Vijana wa Mzizima wanateketea. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa Mzizima wanateketea.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by twahil, Aug 23, 2011.

 1. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  Ndg. Zangu nimeamua kuandika hapa ili tuone tutawasaidia vipi vijana wa K'KOO MTAA WA MZIZIMA-BONDENI.Juzi nilishangaa kuwaona baadhi ya wabunge wakilia kutokana na athari za madawa ya kulevya hapa nchini.Hakika nimejionea live bila chenga kwa kuona vijana wakitumia madawa hayo na bangi kwao ni sawa na kuvuta sigara.Kilichonisikitisha zaidi ni utumiaji wa bangi na dawa za kulevya hadharani na kila kona masaa yote utakuta vikundi mbali2 vya vijana wanavuta bangi,kibaya zaidi kuna shule iko karibu na kiwanda cha bia ina ukuta mrefu utakuta vijana wanafunzi wamejumuika na vijana wa mtaa huo vijiweni wakivuta bangi.MWEMA U WAPI,KOVA U WAPI,USALAMA WA TAIFA MU WAPI.NJOONI HUKU TUOKOE KIZAZI CHA NCHI HII.Vijana wamekuwa matahira ghafla huku.Au haka kakipande si tanzania?.kama huamini rafiki njoo upitepite huku utalia.Kabonde kote kananuka bangi huku vijana wakiwa matahira ghafla.
   
 2. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  Inaumiza sana af wauzaji wakuu ni watu walovaa kofia muhim serekalini,umaskini hauwez pungua coz vijana ambo ndio taifa la leo hawako timam kuijenga nji yao,funny enought wahusika wapo na wanajulikana!
   
 3. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Wacha wafu wazike wafu wao....unataka mwema aje kufanya nini? Wazazi wao wako wapi?
   
 4. JS

  JS JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndo yale aliyokuwa anasema Gerald Hando kwenye Powerbreakfast asubuhi ya leo. Kuhusu hayo madawa ya kulevya/mihadarati na kwamba wanajulikana wanaoyaleta hapa nchini lakini hakuna kinachofanyika. Tumwachie Mungu!!!

  Kama wanajulikana wanaofanya biashara hiyo kwa nini wasichukuliwe hatua? Rais amekalia hayo majina sijui ili iweje yazae majina mengine au ni uoga usiokuwa na kichwa wala miguu...eti unajidai kabisa in public unayafahamu yako kwenye meza yako kwa nini usiwataje tukawafahamu?au uswahiba umezidi kushinda ufanisi wa kazi??

  Labda wangekuwa watoto wa vigogo ndo wanabwia hivo kama hao wa kkoo kungefanyika kitu. Mungu awanusuru tu jamani.
   
 5. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  kazi na sera mbovu za ssm ndo chanzo,
  majina ya wanaoingiza wanayo wameyakalia
  mfumo wa elimu mbovu vijana wanakimbia
  ajira hakuna,hela hakuna unategemea nini
  wakati watoto wa hao vigogo wasoma nje!!!

  think twice na ssm yako
   
Loading...