Vijana wa tanzania na hatima ya siasa za vyama vingi

Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,315
7,113
Ndugu wana JF wenzangu, nimekuwa nikitafakari kwa muda mrefu sana hili swala la uungwaji mkono na vijana kwenye mikutano ya vyama vya upinzani na kufikiri kwamba muda si mrefu chama hiki dhalimu kitatoka madarakani muda si mrefu. Lakini pindi muda wa upigaji kura unapowadia matokeo yamekuwa yakija kinyume na matarajio ya wengi (nami nikiwa mmoja wao). Tumeshuhudia muda mrefu sana kumekuwapo na misururu mirefu sana kwenye mikutano ya vyama vya upinzani yenye kutoa taswira chanya kwa maendeleo ya demokrasia nchini, lakini kumbe asilimia kubwa ya vijana ni washibiki tu kama si wafurukutwa wa vyama hivyo.

Sasa tujiulize ni halali kwa vyama hivi kuendelea kuwaamini vijana wa Tanzania katika harakati za kuchukua dola? Au kuna njia mbadala tunayotakiwa kuitumia? Tumeona jinsi chama cha magamba kilivyowekeza kwa akina mama na wazee (ingawa siyo wote) na kinavyofanikiwa kupata ushindi kwa urahisi. Je! Au uhamasishaji wa vyama vya upinzani una kasoro?

Nafikiri tufike mahali hivi vyama vya upinzani vitoe elimu ya kujitoa muhanga kwa vijana - kama kweli wanataka kuendelea kuaminiwa - kukabili gharama zozote zinazohusiana na uchaguzi (hapa simaanishi gharama ya pesa ghafi. Hapa nazungumzia gharama ya muda). Chama cha magamba kimekuwa na kasumba ya kuhamisha majina ya wapiga kura vijana kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine cha mbali ili kuwakatisha tamaa vijana (kama kweli wanajitokeza kupiga kura). Hivyo katika hili vijana wanapaswa kujua kwamba kukitoa madarakani chama cha magamba siyo ngoma ya kitoto, inahitaji kujitoa muhanga. Kwani ukipoteza siku moja (tena bahati nzuri siku yenyewe mara nyingi huwa ni mapumziko) utapoteza kiasi gani cha kuzidi kura yako?

Kama kweli uchaguzi huu wa Igunga vyama vya upinzani vitapoteza vijana ndo wanapaswa kubeba lawama zote! Itakuwa haina maana kuendelea kuwaponda wazee kwamba wametopea kwenye mawazo ya chama kimoja wakati vijana wenyewe hamjajipanga kukiondoa madarakani hiki chama cha magamba! Inakuwaje wapiga kura zaidi ya 170,000 wajitokeze watu wasiozidi 100,000? Vijana mna safari ndefu ya kuwapiku wazee, vinginevyo mtaendelea kulalamika tuuu!

Kwa upande wangu napata taabu sana kuwaamini tena vijana wa Tanzania katika hizi siasa! Jana nilimsikia kijana mmoja anahojiwa kwa vile amekuta jina lake limehamishwa kutoka kwenye kituo alichojiandikishia sasa atachukua hatua gani? Jibu lake lilikuwa rahisi tu eti "Sasa nitafanyaje wakati nimeambiwa sitapiga kura". Huyu wala hana wazo la kwamba ngoja nikaangalie kwenye kile kituo walichonielekeza - KAAAZI KWELI KWELI!!!.
 
Back
Top Bottom