Vijana wa UDOM tuna malalamiko kwa January Makamba

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
886
206
Wana jamvi kwa ufupi zaidi,mwaka 2010 ndugu j,makamba alikuja udom akakusanya wanafunzi wote wanao tokea tanga na wakutoka mikoa mingine,tukaitika kwa wingi katika kikao kile akaomba tukamsaidie bumbuli kupiga kampeni achaguliwe kuwa mbunge kuanzia kura za maoni CCM.

Baadae katika uchaguzi mkuu kwa ahadi kuwa vijana wote watakao msaidia akipata ubunge atawasaidia kupata ajira za maana popote pale.
Kama kawaida ya wasomi sisi vijana tukaorodhesha majina yetu na tukaenda bumbuli kwa umoja wetu,tukamsaidia harakati zote mpaka akapata ubunge kirahisi. Baada ya kampeni akagawa namba zake na email kila mtu amtumie cv zake tukafanya hivyo mwaka wa 4 sasa hakuna aliepata hiyo ajira hata ya kusambaza bili za maji mitaani.

Ukimpigia simu hapokei kabisa kwa sasa,hivyo vijana kuweni makini ccm hakuna mzuri hata awe nani wote wanaishi kwa ujanja ujanja tu! Wale wanao jiita walimu vijana kuweni makini.
 
Hizo ni propaganda jinsi ya kumchafua tu jamaa kwa saiv ni gumzo na ni chaguo la wengi j makamba for 2015
 
C.C.M Ikimteua Makamba Awe Mgombea Urais Na Akashinda Urais,moods Na Watanzania Wote Nawahakikishia Kuwa, Nitabadili Uraia wa Taifa Hili Nakuwa Raia Wa Kenya Kukwepa Fedhaha Ya Kuongozwa Na Wahuni.
 
Ina maana hata zile smart phone hakuwapa ili wafungue facebook na kuhara hapa jf? Hayo kwa maccm ndio maendeleo na maisha bora kwa kila mtanzania!
 
Kama ulimtumia CV endelea kusubiri labda bado hajapata. Kutafuta kazi kunahitaji uvumilivu bwana mdogo
 
Wana jamvi kwa ufupi zaidi,mwaka 2010 ndugu j,makamba alikuja udom akakusanya wanafunzi wote wanao tokea tanga na wakutoka mikoa mingine,tukaitika kwa wingi katika kikao kile akaomba tukamsaidie bumbuli kupiga kampeni achaguliwe kuwa mbunge kuanzia kura za maoni ccm na baadae katika uchaguzi mkuu kwa ahadi kuwa vijana wote watakao msaidia akipata ubunge atawasaidia kupata ajira za maana popote pale,kama kawaida ya wasomi sisi vijana tukaorodhesha majina yetu na tukaenda bumbuli kwa umoja wetu,tukamsaidia harakati zote mpaka akapata ubunge kirahisi,baada ya kampeni akagawa namba zake na email kila mtu amtumie cv zake tukafanya hivyo mwaka wa 4 sasa hakuna aliepata hiyo ajira hata ya kusambaza bili za maji mitaani,ukimpigia simu hapokei kabisa kwa sasa,hivyo vijana kuweni makini ccm hakuna mzuri hata awe nani wote wanaishi kwa ujanja ujanja tu! Wale wanao jiita walimu vijana kuweni makini

Kaka sasa nimeg'amua kuwa ile thread uliyoanzisha kuhusu maendeleo ya Bumbuli ulisukumwa na maslahi binafsi. Kama ni maendeleo ya jimbo, January amefanya makubwa kuanzia mikopo nafuu, barabara, umeme na kikubwa zaidi kutimiza ahadi ya kuwapatia wananchi wa Bumbuli halmashauri ili kusogeza na kuharakisha maendeleo.

Siwezi kusema kuhusu ahadi yako kwa sababu sina uhakika kama; wewe ulikuwa mwanafunzi wa UDOM, Makamba aliwachukua kwa ajili ya kampeni, na mwisho, kama kweli aliwaahidi. Inawezekana wewe ni mtu unayefanya kazi kupaka matope tu.
 
