Vijana wanapoichukia CCM

Dawa ya Malaria

New Member
Nov 8, 2010
4
0
HATA Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa hakumung’unya maneno amelisema wazi kuwa vijana wanaichukia CCM na ndio waliifanya ipoteze majimbo hayo 58 katika uchaguzi uliopita.

Akamwomba Pinda pamoja na kazi zake zingine, atafute chanzo cha vijana kuichukia CCM na alitafutie ufumbuzi suala hilo.

Zipo sababu nyingi mimi ngoja nijitose kumsaidia Pinda ili atakapokuwa anaanza kazi alione hilo na alishughulikie haraka. Kwanza ni ukosefu wa ajira.

Vijana wengi wanamaliza shule wanajikuta hawana ajira. Hata wale wanaomaliza masomo ya vyuo vya elimu ya juu wanasota majumbani bila kupata ajira.

Kijana wa namna hiyo kamwe hawezi kuipenda CCM kwani ana njaa. Anaona watoto wa wakubwa waliomaliza naye chuoni tayari walishapata ajira na wanakula kuku kwa mrija.

Tena watoto hao wa wakubwa wamepata kazi sehemu nzuri. Wamepata kazi TRA au BoT na ndani ya miezi sita utamwona anaendesha gari zuri na ana nyumba yake ya kifahari.

Yeye mtoto wa mkulima au yule ambaye amezaliwa katika familia ambayo sio bora, pamoja na kisomo chake ataendelea kusaga lami hadi kiatu alichotoka nacho chuoni kinakuwa upande.

Hapo unatarajia nini huyo kijana awe mzalendo? Lakini pia vijana hao hawaipendi CCM kwani wanaona wazazi wao wanaosota huko vijijini wakilima bado hawajakombolewa.

Kwamba maisha ya wakulima hao yameendelea kuwa ya kimasikini hali inayowafanya wajiulize hivi wamekosa nini kwa taifa lao.

Watoto wa wakulima hao wanaosomeshwa kwa shida na wazazi wao kamwe hawawezi kuwa na mapenzi na chama tawala.

Ni lazima wataichukia kwani wanaamini kuwa watawala ndio wanaowanyonya wazazi wao na kuwawasababishia umasikini huo.

Hao ni kwa vijana wasomi. Njoo kwa vijana ambao wamemaliza kidato cha nne au darasa la saba.

Hawa ndio wabaya zaidi kwani wanaamini kuwa kukosa kwao nafasi kwenda masomo ya juu kumetokana na wao kusoma shule zisizo na ubora.

Kwamba pamoja na nia nzuri ya Serikali ya kuzijenga shule hizo, lakini ukosefu wa walimu, vifaa vya kufundishia na vitabu vimezifanya shule hizo maarufu kama voda fasta zisiwe zinafaulisha wanafunzi wa kwenda kidato cha tano kwa wingi kama zilivyo shule zingine.

Hivyo ndugu yangu Pinda jibu ni kwamba wale vijana wanachofikiria ni kwamba zile shule kwa kuwa hawasomi watoto wa viongozi ndio maana zimeachwa yatima kama zilivyo.

Kwamba watoto wa wakubwa wanasoma shule za English Academy au wanasomeshwa nje ya nchi.

Vijana hao wakishafikiria hivyo na kuona matokeo yao ya kidato cha nne ni mbaya na wasichana wanaishia kupata mimba wakiwa masomoni kutokana na ugumu wa mazingira, kamwe hawawezi kuipenda CCM.

Wanataka nao shule wanazosoma ziwe na vifaa, maabara, walimu na mabweni ili nao waweze kusoma vizuri kama watoto wa Watanzani awengine.

Kama shule hizo hazitaboreshwa ni wazi kuwa vijana hao wataendelea kuichukia CCM hadi wanakwenda makaburini.

Kwa hao ambao wamemaliza la saba, hao zaidi wanaibukia kwenye kilimo. Kilimo ambacho nacho hakina tija iwapo atakuwa kijijini.

Atalima mwaka wa kwanza akiona kilimo hakilipi anaondoka kwenda mjini kusaka ajira bila elimu. Akishafika mjini nako kuna matatizo anaishia kuwa kibaka au mpiga debe.

Shida anazozipata kwa kujiingiza kwenye vitendo hivyo mwisho wake sio mzuri. Atakamatwa na polisi na hivyo lazima aichukie Serikali na chama chake.

Iwapo watawala mtaliona hilo na Pinda na viongozi wenzake wakaamua kulishughulikia, kamwe CCM haitakuwa na wakati mgumu kwenye uchaguzi kama huu uliopita.

Lakini mkiachia hali iendelee hivyo nina hakika mwaka 2015 hali itakuwa mbaya zaidi kwa chama hicho kikongwe kwani vijana hao sio waoga na watadai mabadiliko hata ikibidi kwa kumwaga damu.

Si mmeona mifano ya Nyamagana, Ilemela, Mbeya, Arusha, Karagwe, Kawe, Ubungo na Sumbawanga ambako baadhi ya maeneo polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi. Kwa mtindo huo jifunzeni tafadhali!
 
Ngoja nikusahihishe kidogo kuhusu Lowasa; huyu siyo Waziri mkuu mstaafu, bali ni waziri mkuu wa zamani. Kustaafu ni kuachia madaraka baada ya kumaliza kipindi chako au kuamua kupumzika kwa hiari yako; ukifukuzwa au kulazimishwa kujiuzulu kabla kipindi chako hakijaisha huwezi kusema umesataafu.
 
Kwa Tanzania ni mstaafu; na anapokea marupurupu kama wastaafu wengine!
 
Ngoja nikusahihishe kidogo kuhusu Lowasa; huyu siyo Waziri mkuu mstaafu, bali ni waziri mkuu wa zamani. Kustaafu ni kuachia madaraka baada ya kumaliza kipindi chako au kuamua kupumzika kwa hiari yako; ukifukuzwa au kulazimishwa kujiuzulu kabla kipindi chako hakijaisha huwezi kusema umesataafu.

Umesahishisha pia ukakosea

WAZIRI MKUU WALIYEJIUZURU KWA KASHIFA YA RICHMOND
 
Afadhali Malaria Sugu kapata dawa yake!! Hili swala lavijana linakuwa ni kitendawili ila kwa knowledge yangu ni kwamba majority ya vijana wanaizimia sana CDM na wako tayari kufanya lolote! huwezi amini hili! hiyo propaganda ya sijui vijana wa DOM na bla! bla! ni za kuzusha tu! zilitengenezwa kwa manufaa ya kuzua moral panic kwa CDM
 
Suala la vijana ni bomu lililoandaliwa na mafisadi wenyewe. Sasa limeanza kufukuta wameanza kulaumiana. Wamechelewa sana!
 
Swali ni zuri, lakini aliyeuliza hilo swali ....

Ndg Malaria Sugu mkimaliza mjadala chonde unifahamishe, natoka kidogo.


Niwashilishe hivo hivo tu!!
 
Swali ni zuri, lakini aliyeuliza hilo swali ....

Ndg Malaria Sugu mkimaliza mjadala chonde unifahamishe, natoka kidogo.


Niwashilishe hivo hivo tu!!
Aliyewasilisha hoja sio malaria sugu bali ni dawa ya malaria yani kiboko yake malaria sugu.
Mimi naona wamechelewa sana na uchungu walionao vijana ni noma. Mimi nilikuwepo pale loyola siku ya kulinda kura za ubungo niliona hasira walizo nazovijana na uchungu wa kuonewa na kunyanyaswa ni wa hali ya juu. Yani walidiriki kushambulia gari kwa kuhisi tu ni wachakachuaji. na hii wote tuliona maeneo mbalimabali. Kama sisiem hawajajifunza basi sikio la kufa .......
 
Vijana wengi wa Tz wanaishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom