mawazobinafsi
Member
- Aug 15, 2014
- 44
- 14
UTANGULIZI
Watu tunaotaka kuwaunga mkono katika mageuzi tunaanza kuwaogopa. Inasikitisha wachumia tumbo kuwa vinara wa siasa.
MADA
Ni ukweli usiopingika kwamba, siasa kwetu ni kuhubiri chuki na propaganda za uongo baada ya kuangalia ni jinsi gani tutashindanisha sera na utekelezaji wake ulivyo ili kumkomboa mtanzania. Ni tofauti kwa nchi tulizowaiga, siasa kwako ni demokrasia hasa na honest kwa kila mtu. watu wanashindanisha sera na utekelezaji. Lazima tukili kwamba umasikini huu inaoongezeka unatokana na siasa zetu.
Siasa zimeongeza matumizi yetu kwenda kwenye utekelezaji wa vitu visiofaa badala ya maendeleo (majority welfare). Inasikitisha kuona fedha nyingi zimeelekweza kwenye KAMPENI kugharamia vitu visivyo na msingi kama (kununua kanga na tisheti kama takrima, matumizi ya chopa n.k)
Ni ukweli usipingika vijana wengi humu JF ni bora mkalime badala ya kufanya siasa kwani mmekuwa na mawazo tendegu kwa kufikili siasa ni CHUKI na kusambaza PROPAGANDA ZA UONGO. Inakera kuona maeno kama, UDINI, UKABILA, USALITI, na LUGHA ZA LAANA zikitumika.
Inasikitisha kuona vijana wa BAVICHA, ACT na UVCCM mnatumika na kushabikia upuuzi baada ya kujadili changamoto za uchumisiasa. Siasa kama zenu ndio zimeleta machafuko mbalimbali barani Africa.
TUJADILI
Hatma ya siasa zetu katika kutatua changamoto mbalimbali za demokrasia na uchumi. Kwa siasa hizi tutafika tunapopataka au tutachukiana tu?
Critical thinkers tujadili tuokoe Tanzania yetu