Mzee Shelu kakaa miaka 15 kashindwa maji Bumbuli mjini. Makamba kapeleka mradi umeisha watu wanakunywa maji ya bomba. Kuna miradi ya Maji ya Mgwashi (bilioni 1.6), Soni (milioni 418), Kwekitui (milioni 390), Kweminyasa (milioni 365). Hii inatekelezwa sasa. Huko nyuma watu Hawa walikatishwa tamaa ya kupata Maji. Umeme: nenda Vuga kawaulize. Miaka yote wameomba umeme hawapati. Ndani ya miaka miwili umeme umefika. Tangu 2010 vijiji vipya 27 vimepata umeme. Shirika la Maendeleo Bumbuli lina ofisi Soni na hadi sasa wametoa mikopo ya shilingi 250 milioni. Majani ya Chai: Mwaka 2010 bei ilikuwa shilingi 103 kwa kilo, sasa hivi ni mara mbili shilingi 206. Uliza wakulima. Na hili alilisimamia mwenyewe January akiwa Bodi ya Chai. Barabara mbili za Bumbuli (Soni - Mponde - Tamota - Kerenge na Mbelei - Mgwashi-Milingano - Mashewa) zimepandishwa daraja kazi hii ilimshinda Mzee Shelu kwa miaka 15. Pia Bumbuli sasa ni Halmashauri ya Wilaya, ina bajeti yake ya shilingi bilioni 19. Huko nyuma haikuwepo. Wewe inaelekea umejawa chuki na wivu. Watu wa Bumbuli wanampenda saaaana Makamba. Hata kwa greda hatoki.
 
teh teh teh mkuu ukiamka ndiyo utagundua kama ulikua unaota, ni watanzania gani wa kumpa urais makamba? Labda wote tuwe tumetumi sembe inayouzwa na rafki yake r.i.z

wewe ni mkimbiz sasa kundi kubwa la vijana tunamtaka j makamba awe mgombea na tuko tayal kuongozwa naye
 
Mwadilifu ni yule anayejua kwamba kuna watu wanyonge ambao hawali hata milo mitatu kwa Siku. Mwadilifu ni yule anayeweza kuwatetea wanyonge ambao hawana hata uwezo wa kujitete.
Mwadilifu ni mtu anayeweza kushuka na kusikiliza hali ya watu wa chini na kutafuta namna ya kuwainua.
Siku zote narudia siku zote mwadilifu hawezi kuwa mzurumaji. Kama makamba yupo hapa jamii forum katika jukwaa hili hebu akanushe ikiwa hajamdhurumu mfanyakazi wake katika microfinance iliyopo sonny kule bumbuli. Ambae slip salary inaonesha kabisa alikuwa anakatwa makato yote na kuonesha kwamba anapeleka ppf. Lakin mpaka Leo yule dada hajapewa stahiki yake.
Ifikie muda uadilifu uanze kwa wanyonge sio unajisahau na kuwaumiza wanyonge.
Na hili linaniambia hata PAYE hakuwa anapeleka kwa hiyo ameidhurumu serikali. Mimi sina siasa chafu maana makamba hawezi nisaidia lolote maana professional yangu wala hawezi kujilinganisha nami ni tofauti kabisa. Makamba uwe muadilifu lipa pesa za watu mbona ni kidogo sana??
 
wewe ni mkimbiz sasa kundi kubwa la vijana tunamtaka j makamba awe mgombea na tuko tayal kuongozwa naye

Acha kujitekenya na kucheka mwenyewe,, hilo kundi kubwa la vijana unalosema ni lipi? Au unamaanisha nini unaposema kundi,

Njaa na ikae tumboni, ikihamia kichwani ni janga kubwa.
 
Wana jamvi kwa ufupi zaidi,mwaka 2010 ndugu j,makamba alikuja udom akakusanya wanafunzi wote wanao tokea tanga na wakutoka mikoa mingine,tukaitika kwa wingi katika kikao kile akaomba tukamsaidie bumbuli kupiga kampeni achaguliwe kuwa mbunge kuanzia kura za maoni CCM.

Baadae katika uchaguzi mkuu kwa ahadi kuwa vijana wote watakao msaidia akipata ubunge atawasaidia kupata ajira za maana popote pale.
Kama kawaida ya wasomi sisi vijana tukaorodhesha majina yetu na tukaenda bumbuli kwa umoja wetu,tukamsaidia harakati zote mpaka akapata ubunge kirahisi. Baada ya kampeni akagawa namba zake na email kila mtu amtumie cv zake tukafanya hivyo mwaka wa 4 sasa hakuna aliepata hiyo ajira hata ya kusambaza bili za maji mitaani.

Ukimpigia simu hapokei kabisa kwa sasa,hivyo vijana kuweni makini ccm hakuna mzuri hata awe nani wote wanaishi kwa ujanja ujanja tu! Wale wanao jiita walimu vijana kuweni makini.

tatizo la vijana tulio wengi huwa tunaendekeza njaa na shida zaidi, huku tukijidhalilisha na kuuza utu wetu kwa ahadi hewa tena kijinga, kwnza nianze kwa kusema, january makamba hagawi ajira kwani ye nani? pilim yeye mwenyewe alivutwa mkono na baba yake baada ya baba yake.
 
Back
Top Bottom