Vijana wa tanzania wamelala fofofo

lembeni

Member
Sep 8, 2010
31
1
Wakati vijana ulimwenguni wakiwa ni chachu ya mabadiliko ya Kisiasa,kiuchumi na kijamii hali imekuwa tofauti kabisa kwa vijana wa kitanzania ambao bado hawajaonesha uwezo wakuwa chachu ya mabadiliko hayo Vijana wa tanzania bado wamelala ni nini tatizo? Amkeni
 
wakati vijana ulimwenguni wakiwa ni chachu ya mabadiliko ya kisiasa,kiuchumi na kijamii hali imekuwa tofauti kabisa kwa vijana wa kitanzania ambao bado hawajaonesha uwezo wakuwa chachu ya mabadiliko hayo vijana wa tanzania bado wamelala ni nini tatizo? Amkeni


hawapewi nafasi, ukionyesha uwezo kdogo tu unatafutiwa uraia nje. Wazee hawataki kuwaachia vijana nafasi...... Vijana wanao pewa nafasi ni wale wenye fikra kama zao . Ambo wako tayari kuimba wimbo wa hao wazee.
 
Wakati vijana ulimwenguni wakiwa ni chachu ya mabadiliko ya Kisiasa,kiuchumi na kijamii hali imekuwa tofauti kabisa kwa vijana wa kitanzania ambao bado hawajaonesha uwezo wakuwa chachu ya mabadiliko hayo Vijana wa tanzania bado wamelala ni nini tatizo? Amkeni


jAMANI HAWAPEWI NAFASI, UKIONYESHA UWEZO KDOGO TU UNATAFUTIWA URAIA NJE. WAZEE HAWATAKI KUWAACHIA VIJANA NAFASI...... VIJANA WANAO PEWA NAFASI NI WALE WENYE FIKRA KAMA ZAO . AMBAO WAKO TAYARI KUIMBA WIMBO WA HAO WAZEE.
 
Beware of a man of one book

Hahahaha,

Hii nimeipenda mazee. Kuhusu mada kuu, usiulize vijana wa Tanzania wamefanya nini, jiulize wewe mwenyewe umefanya nini. Kama kila mtu atajiuliza mwenyewe wote tutasukumana kwenye maendeleo, tatizo letu tumekuwa wepesi kunyooshea vidole wengine wakati sisi wenyewe mara nyingi hatujafanya lolote.
 
www.vijana.fm

Vijana wa Tanzania tuamke!

Tuwekeni visingizio pembeni. Maisha yetu ya baadae hayana budi kujengwa sasa hivi. Nina uhakika vijana wengi hamtaisoma hii makala kwasababu tu ni "ndefu"!


Na Mkereketwa

Unategemea kuona jinsi utawandazi unavyoathiri matendo na mawazo ya watu, hasa vijana wa Tanzania, ili kuleta mabadiliko kwenye jamii. Lakini ninachokishuhudia kila siku kinanipa hofu na mashaka.

Nimeanza kufuatilia kwa karibu sana mambo yanayofuatiliwa na vijana takribani miezi nane iliyopita; aina ya mijadala tunayopenda kuchangia kwa kina na hoja zetu (kwenye tovuti mbalimbali). Kusema ule ukweli, inasikitisha sana na ninadiriki kusema: Vijana wa Tanzania hatuna dira na hatujui tunapokwenda. Na kwa mwendo huu, sitashangaa tusipokuwa na mabadiliko yoyote ya kifikra, matendo na jamii kwa ujumla kwenye miaka 15 – 20 ijayo!

vijana-butiama.jpg


Najiuliza, sisi kama vijana, takribani 70% ya idadi ya watu Tanzania, hivi tunajua tunachofanya? Mbona hatujui hata kuuliza viongozi wetu maswali ya msingi? Au jambo linalogusa Taifa linapotokea, mbona tunanywea na kujificha? Au muda mwingine, mbona tunakuwa kama majuha na kutetea upumbavu?

Walahi! Ningekuwa fisadi, sijui kama mikwara ninayoiona kwenye blogs na vijiwe vyetu ingenitisha! Kwasababu, najua fika kuwa baada ya siku mbili tatu, watu watasahau na maisha yatarudi kwenye hali ya kawaida - nitakuwa kaunta kwenye kiti changu kirefu huku nikipata moja baridi moja moto kwa mrija na kiti moto. Matawi ya juu.

Nitakupa mifano michache.

Miezi michache iliyopita, wasanii kadhaa wa Bongo Flava walijitosa kwenye vyama mbalimbali, iwe CCM, CHADEMA, TLP, CUF… Hiyo sio hoja. Kama tungekuwa angalau tunajua katiba au sheria vizuri, tusingewatukana; kwasababu wao kama wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wana haki ya kukipigia debe chama chochote kile cha siasa.

Kwa taarifa yako, Prof. Jay hakutuasi kwasababu tu aliimba "Ndio Mzee."

Lakini, kwasababu wao wamekubali kutumiwa kama nyenzo ya kuwahimiza vijana kufuatilia, kukichangia au kukipigia kura chama fulani, si wajibu wetu ungekuwa kuwauliza maswali kuhusu sera za vyama walivyochagua? Mi' namfagilia Nakaaya kwa sana tu (usiulize kwanini!), ila kamwe hautaniona namchagua mgombea fulani wa CHADEMA kwasababu tu Nakaaya yuko CHADEMA. Tungepaswa kuwabana ili watupe sera za CHADEMA au CCM! Je, wanazijua katiba za vyama husika? (Nilitembelea JF mara moja na kushangazwa na mmoja wa wachangiaji na mshabiki mkubwa wa CHADEMA aliyekuwa hajui hata kirefu cha neno "CHADEMA"! True story… Watu walimshambulia!)

