Vijana tusitumike kueneza udini

Status
Not open for further replies.
Mkuu siku nyengine ukiwa na makala unayotaka iwafikie jamii usitumie Tanzania Daima, Hili gazeti ni sawa na KIU,Uwazi ...etc Halina thamani katika jamii ya watu wenye heshima......

Mkuu pia kuna viongozi wa dini walio katika siasa lakini wanaendelea kuongoza nyumba mbali mbali za ibada, utategemea vipi waumini wa hawa watu wasijichanganye pale viongozi wao hawa wa kiroho wanapotaka kura za kuja "KUWATETEA"? Wimbi kubwa la maaskofu, mapadre, wachungaji kujiunga na vyama vya siasa , kuchukua uongozi wa kisiasa huku wakiendea kushikilia nyadhifa zao kwenye majumba ya ibada ndio kichocheo cha haya yote tunayoyaona..

Anyway mawazo yako si mabaya ingawa umeyatoa kwenye gazeti la UDAKU linaloendeshwa kwa hisia na mitazamo ya watu fulani..
 
umesema sawa kabisa, unajua haya mambo watu hawayaelewivzuri. wanaweza sema wanakibomoa chama furani,lakn mbegu hiiikimea sawasawa madhara yake ni makubwa mno. unajua ktk familia mnawezakugawanyika mwingne akawa chama hiki na mwingne kingne, unafikiri anajisikiaje unavyokipaka matope chama chake ambacho yy ni mfuasi wake.mwisho wa siku mambo yakiharibika mnaanza kupambana kwanza ndani humo humo. yusijiingize kwenye ubabaishaji huu.
 
Mi nadhani hapa Jf watu wamepewa uhuru mno wa kupiga propaganda chafu zenye malengo ya kukandamiza vyama vingine na kuvifanya vionekane ni vya kidini au kikabila, propaganda hii haiwezi kufa kama Mods wa jukwaa hili hawatakuwa wakali kwa kiwango cha kutosha kwa sababu kwa vyama vingine namna ya kushindana na Chama kinachokuwa kwa speed ni kukihusisha chama hicho na udini au ukanda, mods wafungie maisha wachochezi wa namna hiyo, itasaidia
 
Tatizo vijana hawana kazi!!!
Ndo maana wanatumika katika mambo yasiyo na msingi!!
Wakubwa achieni vyeo hivyo mtupe vijana!!!

Ukosefu w ajira ni changamoto ambayo sisi vijana tunatakiwa kuitaftia ufumbuzi.
Yatupasa kutumia elimu na uzoefu tulioupata vyuoni na kwenye familia/jamii tulizokulia kubuni mbinu (safi) za kukabiliana na ukosefu wa ajira.
Pia vijana tuache tamaa ya mafanikio ya haraka bila jasho kwani hiyo ndio sababu kubwa inayotufanya tukubali kutumika.
Tuwe na MAPENZI ya dhati kwa NCHI yetu kwani ndio nchi pekee tuliyonayo.
Tuki iharibu hatutakuwa na sehemu nyingine tutakayo iita kwetu.
SASA NI WAKATI WA KUWAAMBIA WABINAFSI "BASI YATOSHA" HATUTAKI KUTUMIKA.
 
Source: Tanzania Daima 12/12/2013
Sina muda wa kusoma udaku.
 
Source: Tanzania Daima 12/12/2013
Sina muda wa kusoma udaku.

Tanzania Daima mnamsema wazi wazi mkwe wa Mbowe hamuogopi kuwakuta yaliyomkuta Kibanda? Maana yeye Mzee Mtei ndio bingwa wa udini na ukabila!

Kila mtu anajua Hilo!
 
Mzee Mtei ni kinara mkubwa wa udini na ukabila! Kumbukeni maneno Mara tu baada ya kutajwa tume ya kukusanya maoni ya Katiba!
 
Pamoja na ukosefu wa ajira unaoleta umaskini lakini umaskini wa kwanza tulonao ni umaskini wa fikra mbaya zaid kwa kundi ambalo limepata nafasi ya kuupunguza huo umaskini wa fikra. Hata kama ww ni shabiki wa chama chako usikubali chama kikuvue akili yako na kukuacha mtupu kichwani na kubaki na fikra za kipuuzi kama udini na ukabila. Kwa yeyote aliekombolewa kifikra ambalo ndio lengo la kupata elimu, ukosefu wa kipato si changamoto ya kwanza, changamoto ya kwanza ni jinsi ya kutumia kile ulichonacho kama elimu, watu wanaokuzunguka na hata simu yako ya mkononi kama resource. Kijana mwenye Fikra Pevu kamwe hawezi kuwa vuvuzela la wanasiasa. Ukiona Kijana anatua na mwaasiasa tena kwa dhana hizi za kidin kikanda na kikabila huyo keshauza utu wake na kununua UTUMWA WA FIKRA
 
Hili ni suala gumu sana kwa Upande wa tanganyika kuweza kulitatua. Kwani kwa tuliowahi kuishi na hata kusoma UDSM miaka ya 70's na 80' hususan tuliokuwa tunatoka Zanzibar tulikuwa tunaliona hilo na lilikuwa linapandwa na kupaliliwa na uongozi wa juu na Serikali ya Tanganyika. na hata makazini kwa tuliobahatika kufanyia kazi afisi za bara tulikuwa tukiliona hilo.

Kwani ilizoeleka kuwa waislam hawakusoma hivyo kazi zao zilikuwa madereva, wafagizi na matarishi tu wakti wa upande mwingine ndio wenye vyeo vikubwa. Mimi ninakumbuka nikiwa wizara ya Fedha muungano ni waislam watatu tu ndio tuliokuwa na ofisi wengine wote madereva, wafagiaji na matarishi. Na hata nilipopelekwa mwanza hali ilikuwa hiyo hiyo.

sasa ili kuepuka hili ni vizuri kwa waTz wajijue kuwa wote ni waTz na mna haki sawa katika nchi yenu. Lakin pia ile DHANA KUWA DINI YETU NDIO WASOMI NA TUNASTAHILI VYEO VYOTE IONDOLEWE MIONGONI MWA VIJANA . iKIMBUKWE KUWA NA WAISLAM SASA WENGI WAMESOMA NA HIVYO WANA HAKI SAWA NA FURSA SAWA KATIKA KUPATA KAZI, VYEO NA UONGOZI.
Lakin mimi kwa mtazamo wangu upande wa Tanganyika sasa ni wakti wa kusikiliza malalamiko ya waislam na kuyafanyia kazi. Kwani kuyafumbia macho itakuwa yale yale ya Africa ya Kati. Kwani kwa sasa Znz ndio inayoibeba Tanganyika katika suala hili la udini. Kwani ukivunjika Muuungano tu lazima tifu la udini Bara litatokea kwa rasilimali zinaliwa na upande mmoja na upande mwingine unaishia kulalama bila kusikilizwa.
 
umesema sawa kabisa, unajua haya mambo watu hawayaelewivzuri. wanaweza sema wanakibomoa chama furani,lakn mbegu hiiikimea sawasawa madhara yake ni makubwa mno. unajua ktk familia mnawezakugawanyika mwingne akawa chama hiki na mwingne kingne, unafikiri anajisikiaje unavyokipaka matope chama chake ambacho yy ni mfuasi wake.mwisho wa siku mambo yakiharibika mnaanza kupambana kwanza ndani humo humo. yusijiingize kwenye ubabaishaji huu.

Naungana na hoja yako, ebu turejee nyuma kidogo wakati wa vuguvugu za kisiasa Zanzibar! wanachama wa ccm na Cuf ambao ni ndugu kabisa wa tumbo moja walikuwa hawazikani, vijana katika hili tunapaswa kujitazama upya kama tupo sahihi , kuweka vyama vyetu mbele maslahi ya Taifa nyuma, hatujachelewa tuanze sasa kukataa kutumika. Safi mleta uzi kwa hoja yako.
 
Naungana na hoja yako, ebu turejee nyuma kidogo wakati wa vuguvugu za kisiasa Zanzibar! wanachama wa ccm na Cuf ambao ni ndugu kabisa wa tumbo moja walikuwa hawazikani, vijana katika hili tunapaswa kujitazama upya kama tupo sahihi , kuweka vyama vyetu mbele maslahi ya Taifa nyuma, hatujachelewa tuanze sasa kukataa kutumika. Safi mleta uzi kwa hoja yako.

Nashukuru. Nimependa rai yako na natumaini vijana wamekusoma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom