Vijana tuijenge Afrika yetu

Vijana tuijenge Afrika yetu

Hekima94

Member
Joined
Mar 16, 2017
Posts
32
Reaction score
91
Habari Wakuu,

Kwanza nitangulize shukrani zangu kwa MUNGU muweza wa yote kwa kuwa hapa muda huu na kushare na nyinyi mawazo haya.

Vijana wenzangu sisi ndio tupo wengi katika nchi zetu hususani Tanzania hivyo basi kama tukiamua kuchukua hatua yoyote ile ya kimaendeleo tunaweza kufanikiwa sana.

Lakini mabadiliko huanzia ndani kwenda nje hivyo basi kwanza tujitahidi kujijenga wenyewe kifikra ndiyo tuweze kusonga mbele.

Huwezi kujenga nyumba kama hujaandaa ardhi vizuri kwa kuchimba msingi mzuri namaanisha tuziweke akili zetu tayari kwa kufanya maendeleo.

1. Tutoe fikra za kikoloni vichwani mwetu, unachofundishwa kuhusu Afrika ni sehemu ndogo sana ya ukweli halisi kwa hiyo soma sana makala na vitabu mbalimbali kujua ukweli halisi.

2. Tutumie vizuri simu zetu haswa smartphones, tutumie muda mwingi kujifunza vitu vipya vyenye tija katika maisha yetu mfano: Unaweza ukaamua kusoma makampuni mbalimbali katika sekta yako yanayopatikana nchi ya jirani. Hapa utajifunza vingi sana.

3. LOVE au UPENDO, utajiuliza imekuwaje tena nimeliingizia hili suala. Nguzo kuu ya amani ulimwenguni kote ni Upendo yaani ukiwa na unampenda binaadamu mwenzako huwezi mtendea uovu hivyo matatizo ya dunia hii yanasababishwa na chuki, ubinafsi yaani kukosa upendo mioyoni mwetu na njia nzuri ya kukuza upendo ni kuangalia mtu au kitu bila kukihukumu mfano: Mtu amekutukana, usikubali kukasirika narudia usikubali kukasirika maana husababisha akili ikudai hukumu kutokana na hasira alizokupa na kusababisha maamuzi ya hovyo lakini ukitulia na kupotezea narudia jitahidi kupotezea utajikuta mwenye amani sanaa..
 
Well vijana wapo jukwaa la mapenzi kulilia kupendwa.

Unashauri tuijenge vipi Africa.
Kabla ya kuanza kujenga unatakiwa ujue nini chanzo cha kutokuendelea kwa ujenzi wa africa.
Unahauri tufocus kwenye nyanja ipi ili tukuze uchumi wetu?

At least there's someone who thinks like me.
 
Tuanze kwa kujaza vichwa vyetu positivity yaani tuache wivu na roho mbaya unajua kuna tabia fulani ya kutopenda maendeleo ya mwengine ambalo lipo kuanzia ngazi za familia mpaka maofisini hii inarudisha sana nyuma maendeleo ifike wakati ufungue moyo na kuamini kwamba maendeleo ya mwenzako ni maendeleo yako pia hata kama hatokupa kitu wewe...

KNOWLEDGE yaani knowledge is power sana wazungu wametuletea vitu vingi vinavyotupunguzia uwezo wa kufikiri hasa Tv programs, pia baadhi ya wasanii wanapewa agenda kama vile kukaa uchi kwenye video hii imewafanya wengi kuwaza sex badala ya vitu vya msingi na mfano mzuri ni dada zetu siku hizi hawataki kazi wanawaza kudanga kwasababu vitu wanavyovitaka wameviona kwenye TV na haviendani na uwezo wao in the end wanatumia sex ambayo kimsingi Mungu aliileta kwa ajili ya Reproduction tu na sio starehe the same kwa sisi wakaka tunawaza tukipata pesa ni kugongana tu. Ukitaka kuona utofauti we ingia vijijini jaribu kuwasoma maisha yao utagundua jinsi wanawake wanavyojituma na wakaka wanavyowahi kujitegemea...

