Vijana wa Tanzania

Sam mirror

JF-Expert Member
Sep 29, 2018
1,462
2,219
Habari ndugu,
Ninaandika haya nikiwa na simanzi kubwa moyoni. Ni wapi sisi vijana wa Taifa hili tutashikilia.

1. Suala la mkopo heslb ni janga zito na unyonyaji wa wazi. Mimi mtoto wa maskini mzazi wangu mkaanga miongo nimejitahidi kusoma mpaka kufika chuo kwa tabu na dhiki kuu, nimefanikiwa kupata mkopo ambao unasaidia familia yangu na mimi kiujumla, kuna sela ya kujiajili hiyo pesa ndogo ndo ilibidi nitumie kama mtaji mana hata nikimaliza leo hakuna kwa kwenda bado serikali yangu pendwa hiyo pesa inaikata, lakini kuna wafanyakazi walilipwa ujira wao wakati wako nyumbani

Kama wanakata iyo pesa wanipunguzie na ada mana sisomi mda wote, nitaambiwa wewe mpumbavu kaa kimya hujui sheria yoyote.

Ada ya chuo silipiwi yote, nategemea boom niongezee hiyo ada, nile nilipe kodi na matumizi mengine pmj na kusaidia nyumbani pesa laki na themanini Saba. Eti kwakua maskini hana kauli tunasema Asante.

2. Ajira kwa vijana
Imekuwa kama historia vijana wanaishi kama wakimbizi, nchi yao Ila utafikiri wapo ugenini Sio madaktari, engineering,walimu n.k
Kuna umuhimu gani wakusoma

Saizi watu mtaani wakimuona msomi wanamuona kama chizi asiye na lolote lile, unaambiwa kaa kimya tununue mandege si unaona nchi yetu ipo uchumi wa kati.

Mabadiko hakuna mtu atakaye yaleta, umoja, ushirikiano, uzalendo utaleta mabadiliko.

Ni muda kama vijana kuacha uoga simamia haki Zako pigana kwa ajili yako na kizazi chako, ata isipokuwa Leo mda unakuja ambao hakuna mtu atakaye kuwa tayari kuendelea kupata maumivu kama haya,

Haiwezekani watu wawili au watatu waalibu maisha ya watu milioni 45 kisa wameshika dola ambayo ni kaka na dada zetu.

Amani ni kitu cha muhimu ila unyonyaji na haki lazima vifuatwe.

Vijana wa Tanzania mda unakalibia, ni bola ufe kuliko kunyanyaswa ndani ya nchi yako.

Siku njema.
 
Ni kweli man umeongea ...na cha kujiuliza je mkataba wa mkopo unasemaje?
Pili na maana ni maamuzi ya kukurupuka au ni nini.
Ya nini sasa. Kujisifia uchumi unakuwa halafu huku tunakatwa fedha kizembe tu yaani.
 
Wakati mwingine ukiona wasomi wanaikimbia nchi yao kwenda kutafuta exposure abroad wanaepuka Mambo mengi sana.
 
Ni kweli man umeongea ...na cha kujiuliza je mkataba wa mkopo unasemaje?
Pili na maana ni maamuzi ya kukurupuka au ni nini.
Ya nini sasa. Kujisifia uchumi unakuwa halafu huku tunakatwa fedha kizembe tu yaani.
Ni hatari
 
Back
Top Bottom