Vijana yawapasa mtambue hili

Vijana yawapasa mtambue hili

Furaha ya mzazi ni kuona watoto wake wamekua wakiwa na afya njema na wameondoka nyumbani wakiwa na vyanzo halali vya mapato.

Tunapokuja kwenye graduations zenu msituone tunapiga vigele gele tunafurahia kuwa na sisi tumefanikiwa. Hayo ya kutununulia flat screens na vitenge ni majaliwa.

Hakuna kitu kinatudhoofisha moyoni kama tunapopata habari za masahibu yaliyowakuta. Unaposikia mwanao amefungwa, unaposikia mwanao ana HIV, na mengineyo huwa yanatupa msiba. Hakuna mzazi anaefurahia kuzika mtoto.

Dalili ya mafanikio ya uzazi na malezi yetu ni pale mnapokuja likizo na kuondoka. Si kukaa na kutegemea pension ya mama inatoka lini.

Msitugeuze mayaya wa kulea watoto wenu wenyewe mnawaita wa majaribio. Miaka 20-30 ya ajira yote nilikimbizana kuamka asubuhi niwahi kazini na kulipa Ada za shule. Huyu baba yenu ni muda wake sasa wa kutengenezewa breakfast, tukae tuangalie vipindi vya nature kwenye TV.

Weekend njema.
Ahsante Sky Eclat
 
Na kweli watuache ingawa nimebakiza miaka michache kuchukua pension yangu
Mungu anijaalie afya njema na wewe pia uone na wajukuu zako wakija kukutembelea tu
 
Ujumbe mzuri mama ! Ile ya Ndoa , hii tena ...Barikiwa sana.
Ukipata nafasi tupe uzoefu wako kwenye malezi sisi wazazi wapya tunapambanaje na utandawazi na teknolojia ? Watoto wetu digital sana
 
Ujumbe mzuri mama ! Ile ya Ndoa , hii tena ...Barikiwa sana.
Ukipata nafasi tupe uzoefu wako kwenye malezi sisi wazazi wapya tunapambanaje na utandawazi na teknolojia ? Watoto wetu digital sana
Mkuu mimi mwenyewe nilijiunga na FB 2006 kwasababu nilitaka kufahamu wanayayafanya huko, siku ya kwanza wameniona waliniuliza unafanya nini huku?
Si kila siku lakini kwa wiki anagalau mara mbili nilikuwa ninduatilia mazungumzo yao na rafiki zao pasi ku comment kitu.
Ninayoonabhayafai ninaongea nao.
 
Back
Top Bottom