Vijana wa Tanzania tuamke! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa Tanzania tuamke!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 23, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280


  Tuwekeni visingizio pembeni. Maisha yetu ya baadae hayana budi kujengwa sasa hivi. Nina uhakika vijana wengi hamtaisoma hii makala kwasababu tu ni “ndefu”!  Na Mkereketwa
  Unategemea kuona jinsi utawandazi unavyoathiri matendo na mawazo ya watu, hasa vijana wa Tanzania, ili kuleta mabadiliko kwenye jamii. Lakini ninachokishuhudia kila siku kinanipa hofu na mashaka.
  [​IMG]
  Nimeanza kufuatilia kwa karibu sana mambo yanayofuatiliwa na vijana takribani miezi nane iliyopita; aina ya mijadala tunayopenda kuchangia kwa kina na hoja zetu (kwenye tovuti mbalimbali). Kusema ule ukweli, inasikitisha sana na ninadiriki kusema: Vijana wa Tanzania hatuna dira na hatujui tunapokwenda. Na kwa mwendo huu, sitashangaa tusipokuwa na mabadiliko yoyote ya kifikra, matendo na jamii kwa ujumla kwenye miaka 15 – 20 ijayo!
  [​IMG]Najiuliza, sisi kama vijana, takribani 70% ya idadi ya watu Tanzania, hivi tunajua tunachofanya? Mbona hatujui hata kuuliza viongozi wetu maswali ya msingi? Au jambo linalogusa Taifa linapotokea, mbona tunanywea na kujificha? Au muda mwingine, mbona tunakuwa kama majuha na kutetea upumbavu?
  Walahi! Ningekuwa fisadi, sijui kama mikwara ninayoiona kwenye blogs na vijiwe vyetu ingenitisha! Kwasababu, najua fika kuwa baada ya siku mbili tatu, watu watasahau na maisha yatarudi kwenye hali ya kawaida — nitakuwa kaunta kwenye kiti changu kirefu huku nikipata moja baridi moja moto kwa mrija na kiti moto. Matawi ya juu.
  Nitakupa mifano michache.
  Miezi michache iliyopita, wasanii kadhaa wa Bongo Flava walijitosa kwenye vyama mbalimbali, iwe CCM, CHADEMA, TLP, CUF… Hiyo sio hoja. Kama tungekuwa angalau tunajua katiba au sheria vizuri, tusingewatukana; kwasababu wao kama wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wana haki ya kukipigia debe chama chochote kile cha siasa.
  Kwa taarifa yako, Prof. Jay hakutuasi kwasababu tu aliimba “Ndio Mzee.”
  [​IMG]
  Lakini, kwasababu wao wamekubali kutumiwa kama nyenzo ya kuwahimiza vijana kufuatilia, kukichangia au kukipigia kura chama fulani, si wajibu wetu ungekuwa kuwauliza maswali kuhusu sera za vyama walivyochagua? Mi’ namfagilia Nakaaya kwa sana tu (usiulize kwanini!), ila kamwe hautaniona namchagua mgombea fulani wa CHADEMA kwasababu tu Nakaaya yuko CHADEMA. Tungepaswa kuwabana ili watupe sera za CHADEMA au CCM! Je, wanazijua katiba za vyama husika? (Nilitembelea JF mara moja na kushangazwa na mmoja wa wachangiaji na mshabiki mkubwa wa CHADEMA aliyekuwa hajui hata kirefu cha neno “CHADEMA”! True story… Watu walimshambulia!)
  Ni upumbavu – kwa maoni yangu – kushabikia chama fulani, eti kisa ulimuona Juma Nature kwenye bango! Fanya utafiti; sikiliza sera za wagombea, halafu amua yupi atakidhi mahitaji yako kama kijana. Hiyo ndio maana ya demokrasia.
  Mfano wa pili: Kuna mijadala ambayo kila kijana anapaswa kuifuatilia na ikiwezekana kujaribu kujifunza vitu viwili vitatu. Hata kama hupendi kufuatilia mambo ya uchumi au siasa, chama fulani kikitangaza mgombea wa Urais, unapaswa kupandisha nyusi zako ili uone yanayoendelea.
  [​IMG]
  Hata kama wewe hupendi wanyama au hujui mambo ya mbuga za wanyama, kelele kama hizi kutoka nchi za Magharibi zinapotua kwenye ngoma za masikio yako, unapaswa kuuliza maswali mpaka majibu yanayoeleweka yapatikane.
  Nadhani unauliza kwanini; mimi sio vegeterian na napenda sana nyama ya nyati, mbogo, nyumbu na pundamilia! Halafu, wanyama wa Serengeti wanapenda sana kwenda Kenya kuzurura, eneweiz.
  [​IMG]
  Fikiria tena. Serikali inasema itajenga Barabara ya Serengeti kama walivyopanga, lakini, “the feasibility studies are still under way.” Mtu unatoa tamko rasmi la kujenga kitu fulani kabla ya kumaliza utafiti? Ok, kwa sasa hivi sahau mambo yanayosemwa na watu kutoka Unyamwezini. Angalia ripoti ya TANROADS kuhusu mpango wa kujenga ile barabara halafu amua mwenyewe. Usisahau kuilinganisha na ripoti ya Frankfurt Zoological Society.
  Binafsi, nimetoka sasa hivi kuisoma (ya TANROADS) na ikanikumbusha lile sakata la uchafuzi wa mazingira Mara lililokufa kibudu. Unakumbuka wataalamu wetu wa Wizara ya Nishati na Madini walioenda Mto Tighithe na litmus papers tu? Karne hii?
  Nina uhakika kuna vijana wengi wapiganaji wenye machungu na Tanzania. Lakini wanasita kutoka kwasababu kelele zao zitakuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Nani ajitoe mhanga, halafu ‘akishindwa’ watu watasema tu, “Oh, alipigania haki za wasio na sauti.” Nukta. Yaani huo ndio mwisho wa upiganaji? Kugombea haki? Mtu katolewa kafara, halafu watu wanaleta upuuzi wa kujibu tu kwa sentensi moja. Kisha wanazima tarakilishi na kwenda kulala?
  Mfano wa tatu: Tembelea ukurasa (facebook) wa Chama cha Vijana Tanzania? Nini kinatokea pale? Mbona porojo tu zisizokuwa na mbele hata nyuma? Kuna mzee (wa maana anayeheshimika Tanzania) alijitolea kutoa mwongozo na kuuliza maswali ya msingi. Unadhani kuna jibu la maana tuliloliona? Mzee akala kona. Sijamuona tena akichangia!
  Halafu linganisha na ukurasa huu ambao unaendesha mijadala inayohusu Afrika – siasa, uchumi, utamaduni na maisha ya Waafrika kwenye kona mbalimbali duniani. Unajua wachangiaji wazuri wanatoka wapi? K-E-N-Y-A! Tunawaita Watani wa Jadi.
  Wewe kama kijana, unajua hili Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki linamaanisha nini? Utaathirika vipi? Je, ulishafikiria labda kuna njia ambazo unaweza ukazitumia ili ufaidike? Tuling’ang’ania tu, “Watakuja kuchukua kazi na ardhi yetu!” Mi’ mwenzenu nimeshaanza kupiga msasa ngeli yangu. Baada ya mwezi natia timu Nairobi.
  Wakati wewe unafikiria kujibu haya, wenzako walishaanza kutuma CVs kwenye makampuni yanayopanga kuwekeza Afrika Mashariki…
  [​IMG]
  Nitaishia hapa kwa leo. Nitaanika mambo mengine yanayonikereketa wiki ijayo. Kabla sijakuacha ili urudie kuisoma hii makala, napenda kusema nina ghadhabu kwasababu nina uhakika baadhi yenu – nyinyi vijana – ndio mtakaoshika usukani wa Serikali baada ya miaka kadhaa. Na sasa hivi kuna dalili inayoashiria kuwa tunayoshuhudia sasa hivi yataendelea kujirudia kutokana na uvivu wenu wa kusoma na kujifunza.
  Kwa maneno mengine, zile kesi za Richmond, EPA, BoT, Uharibifu wa Mazingira Mara na Ujio wa Brazil zitajirudia. Majina tu ya wahusika ndio yatabadilika!
  Kwaheri!
  Chanzo Vijana wa Tanzania tuamke!
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135


  Mkuu kumbe this is how you describe urself, poleeee!!!!!
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Pole na wewe usiekuwa na Dira yoyote ya maisha yako ya baadae. unataka niseme uongo ndio uniunge mkono?
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Laiti ungelijua unachokizungumza ungeendeea kujipa pole na pole!!!!!!!!!! Otherwise sina muda wa kuargue with a f..l. Gd luck!!!!!!!!!!
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  inaonyesha Mkuu Nyambala maneno yangu nimekuchoma ndio maana unakuja juu namna hiyooo? wewe ni CCM nini?
   
 6. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,503
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Vijana tuko macho siyo kawaida, wasukuma huwa wana msemo fulani unasema "mbuli alolile", maana yake ni kwamba "Mjinga katazama/anatazama". Msemo unajaribu kutoa scenerio ambapo mtu yuko mahali akidhaniwa kuwa ni mjinga sana kumbe siyo (na ndiyo mwenye akili sana kuzidi hao wanaomdhani hivyo) halafu anafanya observation ya kila kitu kinachoendelea. Tatizo tu ni kwamba anakuwa hana uwezo wa kuzuia kibaya kisichompendeza! NATURE WILL DECIDE ANYWAY. Makala yako imenigusa lakini siwezi kuyw mnafiki kusema eti naweza kuchukua hatua kuhusu hili, siyo mwoga ila nawajua watu wangu, naijua Nchi yangu, naiachia nature!
   
 7. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,503
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Mzizimkavu, halafu ile avatar yako ya mwanamme mkakamavu kuzidi wapiga mieleka umeipeleka wapi? Nilikuwa naipenda sana pamojana ya Rutunga, ile ya binadamu ana mdomo wa ndege! Hizo zinachekesha sana, za akina FirstLady1, preta, roselyn, etc zenyewe zina....., nisje nikapata kesi hapa wake za watu hao!
   
 8. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watu wanaiteka hii mada.

  Mzizi, ninachoweza kusema ni kwamba kwa kweli thread yako inasema ukweli kabisa. Comprehensive.
  Inabidi wachangiaji hapa waelewe kuwa hii si 'personal attack', ni maelezo ya ukweli wa vijana wa kiTanzania kwa ujumla wao, si mmoja mmoja.

  Hata hapa JF huu mtindo wa kutokupenda kujadili mambo yanayohusiana na mustakabali wa nchi ni dhahiri pale unapoamua kutumia kitufe cha 'New Posts', utakuta post zote mpya ni za mambo yasiyohitaji kuumiza kichwa.
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Inabidi kwanza ujue kwanini trend ipo hivyo, ukijua undani wake ndio unaweza kutoa maamuzi sahihi na pengine kushauri nini kifanywe. Kulaumu tu na kusema watu hawasomi au hawajali haisaidii sana.
   
 10. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama kuna mtu amelaumu, ni maoni
   
Loading...