Vijana tuepuke sana kulewa na mambo haya matano

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
Vijana tuepuke sana kulewa na mambo haya matano,

1.Nguvu/Mamlaka/Madaraka/Cheo (Power),

2. Vitu (Property),

3. Ufahari (Prestige),

4. Umaarufu (Popularity) na,

5. Mbwembwe (Pomposity).

Vimeangusha watu wengi sana kabla ya kufikia hata malengo yao.

Usijiona leo una mamlaka na ungali kijana ukaanza kujiona wewe ndo wewe. Ukaanza dharau na kujiona hutoshuka kwani Wahenga walinena kwamba Uongozi ni Dhamana.

Usijione kwamba leo una mafanikio sana kisa unamiliki nyumba na magari na kuanza kulewa na vitu hivyo, kuwa makini sana kwani sifa hizo za kupitiliza ukishuka huwa ni kiama.

Kuwa makini sana wala usilewe na ufahari mpaka ukaona wewe ndo wewe kwani huijui kesho.

Kuwa makini na umaarufu ulionao leo kwani ukiutumia hovyo kisa wewe ni maarufu sana utakuja kushuka chini na utapata shida.

Punguza mbwembwe kwani huumiza, mbwebwe husababisha mambo mengi ya hovyo usipokuwa makini.

Jambo la muhimu sana ni hili, ukiwa juu au chini ya mafanikio yako usiache kumweshimu kila mtu. Tafuta hekima na busara angali ukiwa kijana kwani vitakusaidia sana kutolewa na mambo hayo niliyoyataja hapo juu.

S. N.Jilala
27/11/2017
 
Mimi nilizani utasema na kuiunga CHADEMA,kwa sababu ni katika mambo ya hatari sana katika awamu hii,kushinda hawatashinda,utalala kwa wasiwasi,ukiona Nisan nyeupe utajinyea,kwa kweli ni hatari.
 
Back
Top Bottom