Ujumbe wa Bollen Ngeti kwa Membe, Kinana na Makamba Senior

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
MEMBE, KINANA, MAKAMBA EPUKENI UPUMBAVU WA JANUARY, NGELEJA NA NAPE, MTAMALIZWA!

Na Bollen Ngetti

SIASA za kutukanana na kuombana misamaha hadharani ni siasa mpya ndani ya CCM na nchini kwa ujumla. Ni siasa za majitaka tusizotakiwa kuendekeza hata kidogo.

Kwanza ieleweke kwamba katika siasa hakuna matusi. Hivi tunajua matusi? Kwenye siasa kuna vijembe, kejeli, mizaha, hoja, ukiita matusi sawa lakini hawaombani misamaha mbele ya kamera.

Mfano; Mwenyekiti wangu Rais Magufuli inadaiwa kina Nape walimwita "mshamba na limbukeni wa madaraka" hili ni tusi kweli. Kama mwanasiasa nilitegemea Magufuli naye kutafuta jukwaa na kuwapa za usoni mfano; "sawa mimi mshamba na limbukeni wa madaraka lakini si mimi ndiye Mwenyekiti wenu wa chama na Rais wenu? Nani mshamba sasa". Kwa kauli hii vijana hawa wangekaa kimya na maisha yangeendelea nao wangeendelea kufanya siasa.

Huku kuomba msamaha kunajenga picha mbili kwanza unayeomba msamaha hujiamini na huamini kauli yako na kuusimamia. Pili inatujengea Picha hasi kwa Mwenyekiti kwamba si mpambanaji wa kisiasa. Kwamba ni mtu wa visasi. Hili si sahihi.

Kama mlimuona Rais mshamba na limbukeni wa madaraka kwa nini msisimamie hilo na kutoa sababu za kushawishi wengine tuamini huo ushamba na ulimbukeni wa Mwenyekiti? Kumbe mlijua mnatenda kosa ndio maana sasa mnajidhalilisha kutubu? Ni lini tutapata mwanasiasa makini na jasiri wanaoamini maneno yao?

Kwani hamkuwa na ushahidi wa maneno mliyosema dhidi ya Rais ? Mmempa Magufuli karata nzuri sana ya kuwamaliza. Lakini pia kumbukeni January, Nape na Mwigulu 2016 niliwaandikia kuwa, " enyi vijana watatu Nape, January na Mwigulu ondokeni peke yenu mtaaibishwa hamtakiwi" mkapuuza. Sasa mmekatwa si mikia tu bali hadi macho ya kisiasa mmetobolewa. Kwani mnaogopa nini kufukuzwa CCM? Kwani siasa ni mpaka uwe CCM? Jinga kabisa.

Nape ni miongoni mwa mwanasiasa vijana aliyejijengea umaarufu kutokana na misimamo. Kwenye hili unakosea wapi? Ngeleja sitaki kumsemea maana ni msaka tonge wa kawaida aliyeingizwa kwenye siasa na Rostam Aziz kwa kazi maalum ya kufanikisha dili la Dowans. Tumweke pembeni lakini Nape ni zao la siasa. Kwa nini Leo ajidhalilishe namna hii?

Tujenge utamaduni wa kushindana kwa hoja na kusimamia unachoamini mwanzo mwisho hata kama kwa kufanya hivyo kutakugharimu jasho na damu.

Nitasikitika na kuumia siku nikiona Bernard Membe naye akibisha hodi Ikulu kwenda kutubu kwa "makosa" yake. Atambue huo utakuwa ni tamati ya maisha yake kisiasa kitakachofuata ni kwenda kuwinda ngiri kijijini Rondo huko Lindi. Haki kadhalika Mzee Kijana na Makamba japo siwaamini sana maana hawana ambition ya madaraka ya kisiasa kama Membe. Lakini all in all hawapaswi kupitia njia walimopitia vijana wao waoga wa vivuli vyao. Kosa la mauti kisiasa.

Mwisho nitoe wito kwa upinzani kuacha kubweteka na yanayoendelea huku kwetu na kuyashadadia. Katika political science the more you talk about us ndivyo tunavyojijenga kisiasa maana vichwani kumejaa Nape, January, Membe, Kinana nakadhalika. Mnasahau kuwa tunaelekea uchaguzi Mkuu. Ni wakati wa kutafakari na kuunganisha vyama vyote vya upinzani na kumpata strong candidate atakayepambana na mgombea wa CCM ambaye hajatangazwa.

Ni wakati wa kutafuta pesa za kampeni kwa njia za uwazi bila kutegemea ruzuku. Kampeni za Urais ni fedha nyingi anzeni sasa. Nunueni vyombo vya habari hasa local radios stations. Sijui kama mnanielewa maana natamani tuzifundishe nchini JIRANI demokrasia.

2020 sitopenda kuona utitiri wa wagombea Urais. Badala yake wawe wawili tu? Vivyo hivyo nafasi za Ubunge. Ili hatimaye Bunge na Serikali visimamie maendeleo kwa hofu kuogopa kung'olewa next time.
#AchaWoga2020
#MguseniAnuke

1568198841007.jpeg
 
Hao wazee hawaa mchango tena...wanahitajika vijana wa IT na vijana wa goli la mkono...hao wengine wazee chukueni.
Naona ufipa mlikuwa mmewategeshea kama vulture hivi. Wamewapiga chenga ya mwili huko ufipani mbanane wenyewe...
Na boeing imerudi mwambieni nyalandu a membe.
 
View attachment 1204382
Mawazo yako ni sawa nakikongwe mwenye ukurutu mavi kasoro kujinyea
 
Nimeona mahalai ameandika "Mgombea wa CCM ambaye hajatangazwa" Angejua hata TLP na Bashiru washatangaza rasmi angefuta kauli. Ila siwezi jua, labda ni kweli.
 
Huyu Kijana ni kichwa!

Sidhani kama Membe anaweza fanya huo ujinga!

Sidhani!
 
Huo ndo 'ushamba wenyewe na limbukeni' wa mwenyekiti wa CCM .... tena mimi nashangaa unasamehe mtu mbele ya camera na kumtesa mtu kutembea muendo mrefu hivo kumzalilisha ili upate kiki na sifa, mimi sijui katika dini ya kikatoliki ila kwa dini yetu, nafsi na nia yako ndo vinavyosamehe mtu, hamna haja ya kudhalilisha mtu ukiwa umeamua kumsamehe inakua sili yako na mola wako.
 
Hao wazee hawaa mchango tena...wanahitajika vijana wa IT na vijana wa goli la mkono...hao wengine wazee chukueni.
Naona ufipa mlikuwa mmewategeshea kama vulture hivi. Wamewapiga chenga ya mwili huko ufipani mbanane wenyewe...
Na boeing imerudi mwambieni nyalandu a membe.
Hivi Bollen ni wa ufipa? Yaani nyie mtu wenu akiwaambia ukweli basi sio mwenzenu tena bali wale wanafiki ndio mnaona wa kufa na kuzikana?
Acheni ubwege nyie!
 
Angalia majibu ya mwenzako 👇👇 hapo chini
Mawazo yako ni sawa nakikongwe mwenye ukurutu mavi kasoro kujinyea
 
Nape walah sijaamini bado nilikuwa namuona at least ana akili akili lkn kwa jana na kitambi yake alivyokuwa anapepea kwenda kuomba msamaha nkaona ujinga huu, lkn pia nadhani wanategemeana wale Mzee wa bao la mkono apate ubunge asikatwe na Meku kwa bao la mkono sio bure
 
Ushauri aliowapa upinzani ni mzuri na wauzingatie maana ugomvi wa watu wa nyumba moja sio vyema sana kuushadadia wanaweza patana any Time T mkabakia mnashangaa na muda umeisha.
 
Huo ndo 'ushamba wenyewe na limbukeni' wa mwenyekiti wa CCM .... tena mimi nashangaa unasamehe mtu mbele ya camera na kumtesa mtu kutembea muendo mrefu hivo kumzalilisha ili upate kiki na sifa, mimi sijui katika dini ya kikatoliki ila kwa dini yetu, nafsi na nia yako ndo vinavyosamehe mtu, hamna haja ya kudhalilisha mtu ukiwa umeamua kumsamehe inakua sili yako na mola wako.
CCM ndiyo inapowashinda upinzani. Wanatengeneza movie na nyie mnaingia king. Mambo mengine mnasahaulishwa mwezi wa tatu sasa mnawajadili wao. Likimalizika hili mnaletewa picha nyingine mkistuka uchaguzi unaingia wanawapatia mpaka mgombea wa urais na Ilani yao iliyokopiwa. Mtazinduka lini?
 
Huwa Najiuliza, katika wote hao Yanayosemwa makosa yao nineyasikia....

Je... MEMBE ana Kosa gani?
 
Hivi Bollen ni wa ufipa? Yaani nyie mtu wenu akiwaambia ukweli basi sio mwenzenu tena bali wale wanafiki ndio mnaona wa kufa na kuzikana?
Acheni ubwege nyie!
Kwenye msafara wa membe kun kenge...kwnye msafara wa chimpanzee kuna baboon pia...
 
Back
Top Bottom