Vijana wa familia maskini tuungane kupambana na hawa wakoloni weusi wa CCM

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
2,420
4,922
Wakuu.

Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu napenda kuwakumbusha vijana wa nchi hii, hasa wale wanaotoka familia masikini mijini na vijijini kuwa imewapasa kuelewa kuwa nchi hii inapelekeshwa na hawa wakoloni weusi wa CCM kwa sababu wao wana advantage moja ya kuwa na urahisi wa kuitafuna keki ya taifa.

Bahati mbaya sana sisi tuliozaliwa katika familia duni ambao kimsingi chanzo cha umaskini wa wazee wetu ni mifumo mibovu iliyoasisiwa na kuendelezwa na hawahawa ma-ccm kwa ajili ya kuhakikisha wanadumu katika utawala wa mabavu wakiteka akili za wazazi wetu kwa vizawadi vidogovidogo kama tisheti na kanga ha ahadi hewa kama milioni 50 kila kijiji.

Nawashauri tusikubali. Kwanza niwapongeze kwa kuendelea kuamka. muamko wa uchaguzi mwaka 2000, na 2015 tuuendeleze na sasa tukaze zaidi mpaka hawa wakoloni weusi watie akili. Hakuna cha Magufuli, hakuna cha nani hawa wakoloni wa CCM hawana jema na nchi hasa sisi watoto wa masikini.

Tuwakatae, tukatae hadaa zao. kama tutakubaliana kupiga kura tukawakatae kwenye sanduku la kura japo wataiba lakini ujumbe wataupata wakati wa kuhesabu hizo kura. Kama tutakubaliana hatuendi kupiga kura kishindo kiwafikie kwa kupata idadi ndogo ya waliojitokeza.

Nawakumbusha pia kuwa chama pekee mbadala cha kuondoa utawala wa hovyo wa CCM ni CHADEMA. Tushikamane na kusimama kwa ajili ya chama chetu. Vyama vingine ndo kama hivyo mnaona wenyewe wenzetu wana bei wameitwa Ikulu wanaunga juhudi wamevuta fungu akili zao wameziacha magogoni sasa wanafanya vituko.
 
Zamani watoto wa maskini walikua wanaambiwa someni mje mpate ajira ila siku hizi serikali inawaambia someni ili mje mjiajiri huku watoto wa wakubwa wakipewa ajira vitengo vinono.

Ndio maisha ya wanyonge hayo.
 
Mimi sitoenda kupiga kura kwa mara ya kwanza mwaka huu,kwasababu mojawapo kati mbili
1:Najua nitakayempigia kura hata nisipompigia atapita tu.
2:Najua nitakayempigia kura hata akishinda kwa kishindo hatapita.
 
Kuzaliwa masikini sio kosa, ila kufa ukiwa fukara ndio tatizo.

Hakukua na haja ya kuingiza siasa ikiwa lengo ni kujikwamua kiuchumi. Imepunguza au kuharibu uzito wa hoja.
 
Hadi aya na baada ya kituo unaanza na herufi ndogo!!!
===========
Serikali imekufanya vipi uwe masikini?
 
Back
Top Bottom