Vijana wengi kwanini mnapenda kula ugoro?

Vijana wengi kwanini mnapenda kula ugoro?

Evz

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
674
Reaction score
130
Kurekebishana tabia hususan kwa vijana wa kiume wengi wao huwa nawaona nikiwa stand za magari pamoja na sehemu za makazi au wanapolinda wamasai.

Vijana wengi huwa wanapenda kula ugoro. Utakuta domo limemvimba utadhani kapigwa ngumi kumbe kajaza ugoro mdomoni.

Enzi za miaka ya nyuma staili ya kula ugoro mara nyingi ilikuwa kwa mabibi na mababu, ila miaka ya hivi karibun vijana nao sijui wanaharibikiwa nanini.

Nimeweka uzi huu ili tupate mawazo na jinsi ya kupata maoni. Ni starehe gani wanapata hawa vijana wa kiume?

Ningependa mtushirikishe kwa mawazo yenu.

Nb matusi hayaruhusiwi.
 
ugoro unalewesha kama pombe...pombe ni gharama sana vijana wengi hawamudu ndio maana wanakula ugoro
 
Wenzetu walipogundua pombe kali kama whiskey tusio na pesa tukagundua Gongo,sasa wenzetu siku hizi wametengeneza SNUS{Pichani}ambayo siku hizi vijana wengi wenye pesa hasa nje ya nchi wanatumia,wao wanasema japokuwa imetengenezwa kwa Tumbaku haina madhara ya moja kwa moja kama sigara na mwonekano wake ni kama ugoro,na sisi tusio na pesa tunatumia ugoro ili kupata stiiimuuuu{onyo ila mimi situmii}



 
Hata mie huwa najiuliza kunani!!

Labda itakuwa bei rahisi au hauna madhara kama madawa ya kulevya/bangi.

Au ugoro sio haramu(not illegal)
Hauko kwny orodha ya madawa ya kulevya.
 
hehehe? Wanaoza hadi meno
 
Toeni majungu hapa,yanawahusu nini?
Bibi yangu kaanza kula ugoro zaidi ya miaka 50 iliyopita,meno mazimaa na meupe pee japo me siutumii ila wabongo mnadharau vyakwenu .
 
Toeni majungu hapa,yanawahusu nini?
Bibi yangu kaanza kula ugoro zaidi ya miaka 50 iliyopita,meno mazimaa na meupe pee japo me siutumii ila wabongo mnadharau vyakwenu .
kwahiyo kama bibi yako kanywa gongo kwa zaidi ya miaka 50 unawashauri vijana nao waige tabia ya bibi yako?
 
Kitu mtu kaamua mwenyewe kula we kinakuumiza kichwa kwann?binadamu wote ni sawa ila kila mtu ana akili yake na mawazo yake.we ukipenda hiki mwenzio anapenda kile so ucpate tabu.
 
Njoo mbuguni arusha uone watu tunavyobwia ugoro stimu yake ni noma chalii yangu, wabongo nyie mmezoe miguu ya kuku na utumbo wake mastimu hamuyajui kaeni na mafoleni yenu.
 
jana tu nilikua na mtu mzima wa heshima zake,anakula ugolo huyo balaa!
 
kuber ilikuwa inauzwa madukani serikali ikapiga marufuku sasa vijana wanatumia ugoro!
 
ila jaman ugoro? Yanini yote? Stimu gani mnazipata?
 
ila jaman ugoro? Yanini yote? Stimu gani mnazipata?

Hii stimu yake ni kama kahawa chungu. inasadia kwa mtu anaetaka kuacha kuvuta sigara kwa kua ina nicotine ndani yake.
 
kwahiyo kama bibi yako kanywa gongo kwa zaidi ya miaka 50 unawashauri vijana nao waige tabia ya bibi yako?

Kaka umeniamlia aisee,sio gongo tu Mbona wazungu wanakunywa ma grants hamsemi au kwakuwa ni localmade?ugoro uliwe tu nawasilisha.
 
hivi nicotin si inamadhara kw binadamu?
 
Sasa mimi nashangaaa mume akiwa anakula ugoro Mke atamla vipi denda mumewe?
 
Back
Top Bottom