Vijana wa Lumumba na ZZK twitter

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Amani iwe kwenu!
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia maandiko ya mheshimiwa zzk huko twitter na jinsi watu wanavyopokea maoni yake. Katika fuatilia kwangu posts zake na mapokeo ya watu nimegundua yafuatayo.
1. Kuna kikundi cha vijana ambao bila shaka limeundwa kwa makusudi kumshambulia zzk kwa chochote anachokiandika bila kutafakari yaliyoandikwa. Hawa vijana kwa mtazamo wangu wamepangwa au wamejipanga kufanya kazi hii kwa nguvu kubwa sana.
2. Bado elimu ni tatizo kubwa nchini, kwa nchi nyingi watu wanaotumia mitandao ya kijamii ni watu wasomi na wenye uelewa mkubwa. Lakini kwa Tanzania mambo ni tofauti sana, kwa tanzania watu wanaotumia mitandao ya kijamii ni miongoni mwa watu wajinga na wasio na uelewa mkubwa wa mambo, ni watu wasioweza kutumia akili zao kutafakari bali huendeshwa kwa misimamo ya viongozi wao wa dini na viongozi wa vyama vyao vya siasa. Ni vijana ambao kiongozi wao wa chama akisema 1+1=2 wanasema amepatia lakini kiongozi wa upande wa pili akisema 1+1=2 wanasema kakosea na wanamkebehi kwa nguvu zote. Maoni ya vijana hasa wa CCM dhidi ya ZZK yananifanya nisikitikie elimu ya vijana wa taifa hili.
3. Nimegundua viongozi wa kisiasa wameshajua kwamba raia hasa vijana ni majuha , hawana uwezo wa kutafakari wala kuchambua kauli za viongozi. Wamejua kwamba sisi tunashabikia vyama hata kama vyama vyenyewe vinakosea.

Mimi naomba vijana hasa wa CCM na CHADEMA tuwe na akili zetu, viongozi wetu wakiwa sahihi tuwapongeze na wakikosea tuwakosoe. Tuache hizi hulka za kijinga za kushabikia kila ujinga na kuona wenye mawazo tofauti na za vyama vyetu kama maadui. Elimu itusaidie kufanya uchambuzi wa kina na kufanya maamuzi ya busara. Wale vijana wanaomtukana na kumkebehi ndg zzk huko twitter hebu angalieni contents ya anachokiandika na si chama au utofauti wenu wa kivyama.
 
Uchambuzi wako umekaa vizuri. Kama ulivyosema, ni kweli kwamba ujuha wa wananchi na hasa vijana ndio mtaji mkuu wa wanasiasa. Ukiitazama hii nchi kwa jicho la tatu utaona ni kama bado iko katika zama za giza (Dark Ages) ambapo juhudi kubwa inatumika katika kukumbatia ujinga. Elimu imevurugwa kiasi kwamba wahitimu wa shule/vyuo wamegeuzwa mazezeta wa kuwaimbia wanasiasa mapambio ya sifa na utukufu!
 
Back
Top Bottom