UZALENDO hapa naomba vijana waachane na propaganda za kisiasa na kuitanguliza nchi mbele na ukitaka usiendeshwe na wanasiasa we kuwa tayari kujifunza na kufuatilia habari za ulimwengu mzima kisha tulia zichakate vizuri pia usipende kuchagua upande hii inakufanya ushindwe kufikiria vizuri na kufanya maamuzi sahii. Hakikisha unapitia taarifa nyingi iwezekanavyo kabla ya kuaminishwa kitu na mwanasiasa yoyote na pia ukiwa unaijua nchi yako vizuri yaani namaanisha unasoma bajeti, uongozi na historia za viongozi, elimu, ulinzi na usalama wa nchi. Hii tabia itakuweka mahali salama....

UCHUMI hapa namaanisha ili kukuza uchumi wa nchi ni lazima tujitolee kufanya kazi kwa jasho kila mtu kwa nafasi yake bila kujali nani anafanya nini. Kwanza tujivunie nchi yetu Vijana kuna mikopo inatolewa kwa vikundi vya vijana tena ni mamilioni ya mapesa mimi nina ushahidi watu wamechukua hundreds of Millions kuanzisha miradi na sasa hivi wanamaendeleo mazuri na wanapeleka marejesho LAKINI changamoto yetu kubwa vijana hatupendi kufuatilia vitu vya msingi tunauoga wa kuongea na viongozi lakini kwenye ujinga na ushabiki tupo faster sana so tuanze kufuatilia wapi pakutoa mitaji pili tujitahidi kushirikiana kwa kuzingatia vipengele nilivyotaja hapo juu.

Mambo yapo mengi lakini tuanze taratibu na tutafika.
 
Tuanze kwa kujaza vichwa vyetu positivity yaani tuache wivu na roho mbaya unajua kuna tabia fulani ya kutopenda maendeleo ya mwengine ambalo lipo kuanzia ngazi za familia mpaka maofisini hii inarudisha sana nyuma maendeleo ifike wakati ufungue moyo na kuamini kwamba maendeleo ya mwenzako ni maendeleo yako pia hata kama hatokupa kitu wewe...

KNOWLEDGE yaani knowledge is power sana wazungu wametuletea vitu vingi vinavyotupunguzia uwezo wa kufikiri hasa Tv programs, pia baadhi ya wasanii wanapewa agenda kama vile kukaa uchi kwenye video hii imewafanya wengi kuwaza sex badala ya vitu vya msingi na mfano mzuri ni dada zetu siku hizi hawataki kazi wanawaza kudanga kwasababu vitu wanavyovitaka wameviona kwenye TV na haviendani na uwezo wao in the end wanatumia sex ambayo kimsingi Mungu aliileta kwa ajili ya Reproduction tu na sio starehe the same kwa sisi wakaka tunawaza tukipata pesa ni kugongana tu. Ukitaka kuona utofauti we ingia vijijini jaribu kuwasoma maisha yao utagundua jinsi wanawake wanavyojituma na wakaka wanavyowahi kujitegemea...

UZALENDO hapa naomba vijana waachane na propaganda za kisiasa na kuitanguliza nchi mbele na ukitaka usiendeshwe na wanasiasa we kuwa tayari kujifunza na kufuatilia habari za ulimwengu mzima kisha tulia zichakate vizuri pia usipende kuchagua upande hii inakufanya ushindwe kufikiria vizuri na kufanya maamuzi sahii. Hakikisha unapitia taarifa nyingi iwezekanavyo kabla ya kuaminishwa kitu na mwanasiasa yoyote na pia ukiwa unaijua nchi yako vizuri yaani namaanisha unasoma bajeti, uongozi na historia za viongozi, elimu, ulinzi na usalama wa nchi. Hii tabia itakuweka mahali salama....

UCHUMI hapa namaanisha ili kukuza uchumi wa nchi ni lazima tujitolee kufanya kazi kwa jasho kila mtu kwa nafasi yake bila kujali nani anafanya nini. Kwanza tujivunie nchi yetu Vijana kuna mikopo inatolewa kwa vikundi vya vijana tena ni mamilioni ya mapesa mimi nina ushahidi watu wamechukua hundreds of Millions kuanzisha miradi na sasa hivi wanamaendeleo mazuri na wanapeleka marejesho LAKINI changamoto yetu kubwa vijana hatupendi kufuatilia vitu vya msingi tunauoga wa kuongea na viongozi lakini kwenye ujinga na ushabiki tupo faster sana so tuanze kufuatilia wapi pakutoa mitaji pili tujitahidi kushirikiana kwa kuzingatia vipengele nilivyotaja hapo juu...

Mambo yapo mengi lakini tuanze taratibu na tutafika.

Mkuu umesema 'UZALENDO hapa naomba vijana waachane na propaganda za kisiasa na kuitanguliza nchi mbele'.

Naona hapo chini afisa elimu akitanguliza maslahi ya taifa mbele.

tapatalk_1577354951190.jpg
 
Tuanze kwa kuondoa vibabu vihafidhina kama Magufuli na Kabudi madarakani, vikongwe hivi fikra zao ni za karne ya 20 ya kupambania ukombozi, havitufai na vinaturudisha nyuma.
 
Mkuu umesema 'UZALENDO hapa naomba vijana waachane na propaganda za kisiasa na kuitanguliza nchi mbele'.

Naona hapo chini afisa elimu akitanguliza maslahi ya taifa mbele.

View attachment 1548498

Mkuu
Kwanza kabisa kama unajua sheria huwezi kuyumbishwa na kauli kama hizi.. hata anayesema hivyo ni Afisa elimu ambaye mamlaka yake ni madogo sana.
Nasisitiza tusome sana tujaze vichwa vyetu KNOWLEDGE na tutumie BUSARA daima.

KUJIAMINI/CONFIDENCE ukiwa unajua unachokifanya na unauhakika nacho basi hakuna anayeweza kukuyumbisha.
Kama wewe ni mwalimu unatimiza majukumu yako na huna tatizo lolote basi ukiona kauli kama hizi una smile halafu unaendelea na maisha yako.
Wakati mwingine kwenye maisha sio lazima kujibu kila kitu na pia unapomjibu mtu uliyemzidi uwezo wa kufikiri yeye ndiye anayefaidika na kunyonya wewe ila wewe hupati faida zaidi ya kupoteza muda.
Kamwe usitumie hasira maana hasira inamuumiza anayekasirika kuliko aliyekasirikiwa.
Tuliza akili.
 
Tuanze kwa kuondoa vibabu vihafidhina kama Magufuli na Kabudi madarakani, vikongwe hivi fikra zao ni za karne ya 20 ya kupambania ukombozi, havitufai na vinaturudisha nyuma.

Mkuu Samahani kidogo.
Nakushauri urudi kusoma Historia ya nchi kuanzia kipindi cha kabla ya kuja wakoloni babu zetu waliishi vipi, wakoloni walikuja kwa style gani, kipindi cha ukoloni kilikuwaje mateso manyanyaso utumwa dini zilivyokuja biashara elimu ulinzi na usalama, harakati za ukombozi wa nchi, Uhuru wa nchi, Uongozi wa nyerere Mwinyi Late Mkapa Kikwete na Magufuli maendeleo na changamoto zao.
Ukitoka hapo kasome jinsi mataifa makubwa ya ulimwengu yanavyoendesha dunia na kutawala kwa ukoloni mambo leo na njia wanazotumia kuleta machafuko kwenye nchi mbalimbali.
Jaribu kuzunguka nchi nzima ya Tanzania kama unaweza halafu toka hapa nenda nchi yoyote ile ya jirani kakae hata mwezi mmoja ukirudi utajifunza kitu.
Kwenye maisha ni ngumu kupata exactly unachokitaka hivyo tunatakiwa kukipenda tulichonacho.
Vitu anavyofanya JPM ni vikubwa sana na vingine unaweza usione faida yake leo lakini vizazi vijavyo vitafaidika na Barabara, Mahospitali ya kisasa, Masoko ya kisasa, Mashule, Umeme, Maji, Miji ya kisasa, Ulinzi na Usalama, Mashule, Airports na vingine vingi.
WATANZANIA WENZANGU TUTULIE TUIJENGE NCHI.
KILA RAIS ATAKUJA NA CHANGAMOTO ZAKE HIVYO TUCHAGUE NCHI KWANZA.
 
Back
Top Bottom