Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,986
- 189,584
Hakika. Shangazi yangu alidekeza sana watoto wake wooote na kwa bahati mbaya sana baba yao alikuwa anasafiri mara kwa mara ,akaja kupata ajali akapoteza maisha- mbona moto unamuwakia shangazi!Hata Kama una uwezo mfundishe mtoto kuwa maisha ni kutafuta vya urithi asivitegemee.
Wazazi tunao wajibu wa kuwaandaa watoto wetu waje kuwa wazazi bora na waoKuna watoto mama ni pharmasist baba daktari. Watoto wale walifundishwa kupika na wanasugua mpaka sufuria. Na shule wanashindana kwa A’s B’s. Yaani dada ni wa kumhudumia wazazi tu.
Dada upo sahihi sana ila wazazi wa siku hizi in tofauti na zamani,Siku hizi wazazi wapo bize sana hata kupata mda wa kukaa na watoto in ngumu wapo wanaotimiza majukumu kwa watoto japo si wengi.watoto ni baraka tuwalee vyema ili kupata familia bora na jamii njema.Kuna watoto mama ni pharmasist baba daktari. Watoto wale walifundishwa kupika na wanasugua mpaka sufuria. Na shule wanashindana kwa A’s B’s. Yaani dada ni wa kumhudumia wazazi tu.
[emoji106]1. Misingi ya dini
2. Upendo
3. Invest muda na mtoto
Ukimlea mtoto katika misingi ya dini kuna atakavyokumbuka akiwa mkubwa pia hutakua na lawama kwa Mungu.
Mpende mtoto ajue unampenda. Hata kama huna hela ya kutimiza mahitaji yake atakuelewa
Panga muda wa kuwa na wanao, hii ita kusaidia kujua tabia zao na inaweza kuzinyoosha mapema. Angalieni mpira pamoja au hata kwenda nao shamba. Kumbukumbu hizi hazitawatoka kichwani.
Ni kile kitendo cha kufahamu mwanao ana maambukizi ambayo hakuzaliwa nayo. Unamfahamu akiacha kutumia dawa atadhurika. Unaumia ila unabidi ujikaze umfarijiSky Eclat kwa hili sijakuelewa kabisa hasa ulipounganisha hili swala lako na HIV.....kwani ukiwa na HIV huwez kuwa na mafanikio ya kihalali kimaisha ya kiweza kufurahisha wazazi?? Tengua kauli tafadhari.....ajira yangu mi ni hospital.....sio kila mwenye HIV bs anafeli kwnye life na sio kila anayepata ni kuzidisha anasa.....no....wengine ni wahudumu wa afya hupata kwa kujichomba na sindano aloitumia kwa mgonjwa bahati mbaya.
Tuufanyie kazi huu ushauri wa mhenga.Tumeelewa
Furaha ya mzazi ni kuona watoto wake wamekua wakiwa na afya njema na wameondoka nyumbani wakiwa na vyanzo halali vya mapato.
Tunapokuja kwenye graduations zenu msituone tunapiga vigele gele tunafurahia kuwa na sisi tumefanikiwa. Hayo ya kutununulia flat screens na vitenge ni majaliwa.
Hakuna kitu kinatudhoofisha moyoni kama tunapopata habari za masahibu yaliyowakuta. Unaposikia mwanao amefungwa, unaposikia mwanao ana HIV, na mengineyo huwa yanatupa msiba. Hakuna mzazi anaefurahia kuzika mtoto.
Dalili ya mafanikio ya uzazi na malezi yetu ni pale mnapokuja likizo na kuondoka. Si kukaa na kutegemea pension ya mama inatoka lini.
Msitugeuze mayaya wa kulea watoto wenu wenyewe mnawaita wa majaribio. Miaka 20-30 ya ajira yote nilikimbizana kuamka asubuhi niwahi kazini na kulipa Ada za shule. Huyu baba yenu ni muda wake sasa wa kutengenezewa breakfast, tukae tuangalie vipindi vya nature kwenye TV.
Weekend njema.
Ujumbe safi kabisa. Kama sikosei unakunywa Winemaking wewe.pFuraha ya mzazi ni kuona watoto wake wamekua wakiwa na afya njema na wameondoka nyumbani wakiwa na vyanzo halali vya mapato.
Tunapokuja kwenye graduations zenu msituone tunapiga vigele gele tunafurahia kuwa na sisi tumefanikiwa. Hayo ya kutununulia flat screens na vitenge ni majaliwa.
Hakuna kitu kinatudhoofisha moyoni kama tunapopata habari za masahibu yaliyowakuta. Unaposikia mwanao amefungwa, unaposikia mwanao ana HIV, na mengineyo huwa yanatupa msiba. Hakuna mzazi anaefurahia kuzika mtoto.
Dalili ya mafanikio ya uzazi na malezi yetu ni pale mnapokuja likizo na kuondoka. Si kukaa na kutegemea pension ya mama inatoka lini.
Msitugeuze mayaya wa kulea watoto wenu wenyewe mnawaita wa majaribio. Miaka 20-30 ya ajira yote nilikimbizana kuamka asubuhi niwahi kazini na kulipa Ada za shule. Huyu baba yenu ni muda wake sasa wa kutengenezewa breakfast, tukae tuangalie vipindi vya nature kwenye TV.
Weekend njema.
Mimi pia Mkuu. Huyu Dada/Mama huwa ana madini sana. Najua unakunywa Wine,embu pitia hapo kwa Mangi akupe chupa moja then nitumie bili yako nimrushie Mangi.Umenigusa sana... Sky Eclat Nashukuru sana.
Shukran mkuuUjumbe safi kabisa. Kama sikosei unakunywa Winemaking wewe.p
Mimi pia Mkuu. Huyu Dada/Mama huwa ana madini sana. Najua unakunywa Wine,embu pitia hapo kwa Mangi akupe chupa moja then nitumie bili yako nimrushie Mangi.
Ni kweli....lakin kuna baadhi ya mambo ni vema yakabaki kuwa vichwani mwetu tu na sio kuyaexpress kwa uwazi kiasi hcho.......am telling u....yeyote aliesoma huu uzi na ni HIV positive atakuwa amenyong'onyea sana mda huu....yn atakua na masaa matatu au mawili ya kuwaza like "" daah ko mi nakufa mda wowote kwa ukimwi jaman!!?""Ni kile kitendo cha kufahamu mwanao ana maambukizi ambayo hakuzaliwa nayo. Unamfahamu akiacha kutumia dawa atadhurika. Unaumia ila unabidi ujikaze umfariji