwanamke anaweza kugundua udhaifu huo na hivyo kutaka kujaribu kulazimisha kusikilizwa kwa makini, hilo ni kosa kubwa sana na linaweza kusababisha mtafaruku ndani ya nyumba.

2. Mwanaume huwa hapendi kumfanya mkewe ajue kwamba, anaangalia wanawake wengine. Kwa hiyo anachofanya ni kuvunja shingo kwa namna ambayo hatabainika. Lakini ukweli ambao wanawake hawaujui, ni kuwa wanaume kimaumbile ni watu wanaovutwa na kuchochewa na vitu vyenye kuonekana kuliko kusikia au kunusika. Mwanamke kujaribu kumzuia mumewe asiwe anavunjia shingo wanawake wengine ni kama vile kumwambia afanye hivyo. Mwanaume kuvunja kwake shingo hakuna maana ya mwanaume huyo kutoka au kutaka kutoka nje ya ndoa.

3. Wanaume huwa wanapenda muda wao wa faragha. Mume anaweza akajikuta tu, anakwenda kutembea mahali, na kurudi akiwa amechelewa kidogo. Kama akimwambia mkewe alikuwa mahali fulani au kwa jamaa fulani, mke hana haja ya kuanza kuuliza na kubabaika hovyo. Bila kumpa mwanaume faragha, anaweza kuingia mahali akachukia nyumba yake na vyote vilivyomo. Lakini hata mwanamke anahitaji faragha pia.

4. Wanaume huwa wanafanya mambo wanayoombwa na wake zao kwa hatua ambazo wakati mwingine zinaonekana kuwa za polepole sana. Mwanaume anaweza kuombwa na mkewe afanye jambo au kitu fulani na akakubali, lakini ikachukua karne kutekeleza. Mke hana haja ya kuzira au kukasirika kwa sababu, mwanaume hufanya mambo kwa kasi na hatua zake mwenyewe. Mwanaume huchukulia mambo na muda, tofauti na mwanamke anavyochukulia. Kuna mambo ambayo kwake hayana haraka na wala siyo ya kuumiza kichwa.

5. Usidanganywe, wanaume wanapenda sana umbea. Kama mume akimsikia mkewe anazungumza umbea, labda kwenye simu anaweza kutikisa kchwa kupinga au kudharau jambo hilo. Lakini mwanaume anapoanza kuelezea habari za watu wengine na kuungwa mkono na mkewe, umbea huo humfurahisha sana. Ukweli ni kwamba wanaume hupenda sana umbea, sema tu wameupa jina lingine, labda wanaweza kusema ni kumjadili mtu. Kwa hiyo mwanamke anapaswa kujua ni umbea upi unaomvutia mwanaume.

6. Mwanaume anapojibu swali kwa kuuliza swali au anapojibu swali kwa sauti ya juu, mwanamke anapaswa kujua kwamba, mwanaume huyo anajaribu tutafuta uongo wa kusema. Kwa mfano, anaweza kuulizwa na mkewe. ‘weekend hii unatarajia kufaya shughuli gani?’ Akijibu kwa kuruda swali, ‘Ninatarajia kufanya shughuli gani?’ Basi, jua hapo anatafuta kusema uongo, inabidi mwanamke awe makini. Lakini haina maana kwamba, uongo huo una maana ya yeye kutaka kufanya jambo baya au kutaka kutoka nje, hapana, siyo lazima. Lakini jambo la kujua ni kwamba, anajaribu kutafuta uongo.

7. Kuna wakati wanawake hubabaika sana wanapoona waume zao wamekaa kinyonge sana. Hukimbilia kuwauliza, ‘vipi mbona leo uko hivyo?’ Mwanaume anapoulizwa hivyo anaweza kujibu, ‘hapana, hamna kitu, nawaza tu.’ Mara nyingi wanawake hawaridhishwi na jibu hilo. Kwa kutoridhishwa, huendelea kuwabana waume zao na kuwafikisha mahali ambapo watawakera. Inabidi mwanamke kujua kwamba, mwanaume pia hutafakari na kuna wakati kutafakari huko huenda kwa kina sana kiasi cha kumfanya kama amekereka. Akishasema, ‘hamna kitu,’ inabidi mwanamke aelewe tu. Anaweza kutafuta muda mwingine ambapo anaona mume huyo anaweza kuwa tayari kuzungumza………………

Nisiwachoshe, nitaendelea kuwaletea vijimambo vya wanaume vinavyowakera wanawake kwa kadiri muda utakavyoruhusu.
 
hahahahahahah Mtambuzi kweli kunavitu vimenichekesha sana na kuvi nilikuw nafanya bila kujijua. Ila hiyo namba mbili hiyo huwa inanitesa sana.

maana wakati mwingine ni kweli navutiwa kumwangalia mwanamke mwingine barabarani pengine kwa umbo lake.
Unaweza kuwa unaendesha gari na mbele yako unamwona mwanamke kwa nyuma akielekea unakoelekea sasa pengine huko juma kunaanza kukuvutia mitikisiko yake unapoendelea kumkaribia na pengine kumpita unatamani kujua na usoni yukoje pengie pembeni amekamaa mamaaa unajiuliza nijeuze shingo nisijeuze, duh hiyo hunipa wakati mgumu sana, ila wakati mwingien unajikuta tu automatic umekwisha geuka ukirudi upande wa pili tayari kama kulikuwa na maongezi yanakata kwa muda au unaona hali ya hewa imebadili na pengine kauso kamekunjwa kiana.

Ila kitu cha kufurahusha hata wanawake wamekuwa na tabia ya kuwaangalia wanawake wenzao mabarabari yaani kama mkikutana na mwanamke mrembo unaweza kumwona mkeo naye navutika kumwangalia na wakati mwingine kwa wivu utasikia anaguna kuwa kweli huyu kanizi. lakini hawataki sisi nasi tuoshe macho yetu
 
Last edited by a moderator:
2. Mwanaume huwa hapendi kumfanya mkewe ajue kwamba, anaangalia wanawake wengine. Kwa hiyo anachofanya ni kuvunja shingo kwa namna ambayo hatabainika. Lakini ukweli ambao wanawake hawaujui, ni kuwa wanaume kimaumbile ni watu wanaovutwa na kuchochewa na vitu vyenye kuonekana kuliko kusikia au kunusika. Mwanamke kujaribu kumzuia mumewe asiwe anavunjia shingo wanawake wengine ni kama vile kumwambia afanye hivyo. Mwanaume kuvunja kwake shingo hakuna maana ya mwanaume huyo kutoka au kutaka kutoka nje ya ndoa.


Hii namba mbili mzee mwenzangu Mtambuzi, unawashauri nini akina dada, wawaruhusu waume/wapenzi wao waendelee kukata shingo kwa vimwana wengine kwa kuwa kuangalia hakumaanishi kutoka nje ya ndoa inhali wao wapo na wangefurahi kuona wanafurahiwa?
 
Last edited by a moderator:
Kaka mkubwa nimesoma kwa makini hoja baada ya hoja na nimetambua kuwa umejaribu kugusa kila kona.
Nadhani wanawake waelewa wakiipitia hii thread na kuisoma kwa makini, hakika wataondoka na kitu muhimu.
Wengi wa wanaume tumekuwa wahanga wa reactions za wanawake kutokana na hivyo vitabia tuvioneshavyo.
Na mahusiano mengi yamevunjika kwa vijitabia hivyo kwani si wanawake wote ni wavumilivu na wadadavuzi wa tabia
 
At last umekubali kuwa wanaume wanapenda umbea. Afu mshua hebu nitafute leo manake nna umbea wa karne.
 
Ha ha ha ha, Daymm yu

Wamesomea umbea, tena hadoi wanaukatia tiketi ya ndege
Kuna mmoja aliwahi ukatia tiketi umbea just kuja kusikiliza nini nkinaendelea mtaani.

Ukitaka kujua ni wambea kiasi gani muulize Roulette

Kupupuuu apupuu kuku eeh?
Wanaume ni wambea hakuna mfano! Yaani mi nikiona mupenzi hanisimulii umbea najua tayari nimeshakuwa overtaken na Kongosho
 
Last edited by a moderator:
NI kweli kabisa usemayo Mtambuzi, hakuna kitu kinakera kama uko na mumeo halafu anatazama mwanamke mwingine, mm huwa nashindwa kushangaa, kiasi siku hizi simuulizi wala simwambii kitu namwacha tu aangalie akimaliza ndipo namuuliza kanizidi nn, basi anabaki anacheka tu. Loh!
Pia hilo la kusoma au kuangalia mechi ukitaka kugombana na mume wangu msemeshe wakati huo anakuwa mkali kama pili pili tena unaweza ukamfanya akatoka kwenda Bar kuangalia hiyo mechi. So siku hizi nikimkuta anaangalia Mpira nasalimia na kupita zangu mpk uishe ndipo tunaweza kuongea. Asante kwa ushauri na kutuelewesha wanawake.
 
Daaaah aisee hata wanawake wanageuka!
 
Asante mkuu Mtambuzi, wanaume ni wasemaji sio wambea jamani, neno umbea its strictly feminine. .
Mkuu Mtambuzi hilo la mpira au saa niko napanga hesabu zangu za ela kwenye laptop mtu ndo anakuja kukusemesha, . .natamanigi nipasuke.
 
Last edited by a moderator:
hapo namba 5 ni kweli wanaume ni wambea kupita kiasi....niliprove hili wakati niko chuo......wanaume wzmnea balaa watungaji wz maneno usipime.... Huko maofisini kwa majungu hawana mpinzani..... Anyway umenikumnusha mkaka mmoja anapenda kuchimba chimba ajue mamno ya watu
 
veeery truuuuh
yani ukishajijuliaga haya ah wala hupati shida!
 
hapo namba 5 ni kweli wanaume ni wambea kupita kiasi....niliprove hili wakati niko chuo......wanaume wzmnea balaa watungajiwz maneno usipime.... Huko maofisini kwa majungu hawana mpinzani..... Anyway umenikumnusha mkaka mmoja anapenda kuchimba chimba ajue mamno ya watu


badili tabia mbona unachemka hovyohovyo,hakuna umbea hapo,watungaji maneno=wazushi,sawa,majungu=fitna,sawa,kuchimbachimba=ufukunyuku,hakuna umbea hapo!jipange urudi upya mtu wangu nakusubiri nikugongee like ukinyoosha maneno........by the way hapo ukisikiliza harufu ya chakula jirani yako rose leo kapika nini?ebu sikilizia mwana unipe habari nikawahadithie kazini kwao kama kalalia ugali matembele(huu sasa ndio mfano wa umbea)
 
usitake kuhalalisha upuuzi wenu,mtu avunje shingo nimtazame tu,mi nina shida nahitaji kusikilizwa yy anasoma gazeti au anaangalia mpira khaa hiyo ndo maana ya ndoa eboooo nitaangalia tamthilia za mara na clara hadi usiku wa manane kwa style hii,USIWAPE KICHWA WENZIO KUNA WENGINE HAWASOMI NYAKATI unawapoteza Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom