bushland
JF-Expert Member
- Mar 6, 2015
- 7,015
- 4,999
Jamani baada ya vijana mbali mbali kupata taarifa juu ya watalii wa kizungu wanaotalii Arusha kuwa na mahusiano na vijana wa kiswahili(black) na kutoka kimaisha kama vile kununuliwa magari na kujengewa nyumba, idadi ya vijana wameongezeka kwa kiasi kikubwa na wengi wao wameonekana maeneo wanayotalii wazungu jijini hapa pamoja na sehemu wazungu wanakopenda kupata msosi na chai.
Leo mida ya mchana nikiwa sehemu nakunywa kahawa kutokana na baridi hapa, basi kuna kijana mmoja alikuja na kukaa kwa pembeni yangu basi akaniuliza, samahani naomba kuuliza " Eti ni wapi wanapopenda zaidi watalii kukaa au kutembelea kwa hapa mjini?" Bila hiyana nikamjibu machimbo yote ya wazungu, basi pale pale akachukua simu na kumpigia mtu(nafikiri ni kijana mwingine kulingana na mazungumzo Yao) lengo akimjulisha kuwa ameshapata taarifa vipi na yeye huko aliko amepata taarifa gani?
Juzi nikiwa na mizunguko yangu basi kuna hotel flani wanayopenda sana kula na kunywa Wazungu nilikuta vijana zaidi ya kumi wamesimama kwa nje wakisubiri wazungu watoke nje ili waambatane nao kila mtu akiwa na nia yake( wengi huwatongoza wazungu hao bila kujali kama ni mzee au vipi).
Kweli jamani haya maisha tuna mengi ya kujifunza.
Karibuni sana Arusha kila mtu ana bahati yake.