Vijana yawapasa mtambue hili

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Furaha ya mzazi ni kuona watoto wake wamekua wakiwa na afya njema na wameondoka nyumbani wakiwa na vyanzo halali vya mapato.

Tunapokuja kwenye graduations zenu msituone tunapiga vigele gele tunafurahia kuwa na sisi tumefanikiwa. Hayo ya kutununulia flat screens na vitenge ni majaliwa.

Hakuna kitu kinatudhoofisha moyoni kama tunapopata habari za masahibu yaliyowakuta. Unaposikia mwanao amefungwa, unaposikia mwanao ana HIV, na mengineyo huwa yanatupa msiba. Hakuna mzazi anaefurahia kuzika mtoto.

Dalili ya mafanikio ya uzazi na malezi yetu ni pale mnapokuja likizo na kuondoka. Si kukaa na kutegemea pension ya mama inatoka lini.

Msitugeuze mayaya wa kulea watoto wenu wenyewe mnawaita wa majaribio. Miaka 20-30 ya ajira yote nilikimbizana kuamka asubuhi niwahi kazini na kulipa Ada za shule. Huyu baba yenu ni muda wake sasa wa kutengenezewa breakfast, tukae tuangalie vipindi vya nature kwenye TV.

Weekend njema.
 
Asante Sky Eclat kwa ushauri mzuri
 
Malezi bora ni kitu muhimu kwa wazazi kukiangalia sana mtoto anapo kosea na kuwa na mwenondo mbaya yapasa kuwa mkali na kumkanya hapo utapata matokeo mazuri kwa kijana wako baadaye
Mfano,kuna kijana tulisoma naye yeye alikuwa mdokozi wa pen na vitabu tukiwa shule kumbe hile tabia aliendelea nayo hadi mtaani juzi nimesikia alienda kuiba sehemu wakampika mawe hadi Roho ikaacha mwili,inatia huzuni kwa familia yake.
 
Shukran mkuu
 
Hakuna kazi ngumu kama kulea na hasa kama mzazi umekosea tangu mwanzo kwa aidha kumdekeza dekeza mtoto akifika umri wa balehe ni janga kubwa- yaan anajiona yy ndio kila kitu hasikii wala haambiwi matokeo yake anakuwa janga.

Umeongea pointi sana Sky Eclat
 
Hata Kama una uwezo mfundishe mtoto kuwa maisha ni kutafuta vya urithi asivitegemee.
 
mlee mtoto katika njia impasayo naye ataicha hata atakapokuwa mzee,naamini mtoto akilelewa vizuri in ngumu kubadilika japo binadamu tubadilika kama kinyonga.
 
1. Misingi ya dini
2. Upendo
3. Invest muda na mtoto

Ukimlea mtoto katika misingi ya dini kuna atakavyokumbuka akiwa mkubwa pia hutakua na lawama kwa Mungu.

Mpende mtoto ajue unampenda. Hata kama huna hela ya kutimiza mahitaji yake atakuelewa

Panga muda wa kuwa na wanao, hii ita kusaidia kujua tabia zao na unaweza kuzinyoosha mapema. Angalieni mpira pamoja au hata kwenda nao shamba. Kumbukumbu hizi hazitawatoka kichwani.
 
Back
Top Bottom