Vijana wengi wana hasira na Zitto Kabwe

Vijana wengi wana hasira na Zitto Kabwe

Joined
Aug 20, 2014
Posts
10
Reaction score
13
Hii topic kuhusu Zitto Kabwe niliweka katika ukurasa wangu wa Instagram nikisema ni mmoja ya vijana wenye ushawishi mkubwa kisiasa nchini na alipelekea vijana wengi kujiunga na Siasa tofauti na hapo mwanzo vijana wengi walikuwa woga.

Nimejifunza mengi kutokana na maoni mbali mbali asilimia kubwa ya maoni vijana wana hasira na Zitto Kabwe. Kama nawe ni mmoja wa wasiomuelewa Zitto, Tuwekane sawa hapa!!! Tatizo la Zitto ni nini? Na nini kifanyike? Pamoja na kumuona Zitto Kabwe ni kijana shupavu, sauti yake inaleta matumaini kwa wananchi! Ameleta mabadiliko sana kwenye fikra za vijana kupenda/kujiunga na siasa.

Mpaka sasa maoni yanayojirudia rudia asilimia kubwa wanasema:-

1. Ni kweli ni mfano wa kuigwa kwa kuwa ana nia njema kusimamia maslahi ya Taifa kwanza Katika umri mdogo amefanikiwa kuwashawishi wananchi kwamba inawezekana kuchukua hatua haijilishi umri wako

2. Ameweza kuonesha ana nguvu kubwa kisiasa ndani ya chama na kuleta mabadiliko ndani ya chama cha chake
3. Vijana wengi wamegawanyika kutokana na "mabadiliko" ndani ya chama kiasi kwamba wengi wanaamini ametumiwa kukihujumu chama.
4. Zitto Kabwe wa 2007 siye wa sasa, kuna mahali ameharibu
5. Pesa na rushwa ni sababisho la vijana wengi wanaoanza vizuri wanamaliza vibaya, wananunuliwa!

Haya ndo maoni niliyopata kuhusu Zitto Kabwe. Wewe kama mpenda mabadiliko. Unaona Zitto yuko sahihi katika siasa zake au anasingiziwa na wanasiasa wenzake? naombeni msaada wenu nakusanya maoni kwa ajili ya kazi maalumu baadae.

Ahsante

Mimi ni katika kundi la watu wanaomkubali sana Zitto na nadiriki kusema kwamba ni mmoja wa mashujaa wangu ambaye kama binadamu ana mapungufu yake. Pia ninawakubali viongozi wengine kama Dr.Slaa na Mbowe ambao pia kama binadamu wana mapungufu yao lakini pamoja na yote haya nitaushutumu uongozi wa Chadema kwa kupoteza mwelekeo. Kifupi ni kwamba Chadema sasa hivi imepoteza nuru walokuwa nayo na sababu ni Unafiki.

Chama hiki kilikuwa tuzo la watanzania wengi na wengi wetu tulitegemea sana chombo hiki kuleta mageuzi nchini lakini walipogeuka na kuanza siasa za ndani toka uchaguzi wa Bavicha ulopita, ugonjwa ule uliingia hadi ndani ya chama na chama kikapoteza mwelekeo maana adui alikuwa mwenza. Kila mtu akawa hamuamini mwenzake,majungu na vitimbi vikazaliwa kushushana wenyewe na mbinu hii waliitegengeneza CCM kiasi kwamba kutoaminiana kukaleta udhaifu ktk uongozi na hata kufikia maamuzi yaloweka ufa mkubwa.

Hivyo, ni lazima tukubali Zitto ana kipaji chake ana mvuto wake na hakika ni mmoja wa vijana ambao mimi nawatazama kwa makini sana kutokana na fikra mpya walizowajenga vijana wetu kutokubali kuburuzwa na kuweka maslahi ya nchi mbele ya Ubinafsi. Hii habari ya mtu mmoja au wawili kuua chama ni kufungashiwa kesi kwa mtu mwenye kutaka mabadiliko ya kisiasa na hakika vyama vyote vya Upinzani vimekumbwa na balaa hii ya kutoaminiana kutokana na kwamba wapo baina yetu na tunakula nao sahani moja lakini walikwisha lishwa sumu mbaya ya Unafiki.
 
Zitto yuko sahihi kabisa, na watanzania wengi bado tuna imani naye!

CHADEMA wanamtenga kwa ajili ya dini yake na kabila lake, pia kwa ajili ya misimamo yake isiyoyumbishwa!

BAVICHA wengi hawampendi Zitto kwa sababu wanafuata mkumbo wa viongozi wao!
 
Last edited by a moderator:
Zitto alipotea maboya pale alipoacha kufuata ushahuri wangu akaona kwamba,ccm wanamthamini sana kumbe walikuwa wanatafuta njia ya kumtoa bungeni,sasa akijaribu kuamia ACT hatopata tena ubunge na ACT haiwezi kupata mbunge hata mmoja na hapo ndipo atakapowajua ccm kwa jinsi watakavyomnogoa
 
Akili ya zito ni zaidi ya viongozi na wanachama wote wa chadema kwa pamoja
 
Nashangazwa humu JF hakuna maada za maana, kila ukifungua ni Zitto weee!!!
Halafu hakuna vitufe vya dis-like, sasa kama mimi sipendi huu uzi inakuwaje ?

MOD ondosha uzi huo!
 
Zitto ni msaliti.....kasaliti kwa lipi? Mwenye ushahidi dhahiri juu usaliti wa Zitto aweke hapa
 
Mkuu vijana gani unaozungumzia mbona mimi kijana halfu sijui hicho unachosema mkuu.
 
Back
Top Bottom