Vijana wa tz na sera za ccm

Vijana wa tz na sera za ccm

wemma

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
230
Reaction score
164
"Ukimwona kijana anashabikia na kukereketwa na CCM leo, ujue akiwa mzee atakuwa mchawi" nakiri kuwa usemi huu si wangu, ila niliusoma humu JF [some three days back] kutokana na comment ya mkuu mmoja, ambaye kwa bahati mbaya jina sikulishika. Nadhani kuna ukweli kuhusu usemi huu. Vijana ni watu wanaopenda mabadiliko chanya. Vijana wanapenda maendeleo yanayoonekana siyo AHADI. Vijana ni wadadisi na wachambuzi. Vijana ni watu ambao kila wakati wanajiuliza ''KWA NINI'' Vijana ni watu wanaoangalia mbali [sasa kuna utandawazi] wana TAMAA na UJASIRI wa kujaribu na siyo KUKATA TAMAA. Vijana wana nguvu ya kuleta MABADILIKO/MAGEUZI kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Vijana ni wapambanaji kwa ajili ya maendeleo. Vijana wanakerwa na mawazo mgando [business as usual] Vijana ni waonyesha njia. Vijana ni VIONGOZI. Vijana ni watu wasiopenda KUTISHWA na kukatishwa TAMAA, kwa nini, kwa sababu VIJANA wanapenda kuthubutu na kujaribu. Sasa inakuwaje kijana wa Tanzania leo anashabikia CCM? Kukatishwa tamaa huku, kutishwa kote huku, kukemewa huku, kukimbizwa mabarabarani huku, kupigwa huku kote na kudumazwa kiuchumi huku kote, leo bado kuna KIJANA wa Tanzania anashabikia CCM? Kweli !!! Mimi sasa ni mtu mzima maana nilikuwa JKT Operation MWAKA MMOJA muda sasa siyo haba. Nawauliza nyie vijana..Achana na akina Nape, Ridhiwan nk ambao ni CCM maslahi. Kweli yupo kijana wa Kitanzania leo anaipenda CCM? Kama bado wapo vijana wa Tanzania wanaipenda CCM [kweli kweli] basi hao wakiwa wazee lazima watakuwa WACHAWI wakubwa.
 
Back
Top Bottom