Vijana, wadau kumchangia aliyemtukana Rais Magufuli

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,156
Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.

Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.

Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (CHADEMA), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh800,000 ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.
 
Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.

Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.

Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (CHADEMA), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh 800,000 ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.

Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.

"Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Tutachangia kwa uwezo wetu kutokana kwamba sheria hizi zinatuhusu wote .Kesho unaweza kukamatwa wewe ukakosa msaada wowote lakini siungi mkono watu kumtukana Raisi ni kutoa hoja kwa lugha nzuri.
 
Jaman Huyo Si Mwanachama Mzuri Wa UKAWA Sasa Mbona Michango Inachelewa Hivyo Wakat Hiyo Ni Pesa Mbuzi Tu Kwa VIONGOZI Wa UKAWA.
Mchuma Janga Hula Na Wakwao. Sasa Hapo Atashika Adabu Kweli.

Mnapokuwa Pamoja Mengi Mnadanganyana, Mara Mtawanyikapo Kila Mtu Na Msalaba Wake.

Sasa Hapo Inaumia Familia Yake Kwa Utovu Wa Nidhamu.

Wanasiasa Wanajuana Wao Wakitukanana Ni Sawa Lakn We Usie Mwanasiasa Jaribu Uone.
 
Nimeona hiyo taarifa MWANANCHI, CHADEMA waweke kwenye website yao tumchangie chochote kidogo tulichonacho, nimeona familia yake imesema ina mil 3.5 ila kwa kuwashirikisha wadau tunaweza kuchangia hata zaidi ya mil 7. Si kwamba tunachangia kutetea kosa alilolifanya la hasha, tunachangia kwa sababu ya sheria kandamizi kuhusu uhuru wa mitandao.
 
Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.

Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.

Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh 800,000 ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.

Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.

"Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
Kweli CDM ni Chama ambacho kimepoteza uelekeo paka kufikia kumtetea mtukani na asiye na nidhamu
 
Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.

Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.

Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh 800,000 ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.

Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.

"Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
Nice move! CDM/CCM na wote wapenda haki mchangieni. hii ni sheria kandamizi. Penalty is not proportional to the offense committed!
 
Hii serikali ingekuwa kweli inafatilia mambo, basi awamu ya 4 tungefungwa wengi mno waropokaji naamini hata jf isingekuwepo hewani
 
Back
Top Bottom