Ni upumbavu – kwa maoni yangu – kushabikia chama fulani, eti kisa ulimuona Juma Nature kwenye bango! Fanya utafiti; sikiliza sera za wagombea, halafu amua yupi atakidhi mahitaji yako kama kijana. Hiyo ndio maana ya demokrasia.

Mfano wa pili: Kuna mijadala ambayo kila kijana anapaswa kuifuatilia na ikiwezekana kujaribu kujifunza vitu viwili vitatu. Hata kama hupendi kufuatilia mambo ya uchumi au siasa, chama fulani kikitangaza mgombea wa Urais, unapaswa kupandisha nyusi zako ili uone yanayoendelea.

Hata kama wewe hupendi wanyama au hujui mambo ya mbuga za wanyama, kelele kama hizi kutoka nchi za Magharibi zinapotua kwenye ngoma za masikio yako, unapaswa kuuliza maswali mpaka majibu yanayoeleweka yapatikane.

Nadhani unauliza kwanini; mimi sio vegeterian na napenda sana nyama ya nyati, mbogo, nyumbu na pundamilia! Halafu, wanyama wa Serengeti wanapenda sana kwenda Kenya kuzurura, eneweiz.

Fikiria tena. Serikali inasema itajenga Barabara ya Serengeti kama walivyopanga, lakini, "the feasibility studies are still under way." Mtu unatoa tamko rasmi la kujenga kitu fulani kabla ya kumaliza utafiti? Ok, kwa sasa hivi sahau mambo yanayosemwa na watu kutoka Unyamwezini. Angalia ripoti ya TANROADS kuhusu mpango wa kujenga ile barabara halafu amua mwenyewe. Usisahau kuilinganisha na ripoti ya Frankfurt Zoological Society.

Binafsi, nimetoka sasa hivi kuisoma (ya TANROADS) na ikanikumbusha lile sakata la uchafuzi wa mazingira Mara lililokufa kibudu. Unakumbuka wataalamu wetu wa Wizara ya Nishati na Madini walioenda Mto Tighithe na litmus papers tu? Karne hii?

Nina uhakika kuna vijana wengi wapiganaji wenye machungu na Tanzania. Lakini wanasita kutoka kwasababu kelele zao zitakuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Nani ajitoe mhanga, halafu ‘akishindwa' watu watasema tu, "Oh, alipigania haki za wasio na sauti." Nukta. Yaani huo ndio mwisho wa upiganaji? Kugombea haki? Mtu katolewa kafara, halafu watu wanaleta upuuzi wa kujibu tu kwa sentensi moja. Kisha wanazima tarakilishi na kwenda kulala?

Mfano wa tatu: Tembelea ukurasa (facebook) wa Chama cha Vijana Tanzania? Nini kinatokea pale? Mbona porojo tu zisizokuwa na mbele hata nyuma? Kuna mzee (wa maana anayeheshimika Tanzania) alijitolea kutoa mwongozo na kuuliza maswali ya msingi. Unadhani kuna jibu la maana tuliloliona? Mzee akala kona. Sijamuona tena akichangia!

Halafu linganisha na ukurasa huu ambao unaendesha mijadala inayohusu Afrika – siasa, uchumi, utamaduni na maisha ya Waafrika kwenye kona mbalimbali duniani. Unajua wachangiaji wazuri wanatoka wapi? K-E-N-Y-A! Tunawaita Watani wa Jadi.

Wewe kama kijana, unajua hili Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki linamaanisha nini? Utaathirika vipi? Je, ulishafikiria labda kuna njia ambazo unaweza ukazitumia ili ufaidike? Tuling'ang'ania tu, "Watakuja kuchukua kazi na ardhi yetu!" Mi' mwenzenu nimeshaanza kupiga msasa ngeli yangu. Baada ya mwezi natia timu Nairobi.

Wakati wewe unafikiria kujibu haya, wenzako walishaanza kutuma CVs kwenye makampuni yanayopanga kuwekeza Afrika Mashariki…

EAC-Common-Market.jpg

Nitaishia hapa kwa leo. Nitaanika mambo mengine yanayonikereketa wiki ijayo. Kabla sijakuacha ili urudie kuisoma hii makala, napenda kusema nina ghadhabu kwasababu nina uhakika baadhi yenu – nyinyi vijana – ndio mtakaoshika usukani wa Serikali baada ya miaka kadhaa. Na sasa hivi kuna dalili inayoashiria kuwa tunayoshuhudia sasa hivi yataendelea kujirudia kutokana na uvivu wenu wa kusoma na kujifunza.

Kwa maneno mengine, zile kesi za Richmond, EPA, BoT, Uharibifu wa Mazingira Mara na Ujio wa Brazil zitajirudia. Majina tu ya wahusika ndio yatabadilika!

Kwaheri!

source: www.vijana.fm
 
Kila kizazi cha mtanzania kina mashaka. A generation embodying apathy at its best.
 
Tatizo ni kubwa sana hata humu ndan ya jf tukiuliza maswal majibu yanakatisha tamaa kweli hamtujibu vizur hamtuelimishi mjilaumu wenyewe kwa kushindwa kutufundisha
 
Back
Top Bottom