tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe Taifa, Ndg. Geofrey Kiliba ameendelea na ziara yake mkoani Singida ambapo alikutana na vijana maafisa usafirishaji katika wilaya ya Manyoni.
Soma pia: Kampeni ya mama asemewe kuandaa kongamano kubwa la wanavyuo Dodoma kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025
Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa mikakati ya kampeni inayolenga kuhamasisha ushiriki wa jamii katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 pamoja na kulinda amani na utulivu wa Taifa la Tanzania
Katika mazungumzo yake na vijana hao, Ndg. Kiliba aliwasisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi, hususan katika kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025, akibainisha kuwa vijana ndiyo nguvu kuu ya taifa na wana nafasi ya kipekee katika kuleta mabadiliko chanya kwa mustakabali wa Tanzania.
Aidha, alihimiza vijana kuendelea kudumisha mshikamano, umoja na amani, akisisitiza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa za maendeleo chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, na ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda mafanikio hayo.
Ziara hii imeendelea kutoa hamasa kubwa kwa wananchi wa Singida, ambapo kampeni ya Mama Asemewe inatarajia kuendelea na mikutano na vikao vya uhamasishaji katika mikoa mingine kuelekea uchaguzi mkuu.