Vijana tusitumike kueneza udini

Status
Not open for further replies.
Alex Manonga

Alex Manonga

Verified Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
155
Likes
4
Points
35
Alex Manonga

Alex Manonga

Verified Member
Joined Oct 8, 2010
155 4 35
Na Alex Manonga

VIJANA katika taifa lolote ni nguzo muhimu katika siku zijazo, na wana jukumu la kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kizazi cha sasa kwa ajili ya kizazi kijacho.

Jukumu hilo ni la urithi na lazima, si hiari ya vijana wenyewe; ni sharti la kimaumbile.

Umuhimu wa vijana kwa taifa ni umuhimu wa kijamiii unaotokana na sababu za kimaumbile. Ni watu wenye ndoto nyingi, ari na nguvu mpya inayohitajika kwa mabadiliko.

Baadhi ya viongozi vijana wakiwemo January Makamba na Zitto Kabwe wamekuwa wakitetea ushirikishwaji zaidi wa vijana katika ngazi mbalimbali za uongozi na uamuzi.

Vijana wasiposhirikishwa katika uamuzi juu ya kesho watakayoishi, watakuja kupambana na matokeo ya uamuzi mbovu wa waamuzi wa leo ambao hawatakuwepo wala kuathiriwa na matokeo ya uamuzi wao.

Ni muhimu ikaeleweka kuwa kusema vijana ni nguzo, hakulengi kupuuza hata kidogo umuhimu wa wazee wala mchango wao katika maendeleo na ujenzi wa taifa lenye dira.

Vijana ni nguzo na wazee ni ardhi inayoshikilia nguzo. Bila ardhi nguzo haitaweza kusimama, na hivyo umuhimu na kazi yake hautakuwa na tija yoyote kuifanya nyumba isimame achilia mbali uimara wake.

Huo ulikuwa ukweli wa jumla wa kidunia kuhusu vijana. Tanzania kama sehemu ya dunia, ndani ya jumuiya ya kimataifa hutegemea vijana wake katika kendeleza maslahi yake ya nje na ya ndani kwa siku zijazo.

Nimelazimika kusema haya kutokana na mambo ya ajabu yanayochochea migawanyiko katika taifa letu, yakielekea kuwa sehemu ya utamaduni wa siasa katika zama hizi za vyama vingi, vijana tukihusika kwa kiasi kikubwa.

Ingawa si nia yangu kukisema chama wala itikadi yoyote, lakini ni dhahiri kwamba mambo hayo yanayomomonyoa misingi uunganishi ya taifa yanatokana na siasa za ushindani zilizokosa sera shawishi ndani ya vyama vyetu.

Tunashuhudia ukuaji wa mtindo wa siasa za makundi ndani na nje ya vyama vinavyoshindana kupata ushawishi wa kisiasa nje na ndani ya vyama vyenyewe.

Bahati mbaya ushawishi wenyewe hauelekei kuzingatia sera wala masuala isipokuwa hujuma ya kundi moja dhidi ya jingine, chama dhidi ya kingine kwa njia ya kupachikana utambulisho mbaya.

Katika mtindo huu wa siasa, baadhi yetu vijana hutumiwa na wanasiasa wasio na nia njema kufikia malengo yao binafsi ya kisiasa.

Tunatumika bila kujua na au pengine kwa kujua, lakini tunavumilia kwa sababu ya maslahi binafsi. Mtindo huu na siasa za namna hii ni mzuri kwa ushindi pekee.

Lakini baada ya ushindi kupatikana changamoto kubwa ni anayeshinda kwani ni vigumu kutawala. Sababu ni kwamba makundi yasiyotokana na utofauti wa kisera au itikadi si rahisi kufa kwa sababu uishi wao hautegemei hoja.

Pia ushindi unaotokana na mbinu zisizozingatia taratibu zinazokubalika za ushindani hukosa uhalali wa kimaadili hata katika yenyewe.

Utambulisho mbaya unaotumika sasa hivi ni wa udini, ukabila na ukanda. Kundi moja hujaribu kutafuta uhalali wa kisiasa kwa kuonyesha udhaifu wa kundi au chama kingine wakati mwingine bila kujali madhara ya muda mrefu ya matokeo ya matumizi ya mbinu hizo chafu.

Ni jambo la kusikitisha kwamba wanaohubiri ukabila wa wengine, udini wa wengine na ukanda wa wengine; kana kwamba kundi lake, chama chake, kimeshuka kutoka kwenye sayari ya Mars, kwamba hakina kabila, hakina dini; ni vijana ambao ndio viongozi wa taifa letu kesho.

Kijana ambaye leo anashiriki kueneza chuki za kidini au kikanda kwa sababu za kisiasa, kesho atakuwa kiongozi wa namna gani na katika taifa lipi?

Huhitaji kuwasoma wanafalsafa wa Kiyunani au wanafasihi kama Chinua Achebe kuelewa kwamba wazo huzaliwa, hukua na kama lisipokufa huweza kumuathiri hata mtunzi wake.

Ukabila, udini na ukanda ni mawazo ambayo sasa yanazungumzwa kama vile ni sehemu ya utamaduni mpya wa kistaarabu katika siasa za Tanzania.

Mawazo haya hayatakufa tu pale tunaoshindana nao watakapotoweka. Washindani wanaweza kutoweka na mawazo haya yataendelea kuwepo na yatawarudia wale wale walioyazalisha.

Hatujiulizi mtoto wa darasa la saba leo anayekua akisikia chama fulani ni cha kabila fulani, chama fulani ni cha wanaotoka sehemu fulani ya nchi, chama fulani ni cha dini fulani anajifunza nini. Wanajifunza nini watoto hawa, kama si kukua wakiamini msingi wa siasa za Tanzania ni ukabila ukanda au udini?

Rai yangu kwa vijana wa Tanzania ni kukataa kutumiwa na wanasiasa kuwa chanzo cha migawanyiko kwa misingi ya ukabila, udini au ukanda.

Matokeo ya mbegu ya ukabila, udini na ukanda hayatatuacha salama kesho.

Nimelazimika kushauri kama kijana ambaye mafanikio yangu madogo yametokana na msaada wa Watanzania ambao baadhi yao sikuwahi hata kujua makabila yao achilia mbali imani zao za kiroho.

Vijana tuungane, tuitetee na kuilinda Tanzania iendelee kuwa moja

Source: Tanzania Daima 12/12/2013
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,907
Likes
2,479
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,907 2,479 280
Dah! Alex Manonga umepotea! Any way si kutumika kueneza udini tu bali tusikubali kutumika kwa jambo lolote. Kwani ni kwa nini sisi tuwe wa kutumika? Mimi naona siku hizi hata kwenye siasa sisi ni watu wa kutumika.Tumegeuka kuwa mavuvuzela ya watu badala ya kufikiri.Inasikitisha sana! Vijana tutaweza kutoa mchango wa maana katika nchi hii ikiwa tutaamua kuwa na fikra huru na za kipembuzi.
 
Last edited by a moderator:
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
527
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 527 280
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
 
Alex Manonga

Alex Manonga

Verified Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
155
Likes
4
Points
35
Alex Manonga

Alex Manonga

Verified Member
Joined Oct 8, 2010
155 4 35
Dah! Alex Manonga umepotea! Any way si kutumika kueneza udini tu bali tusikubali kutumika kwa jambo lolote. Kwani ni kwa nini sisi tuwe wa kutumika? Mimi naona siku hizi hata kwenye siasa sisi ni watu wa kutumika.Tumegeuka kuwa mavuvuzela ya watu badala ya kufikiri.Inasikitisha sana! Vijana tutaweza kutoa mchango wa maana katika nchi hii ikiwa tutaamua kuwa na fikra huru na za kipembuzi.
Nipo ndugu betlehem. Uko sahihi vijana tusitumike katika namna yoyote kwenye mambo ya kupasua Taifa. Kazi yetu kubwa kama nilivyoeleza ni kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na si kubomoa hata misingi yenyewe.
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,907
Likes
2,479
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,907 2,479 280
Nipo ndugu betlehem. Uko sahihi vijana tusitumike katika namna yoyote kwenye mambo ya kupasua Taifa. Kazi yetu kubwa kama nilivyoeleza ni kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na si hata misingi yenyewe.
Dah! ndugu yangu Alex uko sahihi tu ila nadhani hii changamoto ya ukosefu wa ajira pengine ndio kikwazo kikuu.Binafsi nimefanya kautafiti kidogo nikagundua changamoto ya ukosefu wa ajira, kwa kiwango kikubwa huwafanya vijana wawe tayari kufanya mission yeyote ilimradi tu wahakikishiwe kwamba kwa kutekeleza mission husika mkono, utaenda kinywani.Hii ni hatari kubwa.Haiyumkiniki kwa mfano kijana msomi kabisa unakuta kwa mfano anasambaza ujumbe kama huu "ndugu ....., katika wilaya fulani kuna mapambano makali kati ya watu wa dini .....na dini.....,Watu wa dini yetu ambayo ni......, washazidiwa na sasa wanashambuliwa sana.Saidia kwa kadiri uwezavyo watu wa dini......., na mungu atakulipa" (wala hata haieleweki tatizo ni nini na mtoa taarifa haoni kama ipo haja ya anaowapa taarifa kuwaeleza msingi wa tatizo kwanza).Hapo juu ni sms ambayo nimetumiwa juzi na mtu mwenye shahada ya kwanza ya elimu ya jamii.Imagine?
 
Uko sahihi. Hizi sms zinasambazwa na vijana wasomi usioweza kuwadhania. Ni changamoto wa TCRA kudhibiti usambazaji wa sms za chuki.
 
cataliya

cataliya

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2013
Messages
353
Likes
32
Points
45
Age
28
cataliya

cataliya

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2013
353 32 45
Tatizo vijana hawana kazi!!!
Ndo maana wanatumika katika mambo yasiyo na msingi!!
Wakubwa achieni vyeo hivyo mtupe vijana!!!
 
N

Naytsory

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
2,100
Likes
540
Points
280
N

Naytsory

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
2,100 540 280
Utawaona watumiaji propaganda hii watakavyokupinga na matusi kibao.
 
Ground Zero

Ground Zero

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Messages
342
Likes
0
Points
0
Ground Zero

Ground Zero

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2011
342 0 0
Dah! ndugu yangu Alex uko sahihi tu ila nadhani hii changamoto ya ukosefu wa ajira pengine ndio kikwazo kikuu.Binafsi nimefanya kautafiti kidogo nikagundua changamoto ya ukosefu wa ajira, kwa kiwango kikubwa huwafanya vijana wawe tayari kufanya mission yeyote ilimradi tu wahakikishiwe kwamba kwa kutekeleza mission husika mkono, utaenda kinywani.Hii ni hatari kubwa.Haiyumkiniki kwa mfano kijana msomi kabisa unakuta kwa mfano anasambaza ujumbe kama huu "ndugu ....., katika wilaya fulani kuna mapambano makali kati ya watu wa dini .....na dini.....,Watu wa dini yetu ambayo ni......, washazidiwa na sasa wanashambuliwa sana.Saidia kwa kadiri uwezavyo watu wa dini......., na mungu atakulipa" (wala hata haieleweki tatizo ni nini na mtoa taarifa haoni kama ipo haja ya anaowapa taarifa kuwaeleza msingi wa tatizo kwanza).Hapo juu ni sms ambayo nimetumiwa juzi na mtu mwenye shahada ya kwanza ya elimu ya jamii.Imagine?
ulimshauri nini?
 
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Messages
3,393
Likes
251
Points
160
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2013
3,393 251 160
Nikiona habari yoyote imeandikwa na tanzania daima hata kuisoma sitaki lazima itakuwa ya uzushi.
 
African American

African American

Senior Member
Joined
Feb 6, 2012
Messages
166
Likes
1
Points
0
African American

African American

Senior Member
Joined Feb 6, 2012
166 1 0
Sawa gazeti la UDAKU, ila katika maandishi yote hayo umeona maneno mawili tuu ambayo ni Tanzania Daima?hayo maneno mengine hujayaelewa kabisa?
umemaliza kila kitu
 
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
2,524
Likes
6
Points
135
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2013
2,524 6 135
Kaka hili ni jambo la msingi umelisema japo bado kuna vijana wanaotumika kisiasa wanaendelea kukupinga hapa. Vijana tubadilike kutumika hakuna tija yoyote sbb ukishamnufaisha mhusika anakutupa mbali...
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,252,123
Members 481,989
Posts 29,796,278