Vijana wengi wamekatishwa tamaa ya Kusoma mpaka ngazi ya PHD Madaktari na Maprofesa wahusishwa

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Kutokana na utendaji mbovu na pia kukosa msimamo kwa sababu ya maslahi yao binafsi wasomi wa Tanzania wamekuwa mfano mbaya sana kwa jamii yetu tofauti na wasomi wa nje. Jambo hili limesababisha vijana wengi kutokuwa na hamu zaidi ya kusoma au kuwaheshimu watu hawa ambao miaka ya nyuma walipewa heshima sana.

Kumekuwa na wimbi la matamshi na matukio ya hovyo kufanywa na watu ambao wanafahamika kama ni Madaktari au Maprofesa kiasi kwamba wameleta maswali mengi sana katika jamii kutokana na kuwa na kuyumbishwa hata na wasio na usomi.

Maprofesa au wasomi wa Tanzania ni kundi linaloongoza kwa kukosa msimamo na kukana hata waliyowahi kuyaandika au kuyanena.
 
Back
Top Bottom