Konda wa bodaboda
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 7,981
- 4,172
Nimepita sehemu nyingi tu kwa mizunguko ya maisha tangu nikiwa nasoma hadi kufanya kazi.
Katika mazjngira ambayo nimebahatika kuwa ndani yake nimejifunza mengi kuhusu mahusiano na nikajikuta najisemea moyoni tu kwa kuona kuwa wale mabinti kuanzia miaka 18+ wameshashindikana na hawaendani kisaikojia na vijana wa kiume wa rika lao hilo.
Nimesema hivyo kwa kuwa unakuta binti wa miaka 20 ana-date na mzee mwenye miaka 40+ sawa na baba yake unadhani siku akija ku-date na kijana wa umri wake atajisikiaje?
Jambo moja nililoliona ni pesa tu ambapo unakuta kwa kuwa vijana wengi wa miaka 20+ wanakuwa ni kula kulala kwao basi wanakuwa hawana pesa za kuwahudumia wadada ambao kwa kweli wengi wao ni pesa mbele.
Sasa hawa wazee wanaotoka na mabinti wadogo wanakuwa na familia zao mke na watoto juu, kwahiyo huwarubuni mabinti hawa kwa huduma za muda mfupi tu, kwa kuzingatia hilo ndio maana hata maambukizi ya VVU kwa vijana wa kike ni makubwa kulinganisha na vijana wa kiume, sababu kuu ndio hiyo niliyoitaja hapo awali.
Pitia kwenye taasisi za elimu kama shule na vyuo, makampuni, na maofisi makubwa mbalimbali utakuta walioshika nafasi za juu ambao wengi ni wazee ndio wanatoka na ma-secretary wao ambao unakuta ni vibinti vidogo sana kama watoto zao.
Vijana wa kiume wamekuwa chaguo la pili kwa hawa wadada kwa kuwa wengi wao hawajajijenga kiuchumi kama nilivyotangulia kusema hapo juu. Kwa mantiki hiyo nimegundua kuwa mabinti wengi(sio wote ila walau kwa 90%) wanaopitia mazingira hayo yenye ushawishi mbaya kabisa wanakuwa ni wasaliti wakubwa kwenye ndoa pindi watakapoolewa, na wengi wao hukubali kuolewa tu na vijana wenzao baada ya kushtuka umri umeenda na wazee wamewapiga chini.
Vijana amkeni, wekeni wazee wanawaibia hasa wale wenye wapenzi vyuoni, mashuleni na makazini